Harmonize ft Diamond Platinumz - Bado

Harmonize ft Diamond Platinumz - Bado

Well done WCB.Kazi ni nzuri.

Tatizo langu mim ni kwa Diamond,kwanin anasahau tofauti ya kumpa mtu samaki na kumfundisha kuvua samaki?
Huyu dogo bado anahitaj kuwaaminisha watu kuwa anaweza akiwa mwenyew kabla ya mbeleko.
Hii ni hatar mana kuna kesho,na pia ukibebwa sana mgongoni huwez ona machungu ya safari.Ni kweli anatumia njia fupi kumkuza kijana wake lakn hii njia haimjengi.

As nnavyoziskia hata interview za huyu dogo naona kabisa bado ameshikiwa akili,hana personal say na ni kama hukarilishwa vitu vya kuongea.
Lift ikizidi inapumbaza,Hata Diamond alitoa album peke'ke kabla ya kupata boost ya Davido.

Cha mwisho,mtayarishaj wa mdundo ana credit zangu tayar.Alopuliza ile tarumbeta ndo kabisa katisha.Pia nasubir kuskia video imefungiwa mana Basata wao kila kitu kinavunja utamaduni kwao.
 
Back
Top Bottom