Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 18,030
- 25,015
Halafu naona kama huyu jamaa amebebwa kweli na wala sijawahi ona jambo linaloashiria kuwa ni mchapa kazi kuliko wengine wote kiasi cha kudumu katika uwaziri kwa miaka yote 25 iliyopita. Sijawahi kumsikia akiongea na watu anaowaongoza labda kama huwa anafanya hivyo kichini chini tu- jambo pekee linalokuja haraka kichwani mwangu ni pale alipokuwa mbele kufukuza madakari Muhimbili badala ya kuongea nao na kuwatuliza; kiukweli hata sijui sauti yake. Tangu amalize shule hakuwahi kufanya hospitali yoyote; yaani alitoka shuleni tu, Mkapa akambeba kuwa naibu waziri - sielewe kama ilikuwa ni kumfurahisha mzee mwinyi ambaye alikuwa karithiwa na Mkapa, na kuanzia hapo hajawahi kutoka kwenye uwaziri.Nimeona leo Hussein Mwinyi kachukua form huku tetesi zikisema ndo chaguo la chama kurithi Urais Zanzibar..
Watoto mara nyingi Wana kawaida ya kupenda kurithi kazi za Baba zao..ingawa sio wote wanaweza..na mara nyingi watoto hupata wepesi wa kufika Kwa msaada wa Baba au marafiki wa baba..ingawa mara nyingi huwa na uwezo duni kulinganisha na Baba zao..
Ila katika hao watoto mara zote sio wote hurithi uwezo au vipaji vya baba zao..
Mara nyingi ni mtoto mmoja ndo anakuwa.
Amerithi kitu au vitu kutoka Kwa baba yake...wote wanaweza fanana Sura na Baba
Lakini mmoja akarithi 'natural leader'
Mwingine akarithi ucheshi ..
Nadra Sana kurithi kila kitu ....
Sasa katika watoto wa Mwinyi nimewahi msikia Hassan Mwinyi akiongea wakati anagombea ubunge Afrika mashariki..
Nikasema 'huyu ana kitu'..
Nimemsikia sana Hussein Mwinyi akiongea
Mara Kwa mara sijawahi 'feel 'kiongozi anaongea...
Mtoto mwingine wa Viongozi hasa Zanzibar akiongea unajua huyu ni 'kiongozi'..ni Mohamed Thabit Kombo...vipaji vya wazi
Ambavyo vingetazamwa na kundelezwa wangekuwa 'viongozi wazuri ' zaidi...
Hussein sifa ya utiifu ndo inambeba
Na utiifu sio sifa kubwa saana ya Uongozi..
Watoto ambao wanakuwaga 'wild'mara nyingi huja kuwa Viongozi wazuri zaidi Kwa sababu angalau wataweza 'decision making'..kuliko watiifu ..ambao ni rahisi kushindwa kuamua au kutii bila kuuliza..
Watu wengi huwapa huwapa special treatment 'first born 'na kipaumbele ingawa huja kugundua very late walikosea.
Mwenye kipaji ni second born au third born..wakiwa washafanya kosa..
Wazazi wa George W Bush walijua Kwa uhakika second born Jeb Bush angeweza kuja kuwa better Leader zaidi ya first born George..wakiwa tayari washachelewa..
Hata Zanzibar Ally Karume ni more 'natural leader ' kuliko Amani lakini ..washachelewa....
Na hata familia ya Kikwete ..Miraji anaonekana more natural leader kuliko Ridhiwan lakini Ridhiwan atapewa kipaumbele..the list is long.
Atakapokuwa Rais.. Hussein nna uhakika atalaumiwa Sana Kwa 'indecision' kuliko Kwa decisions...na maswali kama ni kiongozi mwenye mamlaka au anapokea maagizo yatajitokeza.
Hassana Mwinyi au Mohamed Thabit Kombo wangefaa zaidi but ..too late..
Kwa Zanzibar, mimi nilikuwa namwona Major General Issa Suleiman Nassor angefaa sana; ni kiongozi mzuri sana ukichukulia jinsi alivyokuwa anaongoza kamandi zake jeshini, na vile vile amweahi kufanya kwenye balozi zetu za India na Misri; sijui sasa hivi yuko wapi.