AKILI ZAKO NA ZA LOWASA NI HIZI HAPAA....
Wapo watanzania wenzetu wanaujua ukweli kuwa tuko zaidi ya watanzania mil.45 miongoni mwao wapo watu hawajawahi kulitia hasara taifa hata senti na ni wachapakazi lakini bado unakuta anatumia social media kumpigia debe Lowasa!
Pengine wanatumia kauli zake akiwa ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)ya ccm nanukuu "Mh. Mwenyekiti nilikuuliza mara nyingi kuhusu ufanisi wa hiyo kampuni lakini uliniambia unawafahamu na mchakato uendelee, inakuwaje unamwachia Nape azunguke nchi nzima kwa hela za Chama kunichafua" ,Uliponitaka ushauri wa mtu wa kutusaidia ili kuondokana na aibu ya Richmond kushindwa kutimiza mkataba wake, nilipokutajia jina la Rostam, haraka ulikubali na kusema, naona hilo ni sawa, Richmond Development Company (RDC), ilivyopewa zabuni ya kufua umeme wa dharura nchini ni kwa nukuu ya kwanza na Dowans nukuu ya pili.
Sasa kwa kauli hizo tu Lowasa munamuondoaje kwenye hizo kashifa na kuona anafaa kuliongoza taifa kama hata ushauri wake kwa raisi ulikuwa ni wa ovyo hata kama raisi aliupokea kwa mikono miwili! Nawataka munaompigia debe tazameni masilahi ya taifa kwa mapana mwingine ameenda shule lakini kakaza buti Lowasa Lowasa fikirieni sana!