Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 39,185
- 90,955
SAYANSI NI ZAIDI YA DINI; CORONA YAZIAIBISHA DINI ZOTE DUNIANI.
Na, Robert Heriel.
Tokea dunia kuumbwa Dini imekuwa msaada mkubwa sana katika kuituliza dunia iwe salama. Dini ni muhimu kama itatumika kulingana na sababu ya uwepo wake. Lengo kuu la dini kuwepo duniani ni Kufunza maadili, hilo tuu. Hakuna ziada katika dini isipokuwa suala la maadili.
Siku hizi watu hutumia dini tofauti na malengo ya uwepo wake. Watu wanadanganywa kuwa kupitia dini watu watajipatia utajiri, magari, fedha, na mambo mengine kama hayo.
Dini siku hizi imejiwekeza zaidi kwenye miujiza bandia, kamwe dini haiwezi kufufua mtu, dini haiwezi kumpa mtu utajiri, dini haiwezi kuponya magonjwa, dini haiwezi kuvumbua na kugundua teknolojia mpya. Dini haiwezi fanya hayo mambo.
Dini ni shule ya kufundishia maadili. Haina la ziada.
Dini inayojiwekeza zaidi kwenye miujiza ni dini za kitapeli, haina tofauti kubwa na watu wa mazingaombwe. Dini ya namna hiyo humnufaisha mmiliki wa dini hiyo yaani mfanyabiashara wa hiyo dini. Usishangae kwa nini kila siku wamiliki wa dini waliojipa jina manabii wakiwa matajiri wa kutupwa. Jibu ni kuwa, ni kwa sababu hiyo ni biashara ambayo msingi wake mkuu ni utapeli na hadithi za kitoto.
Dini hutegemea zaidi hadithi za kizamani, hutegemea zaidi vitu vilivyopita ambavyo kimsingi mtu mwenye akili hawezi kuvipa kipaombele.
Huwezi mwambia mtu mwenye akili kuwa zamani Nabii fulani aliponya mtu kipofu japo inaweza kuwa kweli au sio kweli, hivyo ukimuamini Mungu unaweza kuponya kipofu ilhali zama za leo vipofu wapo na watumishi wanaojiita wa Mungu wapo lakini hakuna uponyaji wa hao vipofu wa zama za leo.
Ni mjinga pekeake anayeweza kukubali kusikiliza hadithi za kitoto akazikubali.
Dini ni nzuri kama itafundisha maadili, lakini dini ni mbaya kama itatapeli watu na hadithi za kizamani zisizo na uhalisia katika zama hizi. Hadithi zinazosimuliwa na watu wasiokuwa mashuhuda wa matukio hayo lakini wanavyosimulia ni kana kwamba walikuwepo. Huo ndio upuuzi wenyewe.
Huwezi danganya watu kuwa UKIMWI ukiombewa unapona, jambo ambalo kamwe haliwezi kuwezekana. Kikawaida maombi hayawezi zuia vitu natural, maombi hayawezi zuia njaa, usingizi, kifo, magonjwa, huzuni, furaha, majanga ya asili miongoni mwa mambo mengine ya asili.
Katika Dini kuna kipengele kinaitwa Imani. Imani ni sehemu ya maadili. Imani huhusu zaidi mambo yasiyobayana, yasiyodhahiri, mambo yanayotarajiwa. Sana zaidi huhusu mambo ya kiroho.
Huwezi tumia imani kwenye ishu za kimwili, imani inahusu mambo ya kiroho. Halikadhalika huwezi tumia mambo ya kimwili kwenye mambo ya imani. Hii ni kusema kila jambo linamipaka yake. Imani haiwezi ingilia mambo ya kimwili(Akili) na Akili haiwezi ingilia mambo ya kiimani.
Maombi huweza kutumika zaidi kwenye ishu zinazohusu madhara ya falme za rohoni, mfano magonjwa ya kimwili yatokanayo na ulozi, ushetani, ujini. Magonjwa haya huweza kuwa na dalili za magonjw ya asili lakini ukienda maabara hayaonekani. Mfano mtu huweza kuumwa UKIMWI wa kichawi lakini akienda hospitalini hataonekana kama anaukimwi lakini kinachofanya watu waseme anaUkimwi ni dalili zote alizonazo mgonjwa ni za Ukimwi wa kawaida.
Magonjwa haya yasiyo ya kimwili ndio yanapaswa kuombewa kanisani, misikitini, na kwenye nyumba za ibada. Na hapo ni baada ya Mgonjwa kwenda hospitalini na kuonekana hana Ukimwi, kisukari, Saratani, n.k lakini mtu huyo anaumwa kikamilifu.
Siyo umeenda maabara kupimwa alafu ukaonekana unaukimwi au ugonjwa wowote ule alafu uende kuombewa kanisani. Utakufa asubuhi kabisa.
Kumbuka Magonjwa na matatizo mengi ya mwanadamu yanatibika kibinadamu ambapo hapo sayansi ndio inahusika.
Watu masikini wengi tunashindwa kwa sababu tunaamini maombi zaidi kuliko nguvu zetu, huo ni upuuzi. Hata mnyama hawezi kufikiri hivyo. Maombi 10% kazi 90%.
Sayansi ni maarifa yanayopatikana kwa kufanya vitendo, kutazama na kujaribu kweli zilizo bainishwa pasi kuthibitishwa. Msingi wa sayansi ni vitendo. Vitendo vya Kisayansi vina njia zake zinazotumikia kusimamisha kweli ya kisayansi.
Mungu hakukupa akili ati umuombe yeye pakeake, hakukupa mdomo na mikono ati akulishe chakula, hakukupa miguu alafu uje umuombe akubebe, hakukupa macho alafu uombe akuangalizie. Mungu amekupa maisha ufanye kwa vitendo.
Ujio wa Corona umefanya dini ziwe duni mbele ya Sayansi. Uduni wake unatokana na ulaghai wa watumishi matapeli wanaodanganya watu sijui Mungu anaweza kuondoa Corona, sijui Corona haitafika nchini, yaani upuuzi upuuzi tuu.
Sasa baada ya Corona kutawala tumeona watumishi wakihaha bila kutafuta suluhu, bila kutafuta chanjo wala dawa. Wao wamekaa tuu wanatunga uongo mwingine wa kudanganya dunia.
Watakuambia dunia imefika mwisho utadhani waliuona mwanzo wa dunia. Wewe hujui mwanzo wa dunia ilikuwa lini iweje ujue mwisho wake. Huo ndio uhuni wa hawa watumishi matapeli.
Badala ya kujikita kwenye fani yao ya kufunza maadili, kwamba watu wawe waadilifu, wasiibe, wasizini, wasiue, wasidhulumu, matokeo yake yao ndio yamekuwa matapeli yanadhulumu akili za waumini wao.
Corona ni sehemu ya mambo yanayowashtua watu kuwa maisha ya mwanadamu yapo chini ya mwanadamu. Matatizo ya mwanadamu atakayeyatatua ni mwanadamu mwenyewe. Hakuna mtu au kiumbe atakayekuja duniani kumuokoa na matatizo yake.
Dini kufundisha kuwa Mungu atakusaidia hivyo umuombe zaidi na zaidi ni fundisho bandia na lakipuuzi. Mungu alishakupa uhai na Afya hiyo ilitosha kabisa, hayo mengine unajiendekeza na kujidekeza.
Sayansi ni zaidi ya dini kutokana na kuwa Sayansi inajikita zaidi kwa mambo ya sasa na baadae, sayansi inajikita kwenye vitendo na mambo yanayoonekana na yanayosaidia watu wote . Lakini dini inajikita katika mambo yaliyopita ambayo yalisaidia watu waliopita bila ushahidi wa kivitendi bali simulizi. Dini haisaidii watu wote zaidi ya hadithi za mtu mmoja mmoja ambao wengi wao tunasimuliwa tuu kwenye majukwaa ya mihadhara. Utasikia Mchungaji au Sheikh anasema; Kule kwetu kijana mmoja, au Mji ambao watu anaowasimulia hawajawahi kufika, utasikia ukifika Marekani mtu fulani aliwahi kutukana akapata madhara, au kufunga akapata hivi. Yaani stori nyingi za kidini ni simulizi za kitapeli tapeli.
Hazina tofauti na stori za Biashara za mtandao za kina Aim Global, unahadithiwa simulizi ya mtu usiyemjua.
Hii ni tofauti na Sayansi. Sayansi haihitaji stori, fanya uone, gusa unate, cheza uchezeshwe, Fanya upate, mfano unaambiwa ukigusa waya wa umeme unapigwa shoti na unaweza kupoteza maisha. Kweli ukijaribu unapigwa shoti na unaweza kufa kabisa.
Lakini watu wa dini wanasema ukiichana sijui QURAN au Biblia unaweza kuchanganyikiwa. Lakini wapo wanaochana, wanaokojolea, wanaoifanyia vyovyote watakavyo na hawapati madhara zaidi ya kuambiwa sijui mji fulani mtu mmoja alichana quran sijui biblia akachanganyikiwa lakini mtu huyo hatumjui mpaka hivi leo.
Hata yule aliyechana Quran hivi majuzi akiwa kalewa hakuna alichotokewa nacho zaidi ya serikali kumchukulia hatua za kinidhamu.
Dini watu wake wamejaa uongo uongo mwingi na propaganda nyingi za kitoto ambazo hazina msingi wowote. Hii yote ni kutaka kuwapa watu hofu na viongozi kutaka heshima kubwa isiyowastahili.
Hii ni tofuati na wanasayansi, wao hawanaga Blah blah! Wanakuambia kabisa, ukigusa kemikali hii ndani ya dakika tano utadhurika, na kweli utadhurika.
Watu wote duniani wanawaheshimu wanasayansi bila ya kulazimishwa, lakini viongozi wa dini huheshimiwa kwa kutunga simulizi za kubuni na kutishia watu. Sijui usimseme mchungaji hata kama kakosea, usichane Quran, au Biblia utachanganyikiwa, wakati yote yanafanyika na hakuna linalotokea.
Kwa nini nimeandika haya?
Nimeandika haya ili kuwashtua watu wanaotumikishwa kwenye dini. Wakiacha kujihangaisha na kujilinda ati wakitegemea maombi na kukesha makanisani.
Nakuhakikishia, Dini haikuondolei umasikini, magonjwa asilia, njaa nyumbani kwako, na matatizo mengine. Dini itakufanya uwe mtu mwema, mwenye maadili, basi. Lakini mtu mwema sio kigezo cha kuwa tajiri, kutokuwa na njaa, magonjwa n.k
Mwisho: Dini tuendelee kuziheshimu ikiwa zinamchango kwenye maisha yetu. Tuheshimu watu wote lakini sio wanaolazimisha kuheshimiwa. Mtu yeyote anayelazimisha heshima hastahili heshima.