Hatari: Majambazi yavamia na kupora raia!

Hatari: Majambazi yavamia na kupora raia!

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,765
Reaction score
29,209
Jana usiku mitaa ya Chamazi Kwa Mkongo ilizizima kwa mirindimo ya risasi baada ya majambazi kuvamia nyumba mbili za raia na kuwakomba kila kitu.

Ilikuwa ni kama sinema vile: Majambawazi hao wa miraba 4 waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito za kivita huku wakiwa wamefika nyuso zao kininja walianza kwa kuvamia nyumba ya kwanza na kuwaamuru raia watoe pesa.

Katika nyumba ya kwanza mume alijificha uvunguni lakini kipigo kilipomkolea mkewe ikabidi atoke uvunguni kumsaidia ila hawakufua dafu mbele ya majambazi hao waliokuwa wamebeba silaha za kivita.

Wote wawili walipigwa kipigo cha mbwa mwizi na kuamuliwa kutoa pesa zote walizokuwa nazo. Kisha walipora nguo, TV, subwoofer na vifaa vyote vya thamani na kuhamia nyumba ya pili.

Walipoingia nyumba ya pili mwenye nyumba alijificha darini ili kujiokoa.

Majambazi walimshtukia na kumshusha kisha wakampa kipigo cha mbweha hadi akazimia na kumpora mali zake zote kisha wakatomea kizani.

Ndugu zangu muwe makini. Dar sio salama tena. Je, tutatoka na roho zetu?

:israel:
 
We nyumba yako ilikua ya ngapi?

nyumba yangu ni jirani kabisa na ya hiyo nyumba iliyovamiwa lakini ilitolewa oda ya watu kutotoka nje na risasi zilikuwa zinarushwa kama njugu...ilikuwa na hatari sana! namshukuru Mungu hawakuifikia nyumba yangu. kwa jinsi nilivyokuwa muoga mbona ningejinyea!!!!!!!
 
Na kweli hata avatar inaonyesha unalia sana
 
nyumba yangu ni jirani kabisa na ya hiyo nyumba iliyovamiwa lakini ilitolewa oda ya watu kutotoka nje na risasi zilikuwa zinarushwa kama njugu...ilikuwa na hatari sana! namshukuru Mungu hawakuifikia nyumba yangu. kwa jinsi nilivyokuwa muoga kidogo. Cha mbe webs mara mbwa mwizi ni lugha isiyo na sitaha kwa watu wa thamani tena ukizingatia kuwa ni majirani wako! Au unaona ujiko kutumia lugha hii?
 
nyumba yangu ni jirani kabisa na ya hiyo nyumba iliyovamiwa lakini ilitolewa oda ya watu kutotoka nje na risasi zilikuwa zinarushwa kama njugu...ilikuwa na hatari sana! namshukuru Mungu hawakuifikia nyumba yangu. kwa jinsi nilivyokuwa muoga mbona ningejinyea!!!!!!!
ha ha haha
 
sio vibaka mkuu, ni majambawazi. wale wanaochomwa moto ni vibaka.
Nimekulia uswazi na tushawachoma moto majambazi na SMG zao. Wengi tu, tena siku hizi hakuna majambazi kama 90s, sema tu mitandao inaripoti kila kitu hata jirani akigeuza chupi nje ndani ataandikwa.
 
nyumba yangu ni jirani kabisa na ya hiyo nyumba iliyovamiwa lakini ilitolewa oda ya watu kutotoka nje na risasi zilikuwa zinarushwa kama njugu...ilikuwa na hatari sana! namshukuru Mungu hawakuifikia nyumba yangu. kwa jinsi nilivyokuwa muoga kidogo. Cha mbe webs mara mbwa mwizi ni lugha isiyo na sitaha kwa watu wa thamani tena ukizingatia kuwa ni majirani wako! Au unaona ujiko kutumia lugha hii?

mkuu samahani nimetumia huu usemi ili kuonyesha kiwango cha ufedhuli na ukatili wa majambawazi haya.
 
Back
Top Bottom