Hatima ya Ubunge wa Chenge baada ya hukumu

Mkuu nadhani hatuwezi kumwita mfungwa kwa kuwa hukumu ilimpa uchaguzi wa kifungo au faini.

Cha muhimu hapo ni kuwa alikutwa na kosa na alihukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi sita.

Hilo ndilo kikwazo kwa ubunge wake.
=======
Mheshimiwa
Chenge alipewa adhabu ya kifungo au faini, akalipa faini.
Kwa maana nyingine kifungo na faini vina hadhi na uzito sawa.
Unaweza kukiita kifungo kuwa faini au faini kuiita kifungo.
Naendelea kuamini kuwa Chenge yuko kifungoni.
 
I see
 
No. 67 (2)
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.

Wakuu kuna hiyo phrase ya mwisho nahisi kama inamlinda. Sidhani kama amekutwa hatiani kwa kosa linalo husu utovu wa uaminifu.
 
Uaminifu mana yake nini? Unapoendesha gari bila Insurance unataka uaminiwe au tubadili maana ya uaminifu? Yaani kwa hadhi aliyonayo its unbelievable lakini Ujambazi na ufisadi huenda sambamba na Wizi.

Khe khe Chama Cha Majambazi wamelikoroga walinywe sasa. Chenge siyo mbunge tena sheria iko wazi labda kama wanataka kuchakachua na hilo chini ya rais Mwizi.
 
Hapo kazi ipo. ngoja wanasheria watusaidie!! Tukifanikiwa kumwangusha na kumtoa kwenye ubunge huyu mwizi, hakika itabidi tufanye tafrija hapa JF!!

Eti anajiita 'Rais wa Afrika', ama kweli fedha za wizi zinamtia jeuri!!
 
Nangoja nione jinsi walio madarakani watakavyofanya.

Wakati wa ugombea uspika walimsafisha Chenge hata tuhuma za RADA mpaka serikali ya Uingereza ikaingilia.

Tuone kama wana ubavu wa kukiweka kifungu hiki cha KATIBA katika katika matendo.

Nani wa kumfunga Paka Kengele??????????????? Haya lets wait and see....!!!:embarrassed:
 
JAMENI NAOMBENI MSAADA NATAKA KUBADILI ID YANGU HUMU MAANA naona kuna mkongwe mwingine mwenye ID sawa na yangu.
NI click au kugonga wapi???? maana nimejaribu kwenye setting na profile sijaona.
 
JAMENI NAOMBENI MSAADA NATAKA KUBADILI ID YANGU HUMU MAANA naona kuna mkongwe mwingine mwenye ID sawa na yangu.
NI click au kugonga wapi???? maana nimejaribu kwenye setting na profile sijaona.

Mtumie PM Invisible ........ ...... wewe mgeni?
 
No. 67 (2)
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.

Wakuu kuna hiyo phrase ya mwisho nahisi kama inamlinda. Sidhani kama amekutwa hatiani kwa kosa linalo husu utovu wa uaminifu.

Kwa hapa anaweza kuchomoa kwani makosa yote manne aliyokutwa na hatia hayahusiani na 'utovu wa nidhamu'. Makosa hayo ni;
1. kuendesha gari kwa uzembe
2. Kusababisha vifo vya watu wawili
3. kuharibu mali
4. kuendesha gari isiyokuwa na bima
 
Chenge hawezi kuendelea kuwa mbunge kutokana na vifungu vifuatavyo kwenye katiba.

Section 71.-(1)(a) A Member of Parliament shall cease to be Member of Parliament and shall vacate his seat in National Assembly upon the occurrence of any of following matters:

(a) where anything happens which, had he not been a Member of Parliament would have disqualified him from election, or would make him lose the qualifications for election, or would disqualify him from election or appointment in accordance with the provisions of this Constitution;

Section 67(2) -
A person shall not be qualified to be elected or appointed Member of Parliament if-
(c) such person has been convicted by any court in the United Republic and sentenced to death or to a term of imprisonment exceeding six months for a conviction of any offence however, styled involving dishonesty;

Huyu ni mfungwa kwa option ya kulipa faini. Kama angepewa kifungo cha nje ungelisemaje, kuwa hakufungwa kwa vile tunae uraiani na hivyo kuendelea kuwa mbunge
 
kumbe hapa wengi hamuwezi kutafsiri katiba. ni kosa la kukosa uaminifu ndilo linaongelewa. rage asingeliweza kugombea. mzee wa visenti pamoja na kuhukumiwa ataendelea kuwa mbunge. katiba mbovu hii tubadilishe

hata ukilipa bado unaendelea kuhesabiwa umehukumiwa kifungo. anapona kwasababu ya hilo la kosa la kukosa uaminifu
 
Katiba iko wazi, kifungo kinachomwondolea mtu sifa za kuwa mbunge ni kile tu kinachotokana na kosa la ukosefu wa uaminifu. wana JF mtakubaliana na mimi kuwa kosa la Chenge alihusiani na ukosefu wa uaminifu, hivyo kifungo chake akihathiri kwa namna yeyote ile ubunge wake.
 
