Hasira zinaniharibia mahusiano

Hasira zinaniharibia mahusiano

KFC?? Hapana
Basi punguza ujuaji,ujuaji na kutaka kushindana kwenye kila jambo na Mwanaume wako vinakucost,
Usisahau na kutafuta hela,pia fanya mazoezi na uwe na muda wa kupumzika,usijiweke bize sana na usiwe na magrp mengi ya WhatsApp/Social media ambayo mkigombana huko,hasira zako unazihamishia kwa dume lako.
 
Hakuna shida, umenifanya nijione siko peke tunaohitaj kupona
Hakika.
Hasira ni jambo moja, ila kufuata hasira inavokutuma ni jambo jingine.

Ni sawa na mtu mlevi anayeamini kuwa kuna baadhi ya matendo anayoyafanya yanapelekewa na pombe anazotumia. Ila mimi nimejenga imani tofauti.

Ukija kujichunguza utagundua kuwa pamoja na hasira zako lakini wewe ni mtu unayejali sana. (Concern, compassion) Ila kauli unazozitoa ukikasirika hupunguza kujiamini kwako na pia huondoa nafasi yako na uaminifu wako na huvunja malengo yako ghafla. Kumbe tatizo sio hasira. Tatizo lako ni kauli. Unaweza kukasirika na ukazichunguza kauli zako.

Mie mwanzoni nilikuwa najizuia kuongea nikikasirika, ilikuwa inasaidia ila mwanzo nilikuwa naharibu nilicholishika au najiumiza mikono kwa kupiga ukuta. Ilifika wakati nikaweza kumudu hasira ndani kwa ndani bila mabadiliko usoni wala bila viashiria vya kauli za maudhi.

Inawezekana
 
Hongera yaan nakuonea raha
 
Nenda kwa wataalam kwanza wakusaidie kuishinda hasira, maana hilo ni tatizo la ndani ya nafsi, siyo nje. Watu wanaweza kukuona u binti mrembo sana, lakini huo urembo si lolote kama ndani ya nafsi kuna wadudu kama hasira, kiburi, fitna, wivu, husda nk... Ukiweza kuyatia kapuni hayo mambo mahusiano yatakua rahisi mno.
 
Hello,

Nafahamu kwenye wengi kuna mengi, tuachane na huu msemo. Naomba mnisaidie jinsi ya kukabiliana na hasira.

I broke up with 2 people kwasababu ya hasira, tena hasira zangu huwa ziko complex. Mfano sioni shida kumwambia mtu tuachane kisha naanza kuumia mwenyewe. Nikijaribu kurudi nakuta block kubwa yaani kufuli kubwa sana.

Nataman kuwa na mahusiano but hayadumu kwasababu ya hasira. Nisaidieni nipone.
Muombe Mungu akuepushe na hiyo roho,inaweza kukutesa maisha yako yote...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom