Harmonize kaingia kusiko!

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
JE ALICHOKIFANYA HARMONIZE NI SAHIHI?

Msanii Harmonize Kupitia Kionjo cha Wimbo wake Mpya Dunia Ameimba kuwa Anaamini Mungu yupo na Anajua hata akitaka kumchukua Sasa Hivi anamchukua Lakini Anataka Kujua Kwanini Mungu aliweka kila Vitu Vizuri Viwe Ni vya Kishetani .

Kondeboy Ametolea Mfano kuwa Muziki ni Shetani, Pesa shetani, Mademu Shetani ,Mapenzi Shetani, Mpira na Pombe, Mihadarati Shetani Kwanini..?


HISTORIA YA HARMONIZE:
Kuna wengi wanamfahamu msanii huyu Ila hawajui vizuri historia ya Harmonize. Kwa majina kamili Anajulikana kama Rajabu Abdul kahali. Ni msanii kutokea nchi ya Tanzania na anafanya mziki wa aina ya bongo flava. Wengi wanamfahamu kama Harmonize, Konde Gang jina lake la kisanii. Majina mengine ya kimatani kama Konde Boy nk

Jina lake la Rajabu hupewa watoto wavulana waliozaliwa mwezi wa saba Kulingana na calendar ya kiisilamu japo kiukweli Harmonize hakuzaliwa huo mwezi.

Abdul humanisha mtumwa kwa kiarabu na pia inamanisha dhoruba Kali. Kwa kweli Harmonize ni dhoruba Kali nchini Tanzania kimziki kwani mziki wake upo juu sana. Katika historia ya Harmonize nadhani pia umejifunza maana ya majina yake.

Kabla ya mkataba wake na Diamond Platnumz mmiliki wa wasafi media WCB, Harmonize alikuwa mtoto wa mtaani aliyekuwa amechoka na kuishi.

Kujulikana kwake ni wakati alipochukuliwa na Diamond Platnumz kwenye record label yake. Alirekodi nyimbo nyingi kwenye label ya Wasafi hadi baadae alipotoka wasafi na kufungua label yake mpya kwa jina Konde Music Worldwide. Kwenye label yake ndipo amerekodi album yake ya kwanza kwa jina “Afro East”

Wakati akiwa label ya wasafi, Harmonize aliachia Ep ( extended play ) kwa jina ” Afro Bongo” iliyohushisha wasanii wengi wakiwemo wasanii kutoka nchi mbalimbali barani Afrika.

Kwa sasa inasemekana anafanya project mpya Ila bado haijajulikana ni project aina gani.

Tuzo za Harmonize:

YearNominee / workAwardResult
2016Bado ft. Diamond PlatnumzWatsAp TV Africa Music Video Awards for Best African Newcomer VideoWon 18
HimselfAfrican Muzik Magazine Awards (AFRIMMA) for Best NewcomerWon 19
African Entertainment Awards (AEAUSA) for Best New ArtistWon 20

Utajiri wa Harmonize​

Tunapoongelea kuhusu historia ya Harmonize basi lazima tutagusia label ya WCB. Harmonize alianza kuingiza hela ndefu wakati alijiunga na Wasafi. Baada ya kutoka Wasafi record, Harmonize alisemekana kupoteza hela nyingi sana kwani alihitajika kulipa kabla ya kuondoka label hiyo kwa kuvunja mkataba.

Hata baada ya kulipa hela nyingi, Harmonize bado yupo vizuri kihela kwani label ya Konde Music Worldwide inamuingizia mamilioni. Bado kabisa haijajulikana pesa anazopata kwa sasa Ila ni pesa nyingi na huenda ikawa baada ya Diamond Platnumz, Harmonize atakuwa msanii wa pili mwenye pesa nyingi.

Umri wa Harmonize​

Harmonize alizaliwa March 15, 1990

Watoto wa Harmonize​

Kama mwaka mmoja uliyopita, Harmonize alitangaza kuwa atakuwa na mtoto na Sarah Michelloti. Baadae ilisemekana kwamba mimba ilitoka. Kuna wakati alionekana na mtoto kwenye mitandao aliyedai ni mtoto wake Ila bado haijafahamika kama ni kweli.

Mpenzi wa Harmonize​

Harmonize alikuwa na mpenzi kutoka Italy kwa jina Sarah Michelloti. Wawili hawa wamekuwa pamoja Ila inasemekana kwa sasa wameachana. Ni hivi majuzi alianza uhusiano na Kajala Ila pia wakaachana kwa kile kilichosemekana kwamba alikuwa pia na uhusiano wa kimapenzi na mtoto wa Kajala anayejulikana kama Paula Kajala.

Nyumba ya Harmonize na magari​

Mziki wake unalipa vizuri na hii imemuezesha Harmonize kumiliki magari makubwa na nyumba ya kifahari. Kuna muda kupitia Instagram page yake ali post nyumba yake ya kifahari iliyoko Katikati ya jiji la Dar es salaam.

Harmonize kwenye label yake ana mkataba na wasanii kama vile Country Boy, Ibraah na Angela. Wasanii hawa wanafanya vizuri kimziki kwani wamepokelewa vizuri nchini Tanzania na nchi jirani. Ni hayo tu kwa leo kuhusiana na historia ya Harmonize.

images - 2021-10-29T204917.834.jpeg
 
Harmonize kaongea ukweli mchungu Sana, Kwa haraka haraka huwez kumwelewa duniani ukishaanza kuwa maarufu Tu, wazee wa kazi wanakufata, ukitaka kumantain status inabd ukubaliane nao.

Jamaa anauliza why kama Mungu yupo na anaruhusu hawa jamaa kuwa na nguvu Kiasi hicho, ni kilio kikubwa Bahati mbaya ukiingia sio rahisi kuchomoka ....!!! Kondeboy mtu mbadi yupo under hot supu.
 
Harmonize kaongea ukweli mchungu Sana , Kwa haraka haraka huwez kumwelewa duniani ukishaanza kuwa maarufu Tu , wazee wa kazi wanakufata , ukitaka kumantain status inabd ukubaliane nao, jamaa anauliza why kama Mungu yupo na anaruhusu hawa jamaa kuwa na nguvu Kias hcho , ni kilio kikubwa Bahati mbaya ukiingia sio rahs kuchomoka ....!!! Kondeboy mtu mbadi yupo under hot supu
I second you vitu vyote vizuri ni vya shetani why?

Harmonize ila huwaga akitulia anaachia vitu vya akili nyie ile ngoma yake ya atarudi dah
 
Kwa industry ya sasa, Ni lazima Bro.. Hata kama hupendi
Labda uwe na nyota ya Michael Jackson
Content zao zikiwa vyema zitajiuza zenyewe, haihitaji muhusika ajitoboe sikio na kuvaa hereni au kusuka ndipo content iuzike.

Kama ulivyomsema Michael Jackson, si unaona content zake zilimpaisha Ulimwenguni!!
 
Content zao zikiwa vyema zitajiuza zenyewe, haihitaji muhusika ajitoboe sikio na kuvaa hereni au kusuka ndipo content iuzike.

Kama ulivyomsema Michael Jackson, si unaona content zake zilimpaisha Ulimwenguni!!
Ndio maana nikamtolea mfano

Mi naamini kadri teknolojia inavyokua, ndivyo vipaji halisi vinavyopotea. Miaka ya 60 mpaka mwishoni mwa 2000 kulikua na 100% Pure talent

Lakini now hakuna talent hizo, kwa sababu 60% ya ubunifu inafanywa na teknolojia. Mimi hata kama nina sauti mbaya, with auto tune naweza sound kama R kelly

So ku ziba hilo gape la Pure talent
Lazima tuweke madem wenye makalio kwenye video

Tuonekane tunatoa moshi mdomoni, mitindo na mavazi ya kisasa
Tujifanye ma gangsters

Na bila kusahau matusi.....bila hivyo ni ngumu
 
Hivi ukiwa msanii ni lazima usuke, uchore tattoo, uvae hereni?
Wasanii wanadai ni vizuri wao kuongeza mapambo na nakshi ili waonekane tofauti na watu wengine
Content zao zikiwa vyema zitajiuza zenyewe, haihitaji muhusika ajitoboe sikio na kuvaa hereni au kusuka ndipo content iuzike.

Kama ulivyomsema Michael Jackson, si unaona content zake zilimpaisha Ulimwenguni!!
Michael Jackson alikua mwanamziki genius,ni mwanamziki aliyekua anafanya kazi kwa mahaba makubwa sana,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom