Hatari ya mafanikio - CHADEMA/UKAWA & Lowassa

Hatari ya mafanikio - CHADEMA/UKAWA & Lowassa

Kwa utumbo ulioharisha hapa na uhakika hujui maana ya demokrasia, tanzania hakuna udikiteta na demokrasia vilevile hakuna. Ila kwa akili zako nimekuona wewe unapoana hakuna udikiteta unaita ni demokrasia aibu ilioje hii? Nenda kajifue upya uje utueleze demokrasia ni nini?

Blac Kid katika jamvi la weledi hoja hujibiwa kwa hoja, hoja dhaifu huangushwa na hoja yenye nguvu Barbarosa amejenga hoja yake, ameipanga, kama wewe unaamini na kujua kuwa hoja yake ni dhaifu basi jenga hoja yenye nguvu na si kufanya haya uliyoyafanya, umetukana halafu hujasema kitu. Eleza unachokifahamu wewe kuhusu demokrasia, eleza kwa nini unadhani hakuna demokrasia na demokrasia gani ungeitaka wewe maana kuna demokrasia za aina nyingi. Pengine demokrasia anayoizungumzia Barbarosa si ile unayoitaka wewe, mi naona hicho ndio kingekuwa kipimo bora kabisa cha kupima akili za mwanajamvi mwenzako kuliko kuhamaki na kujionesha namna ulivyo na uwezo wako wa kujenga na kuhimili hoja za watu wengine
 
Mpaka Leo hakuna aliyechukua form ya Uraisi Chadema ikiwa ni Siku ya mwisho
 
Lowasa anataka Urais kupambana na Umasikini kama umeshamsikia hiyo ndo ajenda yake kubwa, kwakuwa CCM wanapenda umasikini na ujinga ili waendelee kutawala, hiyo imemfanya Lowasa atafute watu wengine wenye malengo ya kuundoa umasikini na ujinga wa watanzania na si wengine ni UKAWA, siku Lowasa anajiunga UKAWA itakuwa ndo mwanzo wa Zama nyingine katika taifa letu, bila CCM kuwa Chama Tawala. Lowasa akiwa Rais atapigana kufa na kupota ku prove kuwa yaliynenwa juu yake si kweli, na watanzania tutanufaika sana na utawala wake.

Lowasa yupi unyemzungumzia hapa? Je ni yule yule Lowasa ambaye yeye mwenyewe amesema ametumia maisha yake yote CCM, yule yule aliyesema yeye hatoki CCM na asiyempenda ahame chama? Lowasa gani mnayemzungumzia hapa? Ni yule yule mliyemtuhumu humu humu jamvini kamlisha sumu Mwakyembe, ni yule yule mliyeleta data zake humu jamvini na kumuita Richard of Monduli? Au kuna Lowasa mwingine ambaye yeye anakerwa sana na umasikini wa watanzania kiasi anataka kujitolea maisha yake kuwaokoa watanzania? Yuleyule au kuna mwingine ndugu zangu?
 
Kwa utumbo ulioharisha hapa na uhakika hujui maana ya demokrasia, tanzania hakuna udikiteta na demokrasia vilevile hakuna. Ila kwa akili zako nimekuona wewe unapoana hakuna udikiteta unaita ni demokrasia aibu ilioje hii? Nenda kajifue upya uje utueleze demokrasia ni nini?

Haya nitajie huko kwenye Demokrasia unakokuongelea halafu pia tukueweke kwenye lens kama tulivyoweka demokrasia ya TanZania kwenye lens pia!
 
Haya Libya, Misri, Iraq, Yemen walikuwa na mawazo kama yako lakini sasa wamejifunza wanajuta. Kwa hiyo unataka kutuambia nasisi watanzania tujaribu mawazo hayo ili tuje pata tabu ya maisha kwetu na familia zetu? ?

Nchi zote ulizozitaja walitumia bunduki,sisi tutatumia sanduku la kura.Kenya,Nigeria,Malawi n.k walivipiga chini vyama tawala mbona hawakujuta?Acha ujinga.
 
Wacha kudanganya watu na kuwatia woga. Siku hizi hakuna ubabe wa hovyo kiasi hicho na ndio maana wengi waliofanya hivyo wametoka madarakani na kustaafia The Hague kumalizia uzee wao.
Fikra za kizamani achana nazo


Nitajie huyo aliyetoka mfumo wa kama CCM halafu akaenda The Hague! Hivi hata unajua The Hague ni nini na kwanini hata ilianzishwa? Unafikiri kila nchi inapelekwa the Hague basi ingekuwa hivyo kungejaa huko Tha Hague!
Mbona Kagame anapiga risasi live wapinzani kila siku na hayuko The Hague? Na anakula bata na wazungu kila siku tena ni hivi majuzi wazungu wamemteua kuwa Kiongozi mwenye Utawala Bora Duniani
 
Usiishushe CCM kwa kiasi hicho! CCM ni Chama Dola usisahau hilo, kama Bw.Lowasa akihamia CHADEMA ujue sasa Bw.Lowasa siyo tu adui wa CCM bali ni adui wa Serikali ya JMT na mfumo wake wote kuanzia TRA, Polisi, Magereza, JWTZ n.k chini ya Raisi wa JMT ambaye ndiye Kiongozi wa CCM, usisahau pia uhusiano mzuri wa TanZania na nchi kubwa Duniani kama Uchina, Marekani, Ulaya n.k hawa wote mpaka sasa hivi wanaipenda na kuikubali TanZania kama ilivyo kumbuka Upinzani wamejaribu sana kuisemea Serikali ya TanZania kwa wazungu lkn walipuuziwa kwa maana TanZania ni kipenzi cha Wazungu pmj na Wachina!



