Ndoa yangu iligharimu sh 36000 tu!.Tulikwenda asubuhi siku ya ijumaa kanisa la hananasif kinondoni,nikiwa Mimi mke wangu na wasimamizi wawili.Mimi si mvaaji tai,ila niliazima kwa muangalizi wa ng'ombe wetu pale Nyumbani.Shela tulipewa na msimamizi wa mke wangu.Me nishapanga siku ya ndoa me na mke wangu best man and woman, ndugu ataependa. Tunafunga ndoa asubuhi then kila mtu na shughuli zake, jioni tunaenda bar ya karibu Kula Bapa na nyama. Biashara ya ndoa kwisha.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nimecheka kwa sauti... mkuu are you serious?Unaamua kufanya kitu tofauti..
Kuna social grounds kibao kwa DSM, Pata wapambaji local, si lazima ukodi professional, piga nguzo na Turbai, weka tujipambo uchwara, tandika mkeka, kafunge ndoa kanisani, mkirudi pigeni kashata na sharbati ya ukwaju...
Waalike watoto wa kitaa waruke ruke hapo siku ipite..
Usisahau mabaunsa wa kulinda usalama.
Ndoa inafungwa madhabahuni. Harusi ni ubongo wako na mwenzi wako. Ushawahi kuona kanisa linauliza bajeti yako ya harusi? Ama hujui tofauti ya ndoa na harusi?Wakuu,naheshimu mkataba wa milele wa ndoa ya kikiristo,na sio mshabiki wa ufahari wa siku moja.
Naomba ya jinsi gani nifanye sherehe ya harusi isizidi milioni moja, labda kuna watu wengine walishafanya hivyo.
nahitaji msaada wenu,najua mchanganuo wenu utakuwa msaada kwa wengi pia.
Mungu awabariki sana
I'm serious brenda18 , just making something different...[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] nimecheka kwa sauti... mkuu are you serious?
Khaaa. ..hakika wee mpare kiboko (joke) [emoji13] [emoji12]maladhi ni nini? wakitaka keki wapinguze idadi ya watu,
halafu hivi ndoa hapa duniani ni keki? kukariri maisha kiasi hiki sio kabisa! wanunue hata kuku choma wa 20k akatwe fresh walishane ndoa sio keki jamani nyama ya kuku ikiwekwa sahani classic ni tamuu kuliko hiyo misukari kwenye keki!
wasimamizi wavae nguo zao wanazovaa kanisani siku za jumapili.
Maadam umejibu vizuri sana.yaani nimekupenda bure, ita watu wachache upande wako na wa mke, tafuta ka hotel flan ambako chakula na vinywaji 2 havizidi sh. elfu 15 waambie labda kuna wateja 40 kwa masaa 3 wataandaa high table simple, fungeni ndoa kanisani elekeeni pale mkitoka kila mtu kwao.
nikimpata wa hivi nitafurah sana
Natamani mualiko kwy hiyo harusi aisee maana hata Muheshimiwa Sana anasubiri kwa hayo matumizi.Kwa ufinyu wa budget, wanafamilia watajitolea kupika, mchele kilo 15- 50,000, nyama kilo 5 = 30,00 salad 20, gas au mkaa wa kupikia 30, 70,000 vinywaji soda na juice. total laki mbili.
Maadam umejibu vizuri sana.
mimi bado sijaamua kuoa ila siku nikioteshwa kuoa ntafunga harusi ya bei ya chini sana, kwanza sitachangisha mtu.
nitafunga ndoa kanisani nitaenda hotel kupumzika.
ntampa mke wangu kadi ya watu ishirini tu na mimi watu 30 tu,
nitakua nimeeandaa mahali kutakua na vunjwaji na nyama choma, kutakua na mziki laini nitaingia nimevaa jens yangu safi na tsht. namtambulisha mke wangu tunagonga cheers then kesho naruka kwenda H.moon ya maana mahali.
hakika hata miloni 4 haiiishi
wewe uki pm inagoma eti??
sio bure yaani hiyo ni kila kitu mpka mahali.mil. 4 ya nini! hebu fanya mil. 1 hiyo mil 3 fungua hata m pesa 2 uweke acount za mtoto msifurahishe watu! hotelini mkienda mnahudumiwa bureeee
Sent from my TECNO_P5_PLUS using JamiiForums mobile app
Hiyo ndoa njoo ufungie huku kwetu Namanyele ukumbi ni bure ila umejengwa kwa matete juu na chini,ndani tunakalia magogo,
Vinywaji vya hapa zaidi ni pombemwitu ambayo debe moja ni sh elfu 4
Hiyo milioni itatosha na kubaki!
Nimeipenda sana hii, hakika ntafanya hivyo, mambo ya kuchangishana ni kupoteza muda tu na kubaki na madeni kibao mtaani.Ndoa yangu iligharimu sh 36000 tu!.Tulikwenda asubuhi siku ya ijumaa kanisa la hananasif kinondoni,nikiwa Mimi mke wangu na wasimamizi wawili.Mimi si mvaaji tai,ila niliazima kwa muangalizi wa ng'ombe wetu pale Nyumbani.Shela tulipewa na msimamizi wa mke wangu.
Baada ya ndoa nilimkodia taxi mke wangu iliyomrudisha Nyumbani ,mi nikatia tai mfukoni nikaingia mtaani kusalimia rafiki zangu.
Jioni nikanunua kreti moja la bia na kuwaita marafiki zangu watatu,sikutaka kishirikisha ndugu wala walezi wetu,kwa upande wangu au wa mke wangu,kwa vile nilipingana na mpango wao wa kutaka harusi iwe ya gharama.
Bank nilikuwa na 470000,baada ya kumaliza harusi,nilitumia pesa hiyo kununua kabati la nguo kubwa,pale mivinjeni na hadi leo ninalo.Na mke wangu ninaye hadi sasa,ndugu walilamika lakini bàadae walinielewa.
Ndugu yetu uliyetaka ushauri ukiwa na roho ngumu na ya kijasiri,unaweza Fanya hiyo ndoa hata 200000 isifike.
Jiulize nini maana ya ndoa,je ni lile tendo la kuunganishwa nyie wawili kwa mungu,au ni sherehe ya kila mtu ale anywe na kusaza.Kwa taarifa yako Sifa za kusifia shughuli yako huiishia palepale ukumbini,na ikiwa ulishindwa kuwakirimisha waalikwa basi ubovu utatangazwa kila mahali na kwa muda mrefu.Na Usisahau utapoteza muda mwingi sana kufuatilia michango kwa watu.
Habari ya kufanya sherehe Mara nyingi huacha makovu kwa nyinyi wanandoa,mkishafika Nyumbani,mnaweza kujikuta mna madeni,huku mkihitaji kununua chakula,vyombo,kodi ya nyumba kama umepanga.Kumbe ungeweza kuwa jasiri kwa kufanya kitu kidogo na kusave pesa na kufanyia mambo mengine ya maana.Hebu watanzania tubadirike
Madam mchanganuo wako mzuri lakini umesahau bajeti ya wasimamizi, keki na maladhi kwa wanandugu
Tena ikiwezekana bibi harusi anaaza kukoroga pilau saa 11:00 asubuhi kabla ya kutengeneza nywele, ndio kanisani.Natamani mualiko kwy hiyo harusi aisee maana hata Muheshimiwa Sana anasubiri kwa hayo matumizi.