Hatari: CCM yaunda KIKUNDI cha kuvuruga UKAWA

Hatari: CCM yaunda KIKUNDI cha kuvuruga UKAWA

kupata katiba ya ukwel Tanzania ni ndoto mana watu wanaleta Interest no never hatuwezfikia lengo.
Jah bless Tanzania
 
Ni wazi kuwa zoezi Zima la kuandika katiba mpya haikuwa ajenda wala sera ya watawala na ccm yao. Hili jambo liliporwa ama kudandiwa na mwenyekiti wa ccm kwa lengo moja la kujipatia umaarufu. Kinachofanywa sasa ni kuvuruga ama kuharibu zoezi hilo baada ya kushindwa kupenyeza mambo ama vipengele vinavyolinda udhalimu, wizi, uhalifu na masilahi yao binafsi.

Ni majuzi tu kiranja mkuu wa ccm ametamka wazi kuwa hili zoezi linaweza kusukumwa mbele hadi mwakani ili kupisha utekelezaji wa mambo mengine. Katika kuonesha dhamira ovu waliyo nayo, jana Kikwete amediriki kutamka wazi kuwa kama mchakato huu utashindikana basi watarejea kwenye katiba ya mwaka 1977 ambayo ilishavunjwa na kunajisiwa na Wazanzibar wenyewe wakishirikiana na watawala walioshindwa kusimamia na kulinda viapo vyao.

Haya yote yanafanywa sio kwa bahati mbaya ila ni makusudi na imepangwa iwe hivyo hasa kwa kurejea hotuba ya Kikwete iliyovishwa kilemba cha uzinduzi lakini kwayo ikiwa na maudhui ya kumshambulia Mhe. Jaji Warioba na watu wengine. Katika hilo tunaona hata wajumbe wengine ndani ya bunge hilo wakijikita kwenye mipasho, kutukana na kushambulia wengine badala ya kujenga hoja za msingi.

Hakika dhambi inayotendwa na watawala pamoja na udhalimu uliojaa hila na ubinafsi kwa watanzania itawatafuna siku zote za maisha yao

Mkuu taffu69 historia ni mwalimu mzuri sana...walikuwepo wenye fikra kama za watawala wa sasa, wakidhani wataishi milele na kwamba bila wao hakuna taifa...wameondoka madarakani na hukumu ya waliyotenda hakika yaambatana nao...waache waendelee kulewa madaraka, lakini kipimo wapimacho ndicho watakachopimiwa tena kikijazwa na kusukwasukwa...heri ni kwao waliopewa macho na wakayatumia kuona...ole ni kwao waliopewa macho wakaamua kuvaa upofu...siku yaja ambapo kila mmoja atalipwa kwa kadri ya matendo yake.
 
Last edited by a moderator:
Yericko Nyerere

[video=youtube_share;ko4A4YKsXDk]http://youtu.be/ko4A4YKsXDk[/video]

SHONZA JK.jpg

Angalia Mama Salma anavyochungulia baada ya Shonza kujilaza kwa Mume wake.
 
Hivi wewe mzee mzima ni lazima uchangie kama umekosa hoja?
Mpuuzi ni mpuuzi tu.

Tanganyika yangu kwanza, Muungano bila Tanganyika siyo Muungano

Hapo upo pamoja na mimi, nilisema siku nyingi sana Nyerere alifanya makosa makubwa sana na mojawapo ni hili la kuiuwa Tanganyika.

Nna furaha sana kuona watetezi wa fikra za dikteta leo mkiungana nami kuzipinga fikra zake.

Amma kweli mnafik hajifichi.
 
Dada inasikitisha sana kuona kuna kundi la vijana nchini tumelipa dhamana yakutunga katiba lakini wao wanajijenga kisiasa.

Unapenda kujikwaza, hivi wewe unauwezo wa kumpa nani dhamana? hebu nenda chalinze kampe dhamana umpendae ya kutunga katiba tuone?

Kalenga vipi? dhamana imeingia mitini?
 
kuna kundi litaanzishwa kesho linaitwa KATIKATI, hili kundi ni hatari maana msimamo wake ni wa katikati, mfano watapiga kura mara mbili, kura ya siri na kura ya wazi, kusimamia maslahi yao ya KATIKATI, kund hili ni hatari
 
Wananchi na umma kwaujumla tuliowekeza matumaini yetu kwa UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI tusimame imara kuzuia hatari iliyombele yetu,

Wiki moja sasa tangu kuibuka kwa nguvu ya wajumbe wakatiba mpya wanaounda umoja uitwao UKAWA,ccm kupitia idara za kijasusi za nchi wamekuwa kwenye mipango mkakati ya kukabiliana na umoja huo hasa baada ya kudorola kile kilichoitwa na JK kundi la Tanzania kwanza yani kundivla wanaotaka Serikali mbili.

Juzi wameridhia kuanzisha kikundi kinachojiita DARAJA, na kinaundwa na wajumbe wengi vijana wenye mawazo na itikadi za ccm,

Dhamira kuu ikiwa ni kuvunja nguvu za UKAWA, yaani kuvunja nguvu za Waamini wa SERIKALI TATU.

Kikundi hicho kitaundwa na baadhi ya wajumbe wafuatao:

1. Hamis Kigwangalla (Kiongozi)
2. Ester Bulaya
3. Zitto Kabwe
4. David Kafulila
5. Maria Sarungi
6. Hamad Rashid
7. Halima Mdee (leo wanamfukuza)


Na wengine wengi.....

Nimejaribu kuzungumza na wanaounda kikundi hiki kama wanamalengo na mitazamo tofauti na UKAWA, wakasema hapana, yani wanaafiki mitazamo na malengo ya UKAWA, nikawauliza tena, kwanini wasiunganishe nguvu hapo UKAWA? hawakuwa na jibu.

Leo wataendele na hatua za mwisho za uundaji wa kundi hilo kharamu.


Tanganyika HURU na Zanzibar HURU kwanza mengine yatafuata, = Serikali TATU
Mpaka Kafulia na Mdee?!! Hi sasa ni hatari!

Alafu mkuu leo Bunge lipo na kama lipo ni kuanzia saa ngapi?
 
Kama UKAWA ni jeshi kubwa na lenye nguvu, vipi liogope kikundi kidogo cha Daraja na kuona kuwa Tanzania kwanza ambayo ndio jeshi kubwa ktk mchakato huu hawalihofii? Hapa jibu ni kuwa kuna hatari kuwa UKAWA ikagawanyika na kua kundi lisilo na ushawishi tena kwani litabakiwa na waumini wachache sana, pili Chadema inamuogopa sana Zitto na kuamini kua kila movement yake italeta matokeo hasi ktk kundi wanaloliamini pia ijulikane kua UKAWA inaundwa na vyama vya CUF, NCCR na CHADEMA bila kua na members kutoka CCM.
Inaelekea una mahaba na Zitto.
Kiufupi Zitto hana ajira.Yaani anachokipigania ni Kuendelea kusaidiwa na Mahakama ili asirudi mtaani.
 
Jana nilisikia tangazo lao la kukutana niliogopa kumsikia mdee nampongeza kwa kujitowa
 
Malengo yao hicho kikundi ni nini haswa!? Kama ni kuirudisha Tanganyika mi nitawaunga mkono!
MUNGU IBARIKI TANGANYIKA
 
Hapo upo pamoja na mimi, nilisema siku nyingi sana Nyerere alifanya makosa makubwa sana na mojawapo ni hili la kuiuwa Tanganyika.

Nna furaha sana kuona watetezi wa fikra za dikteta leo mkiungana nami kuzipinga fikra zake.

Amma kweli mnafik hajifichi.

Acha unafiki, Tanganyika tulianza kuidai zamani mno, nakiri kumpongeza Nyerere kwa kufuta ukabila Tanganyika, lakini namlaumu kuiua Tanganyika hivi hivi, na kuleta matabaka kwenye elimu
 
Kama UKAWA ni jeshi kubwa na lenye nguvu, vipi liogope kikundi kidogo cha Daraja na kuona kuwa Tanzania kwanza ambayo ndio jeshi kubwa ktk mchakato huu hawalihofii? Hapa jibu ni kuwa kuna hatari kuwa UKAWA ikagawanyika na kua kundi lisilo na ushawishi tena kwani litabakiwa na waumini wachache sana, pili Chadema inamuogopa sana Zitto na kuamini kua kila movement yake italeta matokeo hasi ktk kundi wanaloliamini pia ijulikane kua UKAWA inaundwa na vyama vya CUF, NCCR na CHADEMA bila kua na members kutoka CCM.

Tanzania kwanza kivipi wakati zanzibar tayari ni nchi na wana katiba yao? Mkishatengua hicho kitendawili hata mimi nitasema TZ kwanza la sivyo tunaitaka Tanganyika au Tanzania bara yetu!
 
Kama anashinda kwenye vikao vya siri si yeye,achaneni nae,au la mkamjadili kwenye vikao vyenu, mnavyo muongelea hapa jamvini kila mtu anajua kuwa bado mna muogopa.
 
Na wewe tafuta sehemu ya kula hizo hela ili maisha yaende, kila mbuzi atakula kulingana na urefu wa kamba yake.Nchi isha uzwa hii ukipata nafasi ya kula, kula bila kujali pesa zimetoka wapi, watu saivi wapo bunguni wanakula tu hatuoni chochote cha maana wanachokifanya.
 
Kama anashinda kwenye vikao vya siri si yeye,achaneni nae,au la mkamjadili kwenye vikao vyenu, mnavyo muongelea hapa jamvini kila mtu anajua kuwa bado mna muogopa.

We kati ya majina yote umeliona jina la zitto. Anakugonga ama?
 
Back
Top Bottom