Harmonize ameuliza, tumjibu!

Harmonize ameuliza, tumjibu!

Mkulungwa01

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
3,977
Reaction score
5,351
Konde Gang, msanii wa Bongo Flava ameuliza kwenye wimbo wake wa dunia, kuwa ni kwa nini watu wanaokesha kusali misikitini na makanisani wana hali mbaya kiuchumi, wana maisha mabovu, hawapati baraka ambazo Biblia na Quran imeahidi kwa waumini wake, kama ambavyo Wayahudi na Waarabu wa kale walivyopata?

Anauliza kuwa ni kwanini kila kitu kizuri kinaitwa ni cha shetani?!

Haya wanajamvi tumjibu!
 
Dini na imani ni chakula cha roho na kinga dhidi ya 'negative energy'

Kupata pesa na utajiri ni jitihada za akili na nguvu.

Wala usijaribu kukebei dini na imani kwa kisingizio cha pesa na utajiri..

Daima usifanye hilo kosa la kudharau dini na imani. Huo utajiri na mafanikio utapuputika.
 
Konde Gang, msanii wa Bongo Flava ameuliza kwenye wimbo wake wa dunia, kuwa ni kwa nini watu wanaokesha kusali misikitini na makanisani wana hali mbaya kiuchumi, wana maisha mabovu, hawapati baraka ambazo Biblia na Quran imeahidi kwa waumini wake, kama ambavyo Wayahudi na Waarabu wa kale walivyopata?

Anauliza kuwa ni kwa nini kila kitu kizuri kinaitwa ni cha shetani?!

Haya wanajamvi tumjibu!
Kizuri au kibaya??
 
Kesha unafanya kazi,
siyo ukeshe unaomba Mungu, ambaye kiuhalisia hayupo.
Mara mia ukeshe usiku kucha unamuomba mwanadamu mwenzako, atakupa msaada.
Inaitaji ujasili
 
Wameaminishwa kua ukiwa upande wa yesu unakua na thamani kuliko elon max mwenye billions of dollars.

Hiyo imewajengea spirit ya utegevu na kujiona wao ndio bora kuliko wengine, huku wakijikuta wana invest muda wao mwingi kwenye majumba ya ibada na kupuuza shughuli za utafutaji pesa

Kuna mwamba mtaani aligoma kumpeleka mtoto wake shule, mtoto alipofika darasa latatu akamtorosha akampeleka madrasa

Na mchizi anajigamba kua ilmu akhera ndio tunu na kwa kitendo hicha cha kumtorosha mtoto wake tayari kapata thawabu

Source ya haya yote ni UJINGA
 
Back
Top Bottom