Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,613
- 18,840
Kuna Uzi humu nimeuona jana unaongelea ongezeko la watu wasio na hofu ya Mungu mtaani
Ki msingi ni kweli hata humu mtandaoni maneno ya Mungu yenye kutumika kama meme ni mengi lakini pia hata watu walio asi kwenda misikitini na makanisani idadi yao ni kubwa pia.
Mtaani watu kujichukulia Sheria mkononi imekuwa ni kitu rahisi mno,na wamama ambao miaka mingi wameimbwa kama watu wenye huruma na upendo nao wamebadilika hawana uchungu tena wanaua,wanatesa na kutweza utu wa watu.
Ni juzi kati kuna afande alituma watu wakabake binti kule yombo kisa anatembea na mumewe.
Ni wanawake hawa wanaongoza kupiga kelele za wizi na kusababisha mtu kupoteza maisha.
Mwishoni mwa mwaka Jana tumempoteza msanii aitwaye Man dojo kisa tu kuitiwa kelele za mwizi.
Chanzo kikidaiwa ni mwanamke
Sasa hivi maiti hazistui ,hazitishi kama zamani ,macho yetu na roho zetu zimezoea ni kawaida tu siyo kama zamani,ukiona tu jeneza Moyo unakosa Amani.
Lakini swali la kujiuliza,
Unajisikiaje kuwa chanzo cha kutoweka uhai wa mtu mwingine?
Kuna picha tangu Jana zikionesha afande wa jeshi akimuangushia kipigo mtu anayedaiwa alimdhulumu pesa.
Lakini kutokana na kipigo kile inaonesha Yule dhulumat amefariki,
Swali ni kwanini afande ,msomi,mwenye kutambua haki za binadamu kufanya haya ?
Sasa analindq nini ikiwa atashindwa kutetea haki za raia?
Kwanini baada ya kumuarrest asingemfikisha kwenye vyombo vya Sheria?
Inadaiwa Yule dhulmat alianza Kwa kurusha jiwe ,je hata kama alifanya hivyo afande hakuwa na njia nyingine ya kumkabili opponent wake mbali na kupiga?
Sasa dhulmat ni marehemu kanyimwa haki ya kuishi kutokana na utapeli wake.
Na afande ni mfungwa kajinyima Uhuru wake wa kutumikia taifa lake aliloapa kulilinda ni dhahiri anaenda kuwa punda anayetumikishwa.
HASIRA HASARA