hasira+wivu...

MESSI

Member
Apr 3, 2011
38
2
habari zenu wana-jamvi!
Eti unawezaje kumshauri mtu jinsi kupunguza hasira(i mean kukasirika haraka au hasira kali) na kuwa na wivu kupindukia hasa ktk mapenzi??..nawasilisha.
 
mwambie aacha hasira na wivu wa kupindukia,..full stop
 
Hata mimi kuna kipindi nilikuwa na tatizo unalosema,lakini nipogundua nina negative nyingi kuliko positive ilinisaidia sana...........nilikuwa hata nikipiga simu isipopokelewa hasira ,akichelewa hasira yani toka nimejifunza amechelewa ni story zilinoga walaaaa.
 
Mwenyewe mwenye matatizo anatakiwa aichukie hiyo hasira, ndipo anaweza kujitoa huko
 
hiyo rahisi, dawa ya hasira ni kiburi+jeuri, mtu mwenye hasira za ajabu ajabu anatakiwa akutane na watu kama 20 wenye jeuri na kiburi ya kutosha, ikitokea ni wapenzi wake atajuta kuzaliwa, mwisho wa siku ataona bora awe priton ndani ya pipa.
 
habari zenu wana-jamvi!Eti unawezaje kumshauri mtu jinsi kupunguza hasira(i mean kukasirika haraka au hasira kali) na kuwa na wivu kupindukia hasa ktk mapenzi??..nawasilisha.
Mtu mwenye hasira mwambie ajue kosa analofanya binadamu mwenzake kesho atarudia kufanya yeye pia hasira ni dalili kubwa za kutojiamini na kuficha kutojiamini Huko nyuma ya kitu Fulani kama pesa au mamlaka au mapenzi fake.Mtu mwenye wivu kupita kiasi mwambie mapenzi ni sawa na usiku Wa kiza Kwani huwezi kujua kilichopo ndani ya moyo Wa mwenzako bali utaishi kwa kuhisi. Ni ujinga kuwa na wivu Wa kupindukia kwa jambo unaloamini kwa kuhisi. Mwambie asubiri siku tutakayoweza soma yaliyomo katika mioyo ya wapenzi wetu.
 
...ukishaweza kujua kwanini unakuwa na hasira na kwanini unakuwa na wivu, tayari ushapiga hatua moja ya kudhibiti hasira na wivu wako. Hatua ya pili ni kutafakari na kuchukua hatua za kupunguza hizo hasira na wivu.
 
Hata mimi kuna kipindi nilikuwa na tatizo unalosema,lakini nipogundua nina negative nyingi kuliko positive ilinisaidia sana...........nilikuwa hata nikipiga simu isipopokelewa hasira ,akichelewa hasira yani toka nimejifunza amechelewa ni story zilinoga walaaaa.
Ulichosema hapa nakikubali Chauro! Mawazo hasi juu ya mwenzio huwa yanaishua kukuuimiza mwenyewe tu! Its a good learning which I will appreciate ever! Wivu hauwezi kuisha kwa mtu umpendaye ila tu basi sio ndo hata bila sababu za msingi basi ushajiskia wivu! (ngumu aisee kutoona wivu kwa umpendaye) Unaweza kupata uchizi bure, kujiweka roho juu kila wakati.
 
hhha hha,...unataka kuni Restisha-In-Peace?
Mkumbushe jamaa, Hasira na Hasara vinaendana pamoja.

