Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,837
Mkuu Barbarosa unajua asili ya jina lako? Tuache hilo kwa sasa, ni kweli Edward akiondoka CCM atakuwa adui wa dola isipokuwa jua kitu kimoja dola yenyewe haipo pamoja katika hili, ni dola iliyogawanyika na mgawanyiko upo kwa ndani, ni ngumu kujua nani wa kumuamini.
Kuhusu foreigh powers (Uchina, Marekani na Ulaya) hawa wana maslahi yao na bado hayatishiwi kwa Lowasa na UKAWA kuingia madaraki. These powers would only act against the move kama maslahi yao yatatishiwa. Hawaipendi CCM kwa sababu ni CCM wanaipenda kwa sababu inalinda maslahi yao. Hata hivyo mahusioano yao si mazuri kama uanavyotaka kutuaminisha kwa mfano walisimamisha misaada kwa budget hivi karibuni CCM kamasi zikawatoka.
Hili la dola kukaa kimya ndio itakuwa inapiga hesabu zake, je zitakuwa na tija - time will tell ila siasa lazima hesabu kama dola inavyopiga hesabu ana the other side inapiga hesabu vivyo hivyo. Siasa ni kama mchezo wa chess kuna moves na counter moves mkuu.
Shida iko hapa Watu wa CHADEMA/Lowasa siku zote wanawaza yaliyoikuta KANU ndiyo yataikuta CCM kitu ambacho hakiwezi kutokea kwa maana tuna mazingira tofauti (Kenya na TanZania)!
Hivyo basi kitu pekee ambacho Bw.Lowasa na watu wake wanaweza kufanya ni kutumia fedha nyingi walizo nazo au kwa kifupi kununua washabiki ili wawachague na hapa ndipo tatizo litakapokuja kwa maana ni watu ambao hawasukumwi na sababu za Kiitikadi ideology, imani ya kidini, au kiethnic bali wanasukumwa tu kupewa pesa sasa mtu wa hivi siyo hatari sana na anaweza kukugeuka wakati wowote ule na hapo ndipo Dola ya CCM itakapocheza kwani mfumo wa fedha TanZania uko chini ya Serikali na unaweza kudhibitiwa wakati wowote!
Ngoja nikuulize swali dogo tu kwa mfano Serikali wakisema kesho Bw.Lowasa ana kesi ya kujibu kuhusu Richmond hivyo anatakiwa afike mahakamni Bw.Lowasa atafanya nini? Unafikiri kuna Mtz kutoka Karagwe au Tunduru atakayeingia barabarani kupinga kushitakiwa kwa Lowasa na awe tayari kuumia na kufa hata baada ya kuona wenzake wachache walioumizwa na Polisi?
Kuhusu Marekani, Uchina na Ulaya nilichomaanisha ni kwamba TanZania ni kipenzi cha Wazungu na mpaka sasa hivi hivyo kama Serikali ikimkamata Bw.Lowasa na kumfungulia mashitaka Wazungu au Wachina hawawezi kuingilia swala la escrow Wazungu waligoma kwa sababu fedha zao ndio zilizoibwa na walizitaka lkn siyo kwa sababu ya fedha za Mtz!
Hivyo kwa kifupi Bw.Lowasa hana uwezo wa kuwa Raisi wa JMT nje ya CCM na kama anaamini hivyo atakuwa siyo intelligent man kama mnavyomdhania kwanza hata watu hana kwa maana kama angekuwa nao tungeona maandamano nchi nzima pale tu alipokatwa jina lkn mimi nilikuwepo mitaani hata hao waliokuwa wanamshabika walivyosikia amekatwa wote wakahamia kwa Magufuli na kuendelea kunywa bia!
Sasa hii ni tofauti na Kenya, Raila baada ya Kibaki kutangazwa mshindi tayari Wajaluo wote wakaingia barabarani, sasa ni kwa nini?
Ni sababu ya ethnicity ambayo Bw.Lowasa hana zaidi ya fedha ambazo hata nyingi siyo zake na usifikiri CCM hawajui chanzo cha hizo fedha wanajua na swali ni Je, hawa wanaotoa hizo fedha wako tayari kugombana na Serikali na mfuomo wake wote?