Hata nimfumanie kitandani kwangu sitamuacha kamwe..........

Hata nimfumanie kitandani kwangu sitamuacha kamwe..........

Hata ukimfumania..... teh teh yakweli haya ?

Hii Isidingo, Kuna jamaa anataka kulea mimba ya Nikiwe Sibeko aliyopewa na Frank Xavier.....
Honestly inataka moyo sana.

Mkuu anasema hata akimfumania atamsamehe nadhani anamaanisha na anataka kuonyesha ni kwa jinsi gani anampenda na kumthamini mkewe. Iapo siwezi kabisa kutabiri kitu gani kitatokea akimfumania mkewe.
 
Ni safari ndefu yenye milima na mabonde...........safari iliyokua ya kiu kali na machungu mengi.Tabasamu lako la kila siku asubuhi ndio chachu na nguvu ya maisha yetu. Hata ndugu zetu wa damu walipotusaliti ulisimama pembeni yangu kunipa matumaini...........nakumbuka nilipokukimbia ulinitafuta na kujumuika na mimi mafichoni,uliniambia unanipenda na huwezi kuniacha hata kama naishi shimoni,....................ulipobeba ujauzito wa Junior nilikuambia tutoe.........ulilia sana, nilienda kununua majani ya chai mengi nikabandika jikoni ili unywe........nakumbuka kwa tabasamu lilojaa machozi uliniambia ule ndio ulikua mwanzo na mwanga wa maisha yetu..................siwezi kuandika yote maana machozi yatanitoka.............Mke wangu wewe ni kila kitu kwangu na naomba kifo ndio kitutenganishe. Narudia tena Hata nikufumanie sasa ivi sitakuacha kamwe. Hii pia ni kwa ajili ya wanawake wote mnaoumizwa kwa matusi,dharau na kejeli hapa JF..........Nawapenda wote.

credits brother that is the way a man should be talking ,true love never die it only get strong as time passes by!
 
Yani ukute mwanaume mwenzio anahema juu ya kifua cha mkeo halafu umsamehe...!

Huyo mwanamke nae akiendelea kuishi na wewe atakua hayupo timamu
 
Ni safari ndefu yenye milima na mabonde...........safari iliyokua ya kiu kali na machungu mengi.Tabasamu lako la kila siku asubuhi ndio chachu na nguvu ya maisha yetu. Hata ndugu zetu wa damu walipotusaliti ulisimama pembeni yangu kunipa matumaini...........nakumbuka nilipokukimbia ulinitafuta na kujumuika na mimi mafichoni,uliniambia unanipenda na huwezi kuniacha hata kama naishi shimoni,....................ulipobeba ujauzito wa Junior nilikuambia tutoe.........ulilia sana, nilienda kununua majani ya chai mengi nikabandika jikoni ili unywe........nakumbuka kwa tabasamu lilojaa machozi uliniambia ule ndio ulikua mwanzo na mwanga wa maisha yetu..................siwezi kuandika yote maana machozi yatanitoka.............Mke wangu wewe ni kila kitu kwangu na naomba kifo ndio kitutenganishe. Narudia tena Hata nikufumanie sasa ivi sitakuacha kamwe. Hii pia ni kwa ajili ya wanawake wote mnaoumizwa kwa matusi,dharau na kejeli hapa JF..........Nawapenda wote.

kwa mtazamo wangu nafikiri umeandika kufurahisha jukwaa tu, au kuna kitu ambacho sisi wanaume tunacho wew huna, au unamatatizo ya akili. Jiwa tu akiliona dume lingine linanyemelea jike lake zinapigwa, ije kuwa mwanadamu kufumania na kusamehe?
 
Ni kweli mkuu.......tuna miaka mingi sana kwenye ndoa.....tumebarikiwa watoto pia......ni zaidi ya mke....na zaidi ya rafiki pia.
................hongera sana ndugu laiti wangekuwepo wanaume wachache kama wewe ndoa ingekuwa kweli maisha mazuri na ya furaha...........uvumilivu na kusamehe ndiyo nguzo muhimu katika ndoa.....vinginevyo ni vuruguuuu tupu...................
 
Ni safari ndefu yenye milima na mabonde...........safari iliyokua ya kiu kali na machungu mengi.Tabasamu lako la kila siku asubuhi ndio chachu na nguvu ya maisha yetu. Hata ndugu zetu wa damu walipotusaliti ulisimama pembeni yangu kunipa matumaini...........nakumbuka nilipokukimbia ulinitafuta na kujumuika na mimi mafichoni,uliniambia unanipenda na huwezi kuniacha hata kama naishi shimoni,....................ulipobeba ujauzito wa Junior nilikuambia tutoe.........ulilia sana, nilienda kununua majani ya chai mengi nikabandika jikoni ili unywe........nakumbuka kwa tabasamu lilojaa machozi uliniambia ule ndio ulikua mwanzo na mwanga wa maisha yetu..................siwezi kuandika yote maana machozi yatanitoka.............Mke wangu wewe ni kila kitu kwangu na naomba kifo ndio kitutenganishe. Narudia tena Hata nikufumanie sasa ivi sitakuacha kamwe. Hii pia ni kwa ajili ya wanawake wote mnaoumizwa kwa matusi,dharau na kejeli hapa JF..........Nawapenda wote.

This is TRUE LOVE
image.jpg​
 
Najua unachomaanisha....sijawai lakini tumeshapitia mengi magumu zaidi ya kufumania. She is my hero, that's all I can say.
Basi bado hujajua utamu wa kufumania. Subiri ufumanie kwanza ndio urudi humu kutupa habari!
 
mbona watu mnaongea kama vile hakuna aliyewah kufumania na akasamehe?? Tena afadhali ya huyu ambae mema ya mkewe yanampa nguvu ya kuishnda hyo hasira.
 
Ni kweli mkuu.......tuna miaka mingi sana kwenye ndoa.....tumebarikiwa watoto pia......ni zaidi ya mke....na zaidi ya rafiki pia.
Ni safari ndefu yenye milima na mabonde ........ulipobeba ujauzito wa Junior nilikuambia tutoe.........ulilia sana, nilienda kununua majani ya chai mengi nikabandika jikoni ili unywe........
Mkuu Sari', sisi tuliopitia majaribu ya aina hii, tunakuelewa, in fact naelewa hata sababu za zilizokufanya unkanunue majani ya chai!, naimagine jinsi unavyompenda Junior kwa pendo la dhati la baba!.

Mimi nimepitia almost the same, baada ya kuoa nikiwa kijana jana, mimi na wife tukahamia UK kutafuta maisha, utumwa wa box ukanishinda, nikalazimisha kurudi bongo, baadae tuenda US, by that time tuna watoto 2, kule mwenzagu ndio alipata scholaship ya miaka 4, mimi ndie niwe haise boy na baby sitter wa watoto wetu wawili!. Kwa vile mimi bongo nilikuwa na kazi, tukakubaliana mimi nirudi na watoto, niendelee na kazi, yeye asome, akimaliza atarejea bongo!. Japo nilimtembelea kila miaka 2, nilimpomtembelea mara ya pili ambapo ndio anamaliza shule, yalinikuta yaliyokukuta!, sikuijua technick ya "majani ya chai!", nilikubali yote, nikasemehe na kukubali kuendelea!, ila mwenzagu aligoma kurudi!, nilirudi mwenyewe bongo na kusubiri for 7 good years!.

Katika kusubiri huko, ubinadamu nae lazima uendelee, hivyo nililazimika kuwa na "rafiki" tena nakumbuka kuna wakati wakuu wangu wa jumuiya ndogo ndogo, walilalalimika, "wewe una ndoa ya kikatoliki", kwa nini "rafiki" umlete home?!, nilijibu "huyu ni rafiki zaidi ya rafiki"!, kwanza ile kukubali tuu, kuwalea wale watoto wangu wawili wa mwanzo, na kukatokea wawili wengine hapa katikati!, nikajiamini wanawake wenye upendo wa hivyo, ni wale tuu walioshushiwa kutoka mbinguni!.

Katika kuendeleza "ubinaadamu", shetani naye akaleta majaribu mengine!, nilipata very bad accident, nikawa hospitalized, muhimbili, South Africa na India for six months, wife aligoma kuja, nikwa take care na huyu "rafiki" kutokana na lots and lots of anaethessia nilipata "pseudo invalidity" but She stood by me all this time. Hospitali za wenzetu, mgonjwa unalazwa na anaekuangalia, kila chumba private word ina kitanda na jirani kuna kiti-kitanda, mchana kiti, usiku kitanda!. Huyu "rafiki" alilala kwenye kiti-kitanda for all this time, mpaka niliporuhusiwa!.

Baada ya kurejea home, ndipo wife akataka kurudi!, nadhani baada ya kushauriwa na ndugu zake, na nimerudi kwenye wheel chair, hivyo wakadhani nitakuwa confirmed to wheel chair!. Nilisema no!, japo nilimpenda kupitiliza, kumruhusu wife kurudi, kutakuwa sio kumtendea haki huyu "rafiki" aliyeteseka na mimi all this time!. Nilikubali yale ya mwanzo yaishe, nikafuata taratibu, nikamuoa rasmi "rafiki" na nikamuahidi, hivyo hivyo, kwa sucrifice aliyojitolea juu yangu, hata nikimkuta in my bed with someone else, nitamwambia huyo "mwenzangu" avae nguo zake na kujiondokea!, na wife, nitamwambia, hana haja ya kutoa maelezo yoyote, nitasemehe na kamwe sitomwacha!, nitaamini ni shetani tuu ndio anaweza kumpitia!, kwa vile pendo letu ni more than everthing, tutatenganishwa na kifo tuu!, nothing else!.
This is a true story.
Pasco.
 
Swala la kufumania si dogo jamani especially kwa umpendae. It hurts but if u truly love the wuman, the sentence ''I forgive you n don't dare to cheat on me again'' must proceed from your mouth na mapenzi yakaendelea.
 
leo nimejua kwa nini serikali inakataza watu wasivute bangi.,hizi bangi tu hamna kingine....
 
Hii Isidingo, Kuna jamaa anataka kulea mimba ya Nikiwe Sibeko aliyopewa na Frank Xavier.....
Honestly inataka moyo sana.

Mkuu anasema hata akimfumania atamsamehe nadhani anamaanisha na anataka kuonyesha ni kwa jinsi gani anampenda na kumthamini mkewe. Iapo siwezi kabisa kutabiri kitu gani kitatokea akimfumania mkewe.



Huyo frank kazidi sasa

Mwanzo si alimtia mimba Yule mhindi, alafu Rajesh akamuoa na kumlelea mtoto kama ni wake ,
Anaona dezo ee, ndo maana nimeacha kuangalia isidingo
 
Back
Top Bottom