Unaona tena...i was going to quote that semi, umeiandika tena..i will write it however;

"Hasira, hasara." - Wahenga
 
  • Thanks
Reactions: Mbu
hiyo rahisi, dawa ya hasira ni kiburi+jeuri, mtu mwenye hasira za ajabu ajabu anatakiwa akutane na watu kama 20 wenye jeuri na kiburi ya kutosha, ikitokea ni wapenzi wake atajuta kuzaliwa, mwisho wa siku ataona bora awe priton ndani ya pipa.
haha mkuu umenichekesha..nashukuru kwa mchango wako
 
Ulichosema hapa nakikubali Chauro! Mawazo hasi juu ya mwenzio huwa yanaishua kukuuimiza mwenyewe tu! Its a good learning which I will appreciate ever! Wivu hauwezi kuisha kwa mtu umpendaye ila tu basi sio ndo hata bila sababu za msingi basi ushajiskia wivu! (ngumu aisee kutoona wivu kwa umpendaye) Unaweza kupata uchizi bure, kujiweka roho juu kila wakati.
huu ni ukweli kabisa..lkn wivu nao ukizidi sana inakuwa karaha.
 
Mtu mwenye hasira mwambie ajue kosa analofanya binadamu mwenzake kesho atarudia kufanya yeye pia hasira ni dalili kubwa za kutojiamini na kuficha kutojiamini Huko nyuma ya kitu Fulani kama pesa au mamlaka au mapenzi fake.Mtu mwenye wivu kupita kiasi mwambie mapenzi ni sawa na usiku Wa kiza Kwani huwezi kujua kilichopo ndani ya moyo Wa mwenzako bali utaishi kwa kuhisi. Ni ujinga kuwa na wivu Wa kupindukia kwa jambo unaloamini kwa kuhisi. Mwambie asubiri siku tutakayoweza soma yaliyomo katika mioyo ya wapenzi wetu.
nashukuru kwa mchango wako its vry helpful
 
watu tunaongea tu
but ukijua mwenzio ana wivu juu yako inatia raha
Wivu peke yake hausumbui lakini unapozidi na kunyimwa uhuru inaboa..., alafu si ukweli kwamba wivu ndio unaonyesha upendo, mwingine anapenda tu ile possession hata kama hakupendi
 
Dawa ya hasira na wivu iko kwenye kuelimika kuwa hasira na wivu ni negative emotions na kwa kanuni na sheria za negative emotions ni kuwa.

1. Negative emotions is magenetic to what caused it ... hasira, wivu chuki nk ukizalisha zina vuta na kushikilia kile kilichozichochea. Ukitishwa na Paka mkubwaaaa ..ukaogopa, kukasirika nk anakufuataaaa...

Ni mjinga tu anaweza kukasirikia TABIA YA MPENZI wake huku akijua fika tabia hiyo anakuwa anidumisha na itamfuata hata akibadilisha Mpenzi mwingine.

Wivu ni sumaku ..ukiwa na wivu ..kuwa atachukuliwa nk ... Kila Rafiki utakayekuwa naye atachukuliwa nk ...ili kutimiza sheria na kanuni ya wivu. usimlaumu yeye anachukuliwa kwa sababu ya ujinga wako ... wivu wako unakamilisha kanuni zake. unamfanya achukuliwe nk!!

2. Hasira na wivu ni programmer . Vinamprogram anaye zizalisha kuwa infirior... yaani kuwa MNYONGE kwa huyo unayemuelekezea hasira na wivu.

Kila unapozalisha hasira na wivu kwa mpenzi wako ... kwa maneno machahe wewe ni myonge wake na atakuendesha kama gari bovu!!
 
watu tunaongea tubut ukijua mwenzio ana wivu juu yako inatia raha
Alaah hivo eeh?Ss wengine wivu wetu hadi unakua nuisance aisee! Lakini kwa kweli kama humpendi mtu wivu unatoka wapi? Sema tu kiasi sijui ni kipi?Btw: wivu na hasira lazima viende pamoja?
 
Alaah hivo eeh?Ss wengine wivu wetu hadi unakua nuisance aisee! Lakini kwa kweli kama humpendi mtu wivu unatoka wapi? Sema tu kiasi sijui ni kipi?Btw: wivu na hasira lazima viende pamoja?

wivu tu bila hasira ndo raha
mimi mwanamke asieniuliza kwa nini msichana fulani anakuchekeachekea ntaona hanipendi..
mwanamke akiwa na wivu anakuwa more sexy
 
Back
Top Bottom