Hapo kazi ipo. ngoja wanasheria watusaidie!! Tukifanikiwa kumwangusha na kumtoa kwenye ubunge huyu mwizi, hakika itabidi tufanye tafrija hapa JF!!

Eti anajiita 'Rais wa Afrika', ama kweli fedha za wizi zinamtia jeuri!!

Sikuelewa kwanini kajiita hivyo au ndo kutuonyesha jeuri kwamba yeye ni Un-touchable
 
Hili swala haliitaji kusubiri serikali ifanye kazi lintakiwa lifanyiwe kazi na wabunge wa upinzani na bunge litakapoanza mara moja wanyooshe vidole na kuomba mwongozo wa spika.
Mi nakumbuka mrema aliwahi kufukuzwa bungeni na uchaguzi ukarudiwa so why NOT Chenge??? Tena mwizi kama huyu??
 
kumbe hapa wengi hamuwezi kutafsiri katiba. ni kosa la kukosa uaminifu ndilo linaongelewa. rage asingeliweza kugombea. mzee wa visenti pamoja na kuhukumiwa ataendelea kuwa mbunge. katiba mbovu hii tubadilishe

hata ukilipa bado unaendelea kuhesabiwa umehukumiwa kifungo. anapona kwasababu ya hilo la kosa la kukosa uaminifu

Chenge hawezi kuchomoka hapa kwani aliendesha gari ambalo halikuwa na BIMA; hilo ni kosa la kutokuwa mwaminifu!!
 
Sifa za mtu
kuwa Mbunge
Sheria ya
1984 Na.15
ib.13
Sheria ya
1992 Na.4
ib.19 Sheria
ya 1994 Na.34
ib.13 Sheria
ya 1995 Na.12
ib.10
Sheria ya
2000
Na.3 ib.12​
67​
.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyomo katika ibara hii, mtu
yeyote atakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa
kuwa Mbunge endapo-
(a) ni raia wa Jamhuri ya Muungano aliyetimiza umri wa
miaka ishirini na moja, na ambaye anajua kusoma na
kuandika katika Kiswahili au Kiingereza;
(b) ni mwanachama na ni mgombea aliyependekezwa na
chama cha siasa;
(c) katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe ya
Uchaguzi hakuwahi kutiwa hatiani katika mahakama
yoyote kwa kosa lolote la kukwepa kulipa kodi yoyote
ya Serikali.
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa
kuwa Mbunge-
(a) ikiwa mtu huyo anao au kwa hiari yake amejipatia
uraia wa nchi nyingine yote; au
(b) ikiwa kwa mujibu wa sheria inayotumika katika
Jamhuri ya Muungano imethibitishwa rasmi kwamba
mtu huyo ana ugonjwa wa akili; au
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote
katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya
kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi
miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote,
vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa
uaminifu; au
(d) ikiwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe
ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa
adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu
wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya Maadili ya
Viongozi wa Umma;
(e) bila ya kuingilia haki na uhuru wa mtu kuwa na maoni
yake, kuamini dini atakayo, kushirikiana na wengine
na kushiriki shughuli za umma kwa mujibu wa sheria
za nchi, ikiwa mtu huyo si mwanachama na mgombea
aliyependekezwa na chama cha siasa;
(f) ikiwa mtu huyo ana masilahi yoyote katika mkataba wa
Serikali wa aina yoyote aliyowekewa miiko maalum
kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge, na iwapo
amekiuka miiko hiyo;
(g) ikiwa mtu huyo ameshika madaraka ya afisa
mwandamizi katika utumishi wa Serikali ya Jamhuri ya
Muungano, isipokuwa madaraka ambayo Rais aweza
au anatakiwa kukabidhi kwa Mbunge kwa mujibu wa
Katiba hii au sheria iliyotungwa na Bunge;
(h) ikiwa kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
_________________________________________________________________​
53​
inayoshughulikia makosa yanayohusika na uchaguzi
wa aina yoyote mtu huyo amezuiliwa kujiandikisha
kama mpiga kura au kupiga kura katika uchaguzi wa
Wabunge.
(3) Mtu hataweza kugombea uchaguzi kuwa Mbunge wa
kuwakilisha jimbo la uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu wowote ikiwa
wakati huo yeye amesimama katika uchaguzi kugombea kiti cha
Rais, wala hataweza kugombea uchaguzi kuwa Mbunge katika
uchaguzi mdogo wowote ikiwa yeye ni Rais.
(4) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka masharti
yatakayomzuia mtu asichaguliwe kuwa Mbuge wa kuwakilisha
jimbo la uchaguzi ikiwa mtu huyo ni mwenye madaraka
yanayohusika na shughuli za kuongoza au kusimamia uchaguzi
wa Wabunge au shughuli za uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili
ya uchaguzi wa Wabungel isipokuwa kwamba Sheria kama hiyo
haiwezi kuweka masharti yatakayomzuia Spika wa Bunge
asichaguliwe kuwa Mbunge wa kuwakilisha wilaya ya uchaguzi,
wala masharti yatakayosababisha mtu aliyechaguliwa kuwa Spika
kupoteza kiti hicho cha Spika au kiti chake cha kawaida katika
Bunge.
(5) Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka masharti
yatakayomuzia mtu asichaguliwe kuwa Mbunge wa kuwakilisha
wilaya ya uchaguzi kwa muda wowote utakaotajwa na Bunge (ili
mradi muda huo usizidi miaka mitano) ikiwa mtu huyo atapatikana
na hatia mbele ya mahakama kwa ajili ya aina yoyote ya makosa
yatakayotajwa katika Sheria hiyo yanayohusika na uchaguzi wa
Wabunge.
(6) Kwa madhumuni ya kutoa fursa ya kukata rufaa kwa
mujibu wa Sheria kwa mtu yeyote aliyethibitishwa rasmi kisheria
kuwa ana ugonjwa wa akili au aliyehukumiwa na kupewa adhabu
ya kifo au ya kufungwa gerezani au aliyepatikana na hatia ya kosa
lolote lililotajwa katika Sheria kwa mujibu wa ibara ndogo ya (5) ya
ibara hii, Bunge laweza kutunga Sheria kwa ajili ya kuweka
masharti yatakayoeleza kwamba hiyo hukumu inayopingwa na
mtu huyo haitakuwa na nguvu kwa ajili ya utekelezaji wa masharti
ya ibara ndogo ya (2) au ya (5) ya ibara hii mpaka upite kwanza
muda utakaotajwa katika sheria hiyo.
(7) Kanuni zifuatazo zitatumika kwa ajili ya ufafanuzi wa aya
ya ( c), ya (d) na ya (e) za ibara ndogo ya (2) ya ibara hii, yaani-
(a) ikiwa mtu amepewa adhabu mbili au zaidi za
kufungwa gerezani na imeamuliwa afungwe kwa muda
wa mfululizo, basi adhabu hizo zitahesabiwa kama ni
adhabu mbalimbali iwapo muda uliotajwa katika kila
moja ya adhabu hizo hauzidi miezi sita; lakini iwapo
muda uliotajwa katika adhabu yoyote kati ya adhabu
hizo unazidi miezi sita basi adhabu hizo zote​
zitahesabiwa kama ni adhabu moja;
 
