Je, dini inaweza kuimarisha ujinga na umaskini?

Je, dini inaweza kuimarisha ujinga na umaskini?

MIHAYO1710

Member
Joined
Apr 7, 2018
Posts
22
Reaction score
51
Wakuu, heshima kwenu.

Lengo langu siyo kushambulia wala kudhalilisha, bali nikujaribu kuangalia uhalisia wa masuala ya ibada katika maisha halisi na matokeo yake.

Tangu nikiwa kijana mdogo kabisa, nimeshiriki ibada fulani kila mwaka. "Ibada ya kubariki mbegu" Kwenye dhehebu langu.

Kwenye ibada ile waumini wote tulikuwa tunapeleka mbegu tofautitofauti, kulingana na mahitaji ya kila mmoja wetu kwenye msimu huo wa mvua.

Sisi kwa mfano tulipeleka mbegu za mahindi, mpunga, pamba , karanga na maharage kwa sababu ndiyo yalikuwa mazao pendwa. Sambamba na mbegu pia tulipeleka zana za kilimo kama panga, majembe ya mkono na yale ya kukokotwa na ng'ombe.

Katika ibada hiyo mbegu ziliombewa sala maalumu ili ziweze kuleta mavuno mengi, sambamba na hayo kasisi aliomba kwa ajili ya hali ya hewa, hasa mvua kwa ajili ya msimu husika na kubariki vifaa vya kilimo ili pengine visiharibike au kisababisha madhara mengine.

Kilichonishangaza ni kwamba, katika mahubiri Kwenye ibada zile makasisi hawakuwahi kuzungumzia kuhusu umuhimu wa mbegu bora, mbolea na viuatilifu. Matokeo yake kwa zaidi ya miaka 30 (Tangu nianze kujitambua na kufikiri) tuliadhimisha ibada ileile kila mwaka bila kuacha, japo hatukuona matokeo yoyote shambani.

Umasikini na njaa ilikuwa jambo la kawaida kwenye jamii yetu.

Kitu cha kusitikisha zaidi ni kwamba baada ya mavuno tulihamasishwa tena kupeleka shukrani ya mavuno!

kutokana na ukweli kwamba tulifanya ibada kwa ajili ya mbegu kanisani Kwa hiyo hata kile kidogo na duni tulichopata tulilazimika kukirudisha kanisani, kama shukrani kwa Mungu!

👉KINACHONIWANGISHA KICHWA.

Inawezekana vipi kasisi msomi wa kiwango cha PhD. Akomae kubariki mbegu kila mwaka bila kuzungumzia kabisa umuhimu wa mbolea, mbegu bora na viuatilifu kwa waumini wake ambao kimsingi hawana elimu yoyote kama yeye? Pia ni maskini nà wanategemea kilimo tu?
👉Usiniambie wana PhD ya theology na nini sijui. Kwa watu waliosoma darasa la kwanza mpaka angalau kidato cha sita huwezi kushindwa kujua ABC kuhusu kilimo bora? ukajikita tu kubariki kwa miongo na miongo bila kufanya tathmini ya matokeo ya baraka hizo na bado ukawalazimisha maskini hao walete shukrani ya mavuno kanisani japo hawajapata matokeo ya maana!

Mwisho, natoa wito kwa wahubiri wa injili na mambo ya imani,
file_000000003a5c82109586bf011aad9a9b.png
kuacha kuishi kwa kukariri na kufuata kalenda za liturujia tu, Bali wakubali pia kutumia mimbari kuzungumza masuala anuai ya kitaalam kutokana na mahitaji halisi ya jamii, kama wanavyoweza kujadili siasa na maisha mengine nje ya imani.

#shetanianaogopamtuanayejuakitu.
 
Labda dini ya kiislam, kwenye ukristo kuna mafundisho mengi sana yanayopinga ujinga na umasikini. Kitabu cha Mithali kinatanabaisha hayo
 
Back
Top Bottom