NI FARAJA ILIOJE PALE HATA MMACHINGA, MKULIMA, MFUGAJI NA MFANYAKAZI WA KITANZANIA PINDI ANAPOJIHISI KUWA NI MWANAHISA MUHIMU KATIKA CHAMA SAWA TU NA WENGINE????
Jamani ni jambo la kheri ilioje kwa akina kabwela kama vile Wamachinga wa Dar, Mbeya, Arusha na Mwanza kuchangia chama chao CHADEMA hata kama ni sumni tu na wakaondoka mahali pale wakiwa wamejiridhisha moyoni kwamba hapa na yeye pamoja na kipato chake duni pia ni MWANAHISA wa kutegemewa na chama chake!!!
Naam, nasema ya kwamba ni furaha ilioje kwa mfugaji tu hata kuku pindi anapochangia japo ka-kuku wake tena kwa hiari bila kuletewa Balozi wa Nyumba 10, ili na yeye apate kujihesabu kuwa ni sehemu muhimu kati ya MATOFALI YA TAIFA yatakayotumika kujenga misingi imara iliopotea kule CCM ya kulinda HESHIMA NA UTU WA KILA MTANZANIA bila kuzingatia mitabaka katika jamii.
Ndio, nauliza hivi kwamba kama hata nchi tajiri duniani kama Marekani unakuta mgombea wa chama kama vile Obama kwa Democrats anachangiwa hadi dola moja moja na vijana vijiweni tu hadharani, tangu lini CHADEMA kikawa kimegeuka kuwa chama cha matajiri wachache kuchangiwa ma-bilioni na akina Chenge, Lowassa na Rostam Aziz kifichoni??
Ni kweli kabisa kwamba nahoji hapa kwamba inakua vipi mtu kukejeli Tshs 26/- milioni zilizochangiwa na wlalahoi kwa hiari na mapenzi yao wenyewe kwa CHADEMA eti mtu akiona kwamba ni kiasi kidogo mno wakati sote tunajua kwamba siri ya bei ya mafuta ya taa kupaa angani, petroli, dizeli na bidhaa nyingine kibao nchini ni shauri ya CCM kuingiza kitenesi chao mle, bila huruma kwa walalahoi, hivyo kufanya maisha kuwa magumu kupindukia ilmradi wao wawe wanaingiza ma-bilioni ya fedha za kununulia kura hata kama wananchi tunakufa?
Hakika mtu au watu walioiunda hii propaganda dhidi ya CHADEMA nawashauri muende mkamuombe kwanza ushauri Mh Tambwe Hizza ili siku nyingine msije mkajitokeza hadharani na upuuzi kama huu, kukidhalilisha chama chenu, na hata nyinyi wenyewe kupitia huko huko Clouds FM mkaonekana hamnazo!!!
Kila mwana-CHADEMA popote pale ulipo, jitokezeni twende tukamuumbue SHETANI YA UFISADI kule CCM kwa kwenda kukichangia chama chetu wenyewe CHADEMA ili kusaidia kuharakisha juhudi za ukombozi nchini.
Hakika ni jukumu letu sote kujipa wenye RAHA ya kuondokana na ukandamizaji na UFISADI wa CCM-Mamboleo, leo leo na wala tusingoje kesho!