Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,786
- 1,710
Nimeangalia katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na nimeona hivi kuhusiana na hali inayofanana na hii aliyo nayo Mh. Chenge.
Ibara ya 67
(2) Mtu hatakuwa na sifa za kustahili kuchaguliwa au kuteuliwa kuwa Mbunge-
(c) ikiwa mtu huyo amehukumiwa na Mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.
Chenge amekutwa na hatia na amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu au faini 700,000Sh.
Sasa hatima ya Chenge inakuwaje baada ya hukumu hiyo?
Naomba wataalamu wa Sheria na katiba mtufafanulie vizuri.