Harmonize ameuliza, tumjibu!

Mungu Kama yupo au kama hayupo, mimi hainihusu!

Huyu Mungu hanisaidii kwa chochote, wala hanisaidii kwa lolote!
Maisha yangu hayahitaji wala hayategemei Mungu.
Ipo siku utamjua mungu ni nani
 
Mungu Kama yupo au kama hayupo, mimi hainihusu!

Huyu Mungu hanisaidii kwa chochote, wala hanisaidii kwa lolote!
Maisha yangu hayahitaji wala hayategemei Mungu.
Nacheka lakin naogopa
JamiiForums-213931961.gif
 
Konde Gang, msanii wa Bongo Flava ameuliza kwenye wimbo wake wa dunia, kuwa ni kwa nini watu wanaokesha kusali misikitini na makanisani wana hali mbaya kiuchumi, wana maisha mabovu, hawapati baraka ambazo Biblia na Quran imeahidi kwa waumini wake, kama ambavyo Wayahudi na Waarabu wa kale walivyopata?

Anauliza kuwa ni kwanini kila kitu kizuri kinaitwa ni cha shetani?!

Haya wanajamvi tumjibu!
Kwanza siyo kweli ya kila kitu kizuri kinaitwa cha Shetani. Kwa munasaba huu huyo msanii hana achokijua juu ya jambo hilo.

Ukweli ulivyo maovu yote yana hasara kubwa kuliko faida,angalia zinaa,tazama pombe,kadhalila angalia starehe zote amabzo hiyo msanii anaona ni vitu vizuri vina madhara makubwa kuliko faida,sasa huyo msanii ameonyesha kiwango kikubwa cha ujinga kwa kuona ya kuwa starehe na maasi ni katika vitu vizuri.

Lakini kuhusu maisha mazuri si kweli ya kuwa watu wa dini huishi maisha ya dhiki wapo wa hali zote.
 
we umemjuaje huyo mtoa pumzi!?. anaenipushana hayo magonjwa deadly, mbona wengine anawapa!?.
Amekuchagua wewe akupe neema, yeye anampa amtakaye kwa sababu anazozijua yeye.! Kama unakiri kuna miujiza, na ushetani duniani, basi kiri uwepo wa Mungu pia, hujiulizi kwa nini majini yanalipuka likitajwa jina LA Yesu? Jibu ni kuwa, huo ni ushahidi tosha kuwa Mungu yupo.
 
we umemjuaje huyo mtoa pumzi!?. anaenipushana hayo magonjwa deadly, mbona wengine anawapa!?.
Pia yeye ndiye anaamua, wote katuumba yeye, wengine anawapa magonjwa na wengine anawanyima kwa sababu anazozijua yeye.
 
Kama ulimbukeni unanisumbua, ni jambo jema.
Na kama sijapata matatizo makubwa ya duniani, ni jambo jema sana.
Na kama napotea pia ni jambo jema mno!

Nikipotea au nisipo potea, haupati faida yoyote.
Labda tu ili nipotee vizuri, itoshe kusema mungu hayupo. Na kama yupo, basi ni mshenzi.
! Ila mungu angekuwa athumani angetupiga risasi hovyohovyo! We kijana unadiriki kusema mungu ni mshenzi? Laana ya mungu iwe juu yako! Kijibwa Cha roho.
 
Pia yeye ndiye anaamua, wote katuumba yeye, wengine anawapa magonjwa na wengine anawanyima kwa sababu anazozijua yeye.

huu ujinga ndo tulikataa!.. wewe hautambui uwepo wake, ila unaamini, ambayo naweza sema ni speculation tu, ukiona maisha yanakuendea vizuri unadhani mungu anakuhariki yakikuendea vibaya utatafuta positivity reasons zitakazo ku allign na mtazamo wako!.

mwisho wa siku ni vilevile tu, mungu hayupo wala shetani hayupo, akiwepo basi atakua ni lunatic,mshenzi mpuuzi na mkatili!.

Tatizo ni kua watu wengi wako indoctrinated na fears!. siku moja start questioning everything to the details ndo utajua concept nzima ya mungu ni ujinga.

I dont think a god who is all mighty and pure can co exist with evil,
 
Hajui alichokiimba. Wanaomuabudu Mungu wa kweli wanapata na vya kuzidi maana NCHI NA VYOTE VIIJAZAVYO NI MALI YAKE. (Zab ya 24)

Ubaya wa wanaoonekana wana tabu na bado ni wakeshaji wazuri wengi ni wanafiki. Ambao MINGU anasema katika Ufunuo 3: 15-16 kuwa atawatapika

(Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto. Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu.)

Ukiwa vugu vugu huwezi barikiwa. Abudu Mungu kweli. Usiwe mchoyo kutoa zaka na kuwasaidia wahitaji, hapo utabarikiwa na mali itaonekana. Wanaokesha na kushinda na biblia usiku kucha na mchana kutwa bila kufanya kazi na kutumia biblia kama njia ya kufanya maovu ndo hao alowaimba.
 
Kiranga karibu huku unaitwa.
Huyo jamaa kwanza hata h9ja hajaielewa.

Mtu hajakana uwepo wa Mungu, anesema tu haoni umuhimu wake huyo Mungu katika maisha yake.

Sasa ukiona mtu ana tatizo kuelewa hoja nxogo tu hii, mjadala zaidi unaweza kuwa kujitafutia matatizo yasiyo na maana.

Unaweza kujipa kazi ya kumfundisha nyungunyungu hesqbu za String Theory hivihivi.
 
Konde Gang, msanii wa Bongo Flava ameuliza kwenye wimbo wake wa dunia, kuwa ni kwa nini watu wanaokesha kusali misikitini na makanisani wana hali mbaya kiuchumi, wana maisha mabovu, hawapati baraka ambazo Biblia na Quran imeahidi kwa waumini wake, kama ambavyo Wayahudi na Waarabu wa kale walivyopata?

Anauliza kuwa ni kwanini kila kitu kizuri kinaitwa ni cha shetani?!

Haya wanajamvi tumjibu!
maajenti wa shetani utawaona tu, wanatukuza ushetani hadi pale watakaposhushwa chini kuzimu kama alivyoshushwa bashite ndio huwa wanaelewa kuwa wapo vile walivyo kwa neema tu.
 
Ipo siku utamjua mungu ni nani
Bwana anawajua waliowake hivyo haina haja ya kutumia nguvu kubwa kupambana na mtu labda siyo wake, wengine wataokolewa kwa neema tu kulingana na matendo yao yakiwa mema, Sasa jibu kwa harmoniza ni kwamba siyo kushinda kwenye ibada ndo kunaleta hela na Mali Bali Mungu ameshatuelekeza tutakula kwa jasho hivyo tufanye kazi za kuleta hela na Mali bila uvivu na visingizio vya kushinda nyumba za ibada, au bar, au sehemu yoyote bila kufanya kazi ya kuingiza hela na Mali utabaki masikini maana Mungu amesema tufanye kazi na yeye atabariki kazi za mikono yetu hivyo tayari tunawajibu wa kufanya kazi halali zenye baraka za Mungu Ili tupate kubarikiwa.
 
Back
Top Bottom