Harusi ya Kikiristo isiyozidi Milioni 1

Harusi ya Kikiristo isiyozidi Milioni 1

Juz kaka yangu kaoa ndoa kanisani laki saba bajeti na imefana
 
inawezekana fungeni kanisani, hiyo milioni mnatumia laki moja honeymoon, tisa ndo mnafanya maisha.
 
Wakuu,naheshimu mkataba wa milele wa ndoa ya kikiristo,na sio mshabiki wa ufahari wa siku moja.

Naomba ya jinsi gani nifanye sherehe ya harusi isizidi milioni moja, labda kuna watu wengine walishafanya hivyo.

nahitaji msaada wenu,najua mchanganuo wenu utakuwa msaada kwa wengi pia.

Mungu awabariki sana
Mi nadhani inawezwkana... Ukitaka iwe simple. Kama mna uwanja wa wazi kwenu mnaeza pamba hapo sio lazima ukumbi. Unaeza ukawa na rafiki anaeweza kazi ya MC N.K ,Unagharamia sana chakula na vunywaji na nguo.
 
Wakuu,naheshimu mkataba wa milele wa ndoa ya kikiristo,na sio mshabiki wa ufahari wa siku moja.

Naomba ya jinsi gani nifanye sherehe ya harusi isizidi milioni moja, labda kuna watu wengine walishafanya hivyo.

nahitaji msaada wenu,najua mchanganuo wenu utakuwa msaada kwa wengi pia.

Mungu awabariki sana
Nicheck inbox nina uzoefu na hii kitu.
 
wewe unataka ndoa au sherehe ya ndoa? kama ni ndoa mbona haizidi 1M manake padre akisema u may kiss the bride ndo mshamaliza tayar mshakuwa mke na mume nyingine zoote mbwembwe tu

Kuna jamaa yangu anaoa this week nashugulikia taratibu za harusi pia, tumeamua kuondoa sherehe ya harusi instead tukitoka church tunaenda piga picha kwenye hoteli flani ya ukweli then tutapata chakula kwenye open space ya hiyo hoteli na tutawaacha hapo maharusi wale fungate yao

gharama ya kupiga picha kwa 30ppl ni laki2.5 kutokea laki3 waliyotaka wenye hoteli, na msosi na vinywaji ni laki 6 na kulala 3days ni laki3.6. plus mafuta kwenye gari zetu 6 hazizidi laki3 kwa misele yoote ya siku hiyo!

tumebakisha suala la mpiga picha na mrembaji tu!

Harusi yoote haitazidi 3/4M ila itakuwa ni kwa invited guests pekee na itakuwa ya ukweli zaidi ya kufanyia ukumbini
Na hichi kitu naona kinakuja kwa kasi. Yupo ndugu yangu na nimeona wengine pia wakifanya namna hii.

Unasave gharama zisizo za lazima kwakweli
 
mziki laki na nusu.
chakula unapika mwenyewe laki 3
ukumbi nyumbani. kwa ndugu au sehemu yoyote ambayo kuna nafasi na hutotumia gharama.
keki au ndafu isizidi efu hamsini.
mapambo hom tu kisela laki.
viti maturubai lets say laki na nusu.
mc kisela isizidi laki. au kama una ndugu jamaa anaweza si mbaya free.
usafir laki. kwa gar la maharusi.. wengine watajichanga tu siku hyo hyo kwa ajili yao wenyew

inayobaki vinywaji. ...bia si lazima.....
 
Maadam umejibu vizuri sana.

mimi bado sijaamua kuoa ila siku nikioteshwa kuoa ntafunga harusi ya bei ya chini sana, kwanza sitachangisha mtu.
nitafunga ndoa kanisani nitaenda hotel kupumzika.
ntampa mke wangu kadi ya watu ishirini tu na mimi watu 30 tu,

nitakua nimeeandaa mahali kutakua na vunjwaji na nyama choma, kutakua na mziki laini nitaingia nimevaa jens yangu safi na tsht. namtambulisha mke wangu tunagonga cheers then kesho naruka kwenda H.moon ya maana mahali.

hakika hata miloni 4 haiiishi
na wenzetu wazungu mbona ndo inavokuaga.
 
yaani nimekupenda bure, ita watu wachache upande wako na wa mke, tafuta ka hotel flan ambako chakula na vinywaji 2 havizidi sh. elfu 15 waambie labda kuna wateja 40 kwa masaa 3 wataandaa high table simple, fungeni ndoa kanisani elekeeni pale mkitoka kila mtu kwao.

nikimpata wa hivi nitafurah sana
Nipo wala usitie shaka maisha ni magumu mambo ya kufanya harus bajet million kum usawa unabana
 
Kwani jamani ukienda kanisani jioni ukaenda sehemu na watu wasiyozidi 20 mnajipongeza ndoa haiwi jua matarumbeta mbwembwe tu.
 
