Hata kama ni kuswali, ila huu si Ustaarabu jamani

Hata kama ni kuswali, ila huu si Ustaarabu jamani

Status
Not open for further replies.
Ni muda wa saa ngapi hicho kitendo hutokea? kinadumu kwa muda gani kikitokea?
Haihitaji hata kujua hayo uliyouliza, unafunga barabara ya umma kwani ni yako?

Shughuli gani muhimu kwa wanajamii wote pasi kujali dini inaendelea?

Jibu hapo, kila kanisa na misikiti ikiwa inafunga barabara itakuaje
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Ijumaa usipite njia hiyo. Ibada lisaa limoja. Mikesha na mazoezi ya kwaya + loud [emoji344] zipo karibu kila siku. Let's try to live in harmony.
 
Nyani haoni kundule.hakuna wanaokera kama hawa wanaopiga miziki using kucha daily eti wanaabudu! Kibaya zaidi ukichungulia ndani uwenda wapi 5 tu.
izi swala swala za saa 10 usiku, saa7 mchana, 10 jion, saa1 na saa mbili usiku unaziweka kundi gani?

Hivi hamuwezi kuswali bila hizo kelele za kila mda
 
242cc4e08ffb7bb18aacd87a4240cb1a.jpg
d835916bdd7b27df5e343252badd8c70.jpg
104e5ceb7d9b4cfb2ba593fc56d4527d.jpg


Naomba nianze kwa kudeclare interest kuwa hii sio Mada ya kukashfu dini.

Mi napenda kufikisha malalamiko kwa wahusika pitia JF.

Mwanza mtaa wa Lumumba imezuka hii tabia ya kufunga barabara muda wa ibada katika msikiti wa Lumumba. Binafsi sielewi sababu ya kuamua kufunga barabara ila ningependa kuzungumzia kero tunayopata baada ya barabara kufungwa.

Huu mtaa wa lumumba upo katikati ya mji wa mwanza na unabiashara mbalimbali zinazoendelea. Pale wenzetu wanapoamua kufunga barabara muda wao wa ibada kusema ukweli imekuwa kero kwa baadhi yetu maana hata biashara zetu husimama pia na hata kusababisha Traffic jam.

Mi ngependa kutoa ushauri kwa wahusika watafte njia mbadala ya kuhakikisha hii tabia ya kufunga barabara inakoma. Hivi kila msikiti na kanisa hapa mjini ukifunga barabara je itakuaje?


Mbona harusi mnaziba br hulamimiki?
 
Jifunze kuwa mvumilivu. Kama somo hilo wazazi wako hawakukupatia jifunze sasa usilete mambo yako ys udini humu...
 
Haihitaji hata kujua hayo uliyouliza, unafunga barabara ya umma kwani ni yako?

Shughuli gani muhimu kwa wanajamii wote pasi kujali dini inaendelea?

Jibu hapo, kila kanisa na misikiti ikiwa inafunga barabara itakuaje
Ukiongea hayo Angalia upande wako ni mangapi mnafanyia kero Jamii iliyokuzunguka labda uniambie huna dini. Sitabishana na wewe
 
Acheni kutugawa watanzania kupitia dini vyovyote iwavyo wote ni watanzania tofauti ya dini zetu isiwe sumu vichwani mwetu tuache chuki tuvumiliana na kupendana tukichukiana sote hatutobaki salama
 
Arabuni wanafanya ibada ya kufa mtu, bado Israel anawatandika kufa mtu! Huyo Mungu yuko wapi? Bakwata wamekosa mishahara, huyo Mungu yuko wapi? Kusali hakutawafikisha popote ni kupoteza muda tu!
Sasa kama wewe ni atheist, hiyo ndio njia yako unataka na wengine wakufuate wewe ili dunia iangamie? Wewe ni mfano wa watu waliopotea wanaoruzukiwa kwa hawa ya bure, na neema mbalimbali. Badala ya kushukuru wewe unakufuru. Haya kumbuka tu kuwa ulikuwa tone la manii, unakaa tumboni mwa mama yako ukikua hatua kwa hatua kwa uwezo wake Mungu. Sasa kama hutaki kuamini basi waache wenye kuamini waamini.
 
Kwanini mnafunga barabara?
Misikiti haitoshi ndani kudogo wakati waumini ni wengi.

Na nyie Kwanini Kwenye mikesha mfungulie spika hadi Mwisho? Hamuwez kukesha kimyakimya?
Vinanda na magitaa na zile kelele za mapambio unadhan wote tunafurahishwa navyo?
 
Kwani huwa wanaifunga kila siku hiyo barabara ama ni kwa ajili ya Siku ya Ijumaa tu pale waumini wanapokuwa wengi kuliko uwezo wa Msikiti? Pamoja na hilo Ijumaa yenyewe ni Wastani wa Nusu SAA hadi SAA 1 kweli ndo iwe Nongwa kiasi hicho Jamani? Hapana, tupunguze kuzoza Waungwana!!!
Hivi barabara kuu ya jiji ifungwe kwa saa 1 we unaona hakuna shida?hebu funga Nyerere road au tu ka block pale tazara kwa dakika kumi uone mziki! Arusha nako nimeona upuuzi unaofanana na huo,stendi ya mabasi madogo kilombero imegeuzwa uwanja wa injili,uganga wa kienyeji,na msikiti hapohapo! Viwanja vya wazi vimejaa kila mahali wewe unaenda kuendesha ibada Bus stand?au barabarani?
 
Pole mkuu ila ninaomba uwe mvumilivu maana ninadhani hiko kitendo hufanyika sehemu nyingi Tanzania lakini ni kwa siku ya Ijumaa tuu kwa muda wa kama nusu saa tuu.

Hata hivyo Waislam ni muda wa kuamka, sehemu au halmashauri ikitangaza viwanja vya kuuza Jamii ya kiislam inunue viwanja vya taasisi/ibada tena low density kama wanavyofanya upande wa pili, sio kusubiri mtu ajitolee eneo lake la nyumba na kuligeuza msikiti.
 
Hata hao wanaodiriki kufanya ibada kwenye jua, vumbi na adha nyingine kama hizo huwa hawafurahii bali ni kutokana tu namna hali ya eneo ilivyo na wao wanawajibika kutekeleza jukumu la kumuabudu Muumba wao katika yoyote.

Suala hapo ni kustahimili tu na kwa vile adha hiyo kwa watumiaji wa barabara ya mtaa huo ni muda mfupi tu mora moja kwa juma na pia ni mchana ambapo hata idadi ya watumia barabara hupungua ukilinganisha na muda wa asubuhi au jioni.
 
Kuna mabasi yanapiga kwaya mwanzo wa safari mpaka mwisho bila kujali kunaabiria wa dini nyingine humo.kuna waumini wanapanda kwenye mabasi na kuhubiri ulishasikia? Ni kuvumiliana tu hapo tusigusie walokole!
 
Hii ishu inazinguaa afuu na Viongozii pia wanaangalia tuu...!! Wewe kuswali kwako usitupee shida sisi...si Mjenge misikiti mikubwaa... na asubuhi yalee mavipaza sauti huwa yanakeraa sanaaaaaaa...sanaaaaaaaaa...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom