Dumas the terrible
JF-Expert Member
- Jan 20, 2021
- 4,104
- 8,339
Salamu wakuu,
Poleni na changamoto za January naamini zitapita tu Kama upepo wa kisulisuli
Husika na kichwa cha habari hapo juu,
Katika hali ya kushangaza na kustaajabisha kama sio kukera sana ni suala la makondakta wa Daladala kuwanyanyasa wanafunzi waendapo shuleni asubuhi na jioni wakati wa kurudi.
Kuna tabia ya ajabu nimeishuhudia hapa Tegeta kwa Ndevu watoto wakizuiliwa kupanda Daladala za kwenda mjini kwa kisingizio limejaza huku wakiruhusu watu wazima.
Vilevile katika hatua hiyo watoto wanapogombania kupanda husukumwa vibaya na makondakta hao na kuanguka na kusabasha majeraha na hatari kubwa bila huruma.
Kikubwa cha kushangaza ni abiria wa Tegeta kukaa kimya kama hawaoni sababu ya ubinafsi mkubwa. Note: Hakuna raia wa ajabu Kama wa hii Bagamoyo road ni watu wasiojali tofauti na wa Buza wenye ushirikiano mkubwa na umoja.
Ifike mahali Watanzania tubadilike Kama tusipojali Mambo madogo makubwa yatatupiga mweleka.
Imagine hawa watoto wanajengewa roho mbaya na kutokujali siku wakija kua viongozi wasipojali maslahi ya wengi tusilaumu maana Mtu roho mbaya haziliwi nayo Bali hujifunza hapa hapa.
Imagine watoto wanaosukumwa waje kua Trafiki mbeleni halafu waaanze kuwafanyia roho mbaya msije mkalaumu.
Kesho yetu hujengwa na leo Makondakta mbadilike muwe na huruma. Vilevile napendekeza wahusika hasa kitengo cha usalama barabarani tunaomba angalau kwenye vituo vya Daladala kuwe na Askari maalumu wa kuwasaidia watoto Hawa maana huteseka Sana bila msaada!
The terrible!