Wakuu,naheshimu mkataba wa milele wa ndoa ya kikiristo,na sio mshabiki wa ufahari wa siku moja.

Naomba ya jinsi gani nifanye sherehe ya harusi isizidi milioni moja, labda kuna watu wengine walishafanya hivyo.

nahitaji msaada wenu,najua mchanganuo wenu utakuwa msaada kwa wengi pia.

Mungu awabariki sana
ndoa sio sherehe.ni ww kwenda kanisan na mwenza wako nakufungishwa na padre cha zaid ni sadaka na gar la ndugu wakuja kushuhudia muungano wenu but the rest from hapo n anasa za dunia
 
Kuna jamaa mmoja alioa mwezi wa 3 na alinialika baada ya kuwa tunakutana nae hapo hotelini kuangalia mpira, jamaa sherehe ya harusi yake hata milioni 2 haikufika na waalikwa tulikua kama 50, na kwa bei ya vyakula pale ni 10,000 ~ 20,000 na ilikuwa ni kwa masaa 2 tuu siku moja kabla tulitumiwa menu ya vyakula na vinywaji hivyo tulipaswa kuchagua chakula na kinywaji utakachotumia, ndicho utakachoandaliwa na kujibu kwako ndio confirmation. ilikuwa nzuri sana

Hamna MC, zawadi kama umekuja nazo za kubebeka wameweka gari nje unaweka na ku sign, dk kama 15 za kutambulisha wazazi n.k mwisho kabisa kama mtu anazawadi ya maneno aliomba kuongea.
 
karibu,
ukiita watu 19 upande wa mke, 19 upande wako plus ninyi 2 ni 40
40×15= 600000, laki nne mke gauni simple elf 60, viatu 30, nyele akaset kawaida elfu 10 achane mtindo mzuri tu apake poda na wanja mwenyewe au saloon hapo hapo bila kuwaambia ni bi harusi hawatampiga bei

, wewe chukua kiatu elf 35, suruali nzuri 30, shati moderate 20, saloon nyoa ya buku 5 ten ilobaki tafuta kajitai kalofanana na gauni la mke basiii
laki 2 ilobaki safirisha hao watu kwa coster kwenda hapo ninyi tax to and from mfano 30 coster 170
itatosha hiyo milioni kabisa
[emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] [emoji12] safi sana!! Hii iko sawa
 
1.funga ndoa kanisan
2.pika masufuria 5 ya pilau nyumban kwako.
3.usafir ni fuso au toyo
4.hakuna honeymoon
5.mengine baadae
 
Wazo zuri tena la kijasiri! Chukua ushauri wa wadau hawa waliokusapoti

Maana sherehe zenyewe za ukumbini zinaboa sana sku hizi,,,,watu wako bizy kuchat hata hawafatilii kiachoendelea maana ratiba ni ileile tu ya sku zote tena chakula umetumia mamilioni watu wanadonoadonoa tu kinamwagwa shubaaaamit😡
 
Mahari nitatoa mkuu,je haiwezekani kupata kajiukumbi ka gharama nafuu?
Hapo ndipo unapokosea,
Mimi ni muumini wa kutokufanya sherehe kabisa.Unaposema huhitaji sherehe basi iwe kweli.
Sasa fanya hivi pata mahali pakutosha hata kama ni Sebule tu nyumbani kama inanafasi basi inatosha.

Mimi sijui wewe ni dhehebu gani lakini kama ni mroma nenda ufunge ndoa misa zile za asubuhi saa 12 hili ni jambo la dk 15 tu.

Hapa utakua na wale ndugu wa muhimu kama mashangazi wajomba na kadhalika ili tu washuhudie na wala haihitaji ukanunua piere kardin wala suti nenda uvae vile unavyotumia siku zote achana na gharama zisizo na msingi.

Baada ya hapo mnarudi nyumbani hasa kutambulishana na kupata chakula na vinywaji kwa wale uliokua nao kanisani hasa wageni upande wa mwanamke na ndugu wamuhimu tu mchezo umeisha.

Budget hata 500,000 haishi mtu huna hata ka plot unaenda kupoteza pesa kwenye mambo ya hovyo.
 
Bas usifanye sherehe kubwa pika tu chakula ita ndugu wa karibu na marafiki bas ndo hyo ela itatosha coz kwa sherehe kubwa iyo 1m ni ya ukumbi tu au mapambo tu bajet ya sherehe ni kubwa sana
 
Back
Top Bottom