siyo kuwa na bima tu na lessen yake ulikuwa imeisha muda mrefu hivyo alishiriki kuibia TRA

na hili tu linamaliza
labda afanye janja ya Rage kuapili

(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote
katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya
kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi
miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote,
vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa
uaminifu; au
(d) ikiwa katika kipindi cha miaka mitano kabla ya tarehe
ya Uchaguzi Mkuu amepata kuhukumiwa na kupewa
adhabu ya kifungo kwa kosa linaloambatana na utovu
wa uaminifu au kwa kuvunja sheria ya Maadili ya
Viongozi wa Umma;
 
Kwa mantiki ya wasemaji hapo juu ni kuwa, Chenge kwa sasa ni mfungwa, yuko kifungoni, si mbunge na jimbo liko wazi.

Hii inanifanya niwashtukie waandishi wetu wa habari kwamba hawasomi katiba. Hakuna gazeti hata moja la leo lililoandika juu ya implications za hukumu hii.

Criminal Chenge yuko mitaani kama mfungwa, hatakiwi kwenda bungeni, na akienda tuandamane na kupigwa mabomu.

Kijana naomba ujue tofauti kati ya hatia(conviction) na (sentence), change amekutwa na hatia na haifutiki, ila c mfungwa kwani ameshatumikia adhabu yake kwa kulipa faini, adhabu ilitolewa kwa option, na sio kutumikia kwa pamoja....... so chenge is free but a convict.

2-Kuhusu jambo la Chenge, hapa lazima tujue kuwa katiba hajazungumzia circumstances kama za Chenge, ila inazungumzia kuwa kabla ya kupata haki ya kugombea , ikiwa umeshahukumiwa then haki hiyo inaceas sasa hili la Chenge , mwenye mamlaka ya kulishughulikia hili ni High Court of Tanzania , watu wafungue shauri la madai juu ya tafsiri ya Article 67, huku chenge awekewe court injuction.......... kwa sasa mtapiga kelel lakini yule ni mwanasheria na anajua hajavunja kifungu chochote cha katiba
 
Back
Top Bottom