Hatari: Majambazi yavamia na kupora raia!

Hatari: Majambazi yavamia na kupora raia!

nyumba yangu ni jirani kabisa na ya hiyo nyumba iliyovamiwa lakini ilitolewa oda ya watu kutotoka nje na risasi zilikuwa zinarushwa kama njugu...ilikuwa na hatari sana! Namshukuru mungu hawakuifikia nyumba yangu. Kwa jinsi nilivyokuwa muoga mbona ningejinyea!!!!!!!
kwahyo kumbe hukuwaona ila ni simuliz za majiran? Siku nyingne wakija waambie waje kabisa kwako ili usimulie kwa ushuhuda kabisa(natania mkuu)

all in all hongera kwa kusalimika na kuish na majiran wanaojiweza maana wangekosa wanayoyahitaji wangekuja kwako
 
inaonekana kama unashabikia hilo tukio

kivipi mkuu? majambazi huwa wanashabikiwa? labda hujawahi kukabiliana na mafedhuli hao ndio maana unasema hivi.
 
Ni hatari sana, poleni kwa kweli...

asante sana mkuu. usiombe kukabiliana haya majitu yanayoitwa MAJAMBAWAZI...hayana utu kabisa. nadhani badala ya polisi kuhangaika na GWAJIMA wangeshughulikia hili tatizo la ujambawazi kwanza. kila siku tunasikia wapambanaji wa ufisadi wakiuawa lakini hatujawahi kusikia polisi wameua jambazi zaidi ya wao polisi kuuliwa na kunyanganywa silaha. hv sisi raia tusiokuwa na ulinzi tukimbilie wapi?
 
hata kupiga simu polisi mlishindwa ?
Wote tunatambua kuwa Jeshi la Polisi halina nyumba za kutosha licha ya magofu/ magodown yaliopo hivyo hivyo kwa JW.
Kitaa humu tunaishi nao wengi tu. Ila wakati wa tukio hawatoki nje! Sijui uoga au nyenzo au mafunzo haba!

Mm naomba Majambazi yaanze kuvamia Nyumba za ma askari Polisi na wanajeshi.

Wengine siku hizi wanaenda na vibegi kazini, akimaliza zamu anavua nguo za kazi anatupia ndani ya kibegi! Sijuiantiki yake nini?

Nadhani ukipiga simu usiku wanajua tu "tiyari kimenuka" hivyo hawaipokei au wanasubiri baada ya nusu saa ndio wanakutafuta wao.
 
kwanin mkuu
si watakajua nyumba yake ilikuwa ya ngapi,huo ni uchokozi wa dhahiri...Pia yawezekana ni katoto hakana hata nyumba....., yawezekana ameambiwa na mtu......, yawezekana amesikia katika TV/Radio kuhusu haya majambazi.....yawezekana amesikia katika daladala na yeye ameongeza chumvi yaani JF full raha kutmia fake names, ni hayo tu mkuu. All in all tumwombe Mungu atuepushe na MAJAMBAZI maana ukiwa katika 18 zao wana makeke ya hatari.
 
huna ustaarabu wala staha kwa wenzako.. sawa walipigwa na kuumizwa mbaya zaidi waliibiwa...JE ULIKUWA NA HAJA YA KUCHAGIZA KISHABIKI "KIPIGO CHA MBWA MWIZI" MARA "KIPIGO CHA MBWEHA".. usitukane mamba .... kuna leo na kesho... IT SEEMS LIKE UMEFURAHIA MATATIZO YA WENZAKO....
 
Nilifikiri peke yangu sikumwelewa, hizi lugha hizi zichanganywe na jani la A town ni shida
 
Awapigie simu polisi wapi? ninao wafahmu mimi? au kuna polisi wengine

jeshi letu ni sikivu wape taarifa uone. wananchi tunatakiwa tujitambue yakua, ulinzi ni sisi wenyewe kwa kusaidiana na polisi.
 
ni majambazi mkuu. vibaka hawana silaha za kivita.

Cha kwanza ulijuaje ni siraha ya kivita
Cha pili,yani watu watumie siraha ya kivita kwenda kuiba TV na sub woofer ambazo saaa hivi zinauzwa mpaka elfu hamsini!?
 
nyumba yangu ni jirani kabisa na ya hiyo nyumba iliyovamiwa lakini ilitolewa oda ya watu kutotoka nje na risasi zilikuwa zinarushwa kama njugu...ilikuwa na hatari sana! namshukuru Mungu hawakuifikia nyumba yangu. kwa jinsi nilivyokuwa muoga mbona ningejinyea!!!!!!!

inaonekana wangeingia kwako hata mzigo wangekula...kunguru.
 
Taharifa ya watu kupigwa inaandikwa hivyo,kipigo cha mbwa mwizi,kipigo cha mbwea? Hao ni vibaka waliokua na siraha.majambazi hawaibi tv moja wala nguo za kuvaa.
 
Taharifa ya watu kupigwa inaandikwa hivyo,kipigo cha mbwa mwizi,kipigo cha mbwea? Hao ni vibaka waliokua na siraha.majambazi hawaibi tv moja wala nguo za kuvaa.

watakuwa majambazi njaa...vibaka hawamiliki bunduki na huja kwa kunyata. hawa waliforce kwa nguvu, wakavunja milango na kuingia ndani kwa lazima na kuwazuia majirani kutoka nje kwenda kusaidia.
 
inaonekana wangeingia kwako hata mzigo wangekula...kunguru.

mimi nimetoa tahadhari ili wana dar es salaam muwe makini na matukio haya ya kijambazi. sasa povu la nini badala ya kunipongeza kwa kutoa tahadhari kwa wananchi? hujui kesho mijitu hii itavamia nyumba ya nani. hili ni tukio la pili kutokea katika maeneo haya? wewe huoni kwamba hili ni tatizo linalopaswa kukemewa na kila mzalendo? wewe mnyarwanda au mrundi? na mbona una roho ya kikauzu hivi?
 
mmh. ulivyo andika. either umefurahia.. au mmoja wao

hiyo ni negative perception yako. nimetumia staili hii ya uandishi ili kuweka msisitizo. nifurahie masaibu ya majirani zangu ili iweje? always try to think positively!
 
mimi nimetoa tahadhari ili wana dar es salaam muwe makini na matukio haya ya kijambazi. sasa povu la nini badala ya kunipongeza kwa kutoa tahadhari kwa wananchi? hujui kesho mijitu hii itavamia nyumba ya nani. hili ni tukio la pili kutokea katika maeneo haya? wewe huoni kwamba hili ni tatizo linalopaswa kukemewa na kila mzalendo? wewe mnyarwanda au mrundi? na mbona una roho ya kikauzu hivi?

mm sio mnyarwanda mie somali original.
 
Back
Top Bottom