Wazungu wanasema chama chochote kilicho tawala zaidi ya mia 40 barani afrika hakiwezi kuwaletea maendeleo wananchi husika.Isipokuwa ni kuwanyonya wanachi kama walivyofanya wakoloni.Chama hicho inatakiwa kiondoke madarakani.



Ni wapi na lini Wazungu wamesema hivyo leta Ushahidi hapa, kwa maana hao pekee ndiyo wanaoweza kuamua kama CCM iondoke au isondoke na siyo Lowasa, Slaa au sijui Mbowe!
 
Ila nilichojifunza hapa faida ni nyingi kuliko hasara


Lowassa anafaida nyingi ndani ya ukawa kuliko hasara lazima tuwe risk takers ili taifa hili liweze badilika
 
Usiishushe CCM kwa kiasi hicho! CCM ni Chama Dola usisahau hilo, kama Bw.Lowasa akihamia CHADEMA ujue sasa Bw.Lowasa siyo tu adui wa CCM bali ni adui wa Serikali ya JMT na mfumo wake wote kuanzia TRA, Polisi, Magereza, JWTZ n.k chini ya Raisi wa JMT ambaye ndiye Kiongozi wa CCM, usisahau pia uhusiano mzuri wa TanZania na nchi kubwa Duniani kama Uchina, Marekani, Ulaya n.k hawa wote mpaka sasa hivi wanaipenda na kuikubali TanZania kama ilivyo kumbuka Upinzani wamejaribu sana kuisemea Serikali ya TanZania kwa wazungu lkn walipuuziwa kwa maana TanZania ni kipenzi cha Wazungu pmj na Wachina!

Nafasi pekee ya Bw.Lowasa na CHADEMA wake ni labda waasi waingie porini kwa kutumia fedha zao walipe wagaidi na kuanza kufanya nchi isitawalike lkn wakifanya hivyo kama wana huo uwezo kumbuka WatanZania watawageuka na kuwaona wanaleta machafuko pmj na UN na wengineo!

Kumbuka mpaka sasa hivi ukisikia CCM na Serikali wako kimya usifikiri wamelala wanaangalia kila kitu na wanajipanga kumbuka wana uwezo tu wa kufungia chombo chochote kile cha habari pmj na JF na hakuna kitu tutafanya! Hivyo kwa kifupi kama Bw.Lowasa kweli anataka kwenda Upinzani basi naweza kusema kama wazungu wasemavyo yuko out of touch with reality!

Mkuu Barbarosa unajua asili ya jina lako? Tuache hilo kwa sasa, ni kweli Edward akiondoka CCM atakuwa adui wa dola isipokuwa jua kitu kimoja dola yenyewe haipo pamoja katika hili, ni dola iliyogawanyika na mgawanyiko upo kwa ndani, ni ngumu kujua nani wa kumuamini.

Kuhusu foreigh powers (Uchina, Marekani na Ulaya) hawa wana maslahi yao na bado hayatishiwi kwa Lowasa na UKAWA kuingia madaraki. These powers would only act against the move kama maslahi yao yatatishiwa. Hawaipendi CCM kwa sababu ni CCM wanaipenda kwa sababu inalinda maslahi yao. Hata hivyo mahusioano yao si mazuri kama uanavyotaka kutuaminisha kwa mfano walisimamisha misaada kwa budget hivi karibuni CCM kamasi zikawatoka.

Hili la dola kukaa kimya ndio itakuwa inapiga hesabu zake, je zitakuwa na tija - time will tell ila siasa lazima hesabu kama dola inavyopiga hesabu ana the other side inapiga hesabu vivyo hivyo. Siasa ni kama mchezo wa chess kuna moves na counter moves mkuu.
 
Lowassa hata akienda chama gani hatashinda urais, Halafu mnapozungumzia ukawa ya lowassa je mmejumuisha vyama vingine kama CUF na wengine? Naona hapa kuna makubaliano ya chadema na lowassa sio lowassa na ukawa, kwa hiyo kuna uwezekano wa lowassa kwenda chadema na akagombea kwa chadema sio ukawa, kwa sababu vyama vingine havijaonyesha kukubaliana na mpango huo,
Hapo ndio ccm watatumia ile ile ya kugawa kura wao wapite kama mwewe,

Umeandika kwa kujiamini sana Mr Hero, siasa is very dynamic, haijanyooka kihivyo
 
Kama nia nikushika dola kwa kutumia watu wahalifu,! Mi sidhani kama watanzania wanaweza kukubaliana na wazo Hilo. Namimi sidhani kama tumefika huko
 
Mwandishi wa story hii amesahau kuwa, one of the best move ambayo itafikiwa na serikali ya ukawa ni kuunda chama kipya cha siasa kwa umoja wao. Kitu ambacho kingekuwa ni kigumu ktk utawala huu wa CCM
 
Itakuwa hakuna kilichofanyika km maslahi yk binafsi atakuwa hana nia ya watanzania bali yy binafsi
 
Back
Top Bottom