Harmonize ameuliza, tumjibu!

Harmonize ameuliza, tumjibu!

Subhanaalah! Hivi binaadam tuna nini lakini? Mkuu umepatwa na maswahibu gani hata ukane uwepo wa Mungu?
Hivi mbona huwa mnashangaa mtu asiyeamini kitu kisichothibitishika na hakionekani...badala ya kuwashangaa wanaoamini mambo kama samaki mtu,mizimu,majini,malaika, mungu ambavyo havionekani,havina ushahidi na havithibitishiki?
Mimi naona wasioamini mungu ndo wanatakiwa kuwashangaa na kuwauliza wanaoamini.
 
Mungu Kama yupo au kama hayupo, mimi hainihusu!

Huyu Mungu hanisaidii kwa chochote, wala hanisaidii kwa lolote!
Maisha yangu hayahitaji wala hayategemei Mungu.
Dogo najua tu ulimbukeni bado unakusumbua, mtapotea kwa kufuata mkumbo wa Kiranga.

Ukiwa unakula, unashiba, unakwenda chooni na hupati shida kubwa kubwa, ni rahisi sana kusema Mungu hayupo. Ila siku ukikutana na mitihani ya dunia ndio utakapojua Mungu yupo

Omba Mungu akuepushe na mitihani ya dunia kijana.
 
Dogo najua tu ulimbukeni bado unakusumbua, mtapotea kwa kufuata mkumbo wa Kiranga.

Ukiwa unakula, unashiba, unakwenda chooni na hupati shida kubwa kubwa, ni rahisi sana kusema Mungu hayupo. Ila siku ukikutana na mitihani ya dunia ndio utakapojua Mungu yupo

Omba Mungu akuepushe na mitihani. ya dunia kijana.



Sent from my TECNO RC6 using JamiiForums mobile app
Kala maharage kashiba huyo
 
Hili ni jambo la kiimani zaidi, hivyo kila mtu na aminicho..

Kwangu iko hivi, kwa mungu kuna neema tofauti, yaani neema za dunia(naita neema ndogo ndogo) mfano kupata mali, kupumua, uzima wa afya, watoto n.k n.k, kuna neema kubwa hii ndio kuingia peponi, hii ndio neema kubwa kabisa.

Mungu kila kitu katuumbia ni mtihani, mali watoto, na mazaga zaga yoote ni mtihani,hata ufukara ni mtihani pia,mpaka tamaa za kimwili ni mtihani, vyoote hivyo katupa halafu katuwekea namna ya kuviendea, mathalani, kukwichi kwichi, ametuamuru tuoe na tusizini, tukizii tumefeli, mali katupa katuelekeza jinsi ya kuzitumia(mf. Kusaidia yatima, maskini,wajane, wapita njia n.k)

Kama kila jambo ni mtihani, basi kwenye kila mtihani kuna kufaulu na kufeli, je nikifeli inakuwaje na nikifaulu inakuwaje, ndio hapo kaumba moto na pepo wanaofeli wataingia motoni na wanaofaulu pepono ambayo hii ndio neema kubwa kabisa kuliko neema zoote.

Anaepewa mali na kunyimwa mali wote ni wapo katika mawili afaulu(ashukuru) ama afeli(akufuru).
Tajiri anaetumia mali zake kiuadilifu vile mungu inampendeza huyo kafaulu, vingimevyo kafeli akifeli motoni akifauulu nfio anapata neema kubwa kabisa ya pepo, hivyo hivyo maskini, akiridhika na umaskini wake akaona mungu ndio mpaji akitaka kumpa atampa, na akaacha kukufuru kuwa mungu anamuonea, akatenda mambo mola anayapenda(akafaulu) nasi nae atapata meema kubwa kabisa ya pepo

Mungu sijaona sehemu kasema niabuduni niwape mali, ila kasema nitaweneemesha na neema za mungu ni kama nilizoorodhesha na anatoa kadri apendavyo, kuwa mzima wa afya tu ni neema kubwa mnooo, kuna wachamungu wanapewa mali, kuna wachamungu masikini, kuna mabaradhuli wanapewa mali na kuna mabaradhuli maskini... Shida ni sisi wanadamu kuona neema ni mali tu, la hasha hilo si kweli.. neema ni nyingi.

Malipo ya mungu ni makubwa mnoo, watu hatuelewi kuna vitu vinatusumbua, mfano umenikuta njiani naumwa, ukanichukua ukanipelela hospitali, unauwezo wa kunighamikia, ukafanya hivyo, siku ya siku tukakosana nikakutukana, we fala tu, huna lolote kimeemda kimerudi!? Je malipo yako kwa mungu hayapo!? Au kwa wema ulionitendea nami nikakutendea wema je, mungu hakulipi tena, la hasha malipo ya mungu costant, mtu atalipwa kwa kile alichotenda, umenitendea wema nimekufanyia ubaya, wema wako utalipwa,umenitendea wema nikakutendea wema, bado wema wako utalipwa tu.
Ndio ufukara na utajiri.. uwe maskini uwe tajiri, kizuri ni kufayanya mema tu. Kila mtu ataulizwa neema aliyopewa aliitumia vipi!? Kimbembe kitakuwepo hapo kudadeki.

Ni jambo refu kidogo, niishie hapa.
 
Dini na imani ni chakula cha roho na kinga dhidi ya 'negative energy'

Kupata pesa na utajiri ni jitihada za akili na nguvu.

Wala usijaribu kukebei dini na imani kwa kisingizio cha pesa na utajiri..

Daima usifanye hilo kosa la kudharau dini na imani. Huo utajiri na mafanikio utapuputika.
Si kweli mkuu, fanya tafiti upya.

Kupata pesa na utajiri kamwe si jitihada za akili na nguvu.

Ushawahi kuwaona ambao hawakuw na akili vizuri na walikuwa dhaifu ki nguvu lakini ni matajiri wakubwa tu. Na wengine walikuw na akili na mungu aliwajaalia nguvu lakini waliishia kwenye umaskini??

Think again bro
 
Dogo najua tu ulimbukeni bado unakusumbua, mtapotea kwa kufuata mkumbo wa Kiranga.

Ukiwa unakula, unashiba, unakwenda chooni na hupati shida kubwa kubwa, ni rahisi sana kusema Mungu hayupo. Ila siku ukikutana na mitihani ya dunia ndio utakapojua Mungu yupo

Omba Mungu akuepushe na mitihani ya dunia kijana.
JamiiForums mobile app
Kama ulimbukeni unanisumbua, ni jambo jema.
Na kama sijapata matatizo makubwa ya duniani, ni jambo jema sana.
Na kama napotea pia ni jambo jema mno!

Nikipotea au nisipo potea, haupati faida yoyote.
Labda tu ili nipotee vizuri, itoshe kusema mungu hayupo. Na kama yupo, basi ni mshenzi.
 
Sasa unasema Mungu hayupo pumzi unayovuta unaitoa wapi, na si ajabu hiyo pumzi akaichukua mda huu, watu wakikusanyika huku wakisema marehemu tulikuwa naye jana tu leo hatunaye,

hiyo pumzi siku akihihitaji ndo utajua kuwa yupo, siku akimtuma malaika mtoa roho ukiwa umetazamana nae face 2 face kwa mara ya Kwanza akiichomoa roho yako na kusepa nayo akiipeleka kwa Muumba.
 
Back
Top Bottom