Mnamo Julai 2013, afisa mmoja wa ujasusi akiwa na kifaa kama master key cha kufungua milango na bastola yenye kiwambo cha kupunguza sauti alivamia nyumba ya Sergio Massa, mwanasiasa wa Argentina aliyekuwa akijiandaa kuwania urais.👇
Alijulikana kwa jina la Alcides Díaz Gorgonio alikuwa amehudumu katika Kikosi cha Ulinzi wa Pwani cha Argentina tangu mwaka 1985. Wakati wa tukio hilo, alikuwa akifanya kazi katika Kituo cha Mipango na Udhibiti cha Wizara ya Usalama wa Taifa, kilichojulikana kama
situation room. Na Aliripoti moja kwa moja kwa Katibu wa Usalama, aliyekuwa mshirika wa karibu wa Rais Cristina Kirchner.
Wakati huo, Massa alikuwa Waziri wa Uchumi, Mkuu wa Baraza la Mawaziri na meya wa mji wa Tigre, eneo lililopo pembezoni mwa jiji la Buenos Aires alikoishi.
Hata hivyo, wiki chache kabla ya uvamizi huo, alikuwa amejitenga na chama cha kisiasa cha Rais Kirchner na kuunda chama chake kipya kilichoitwa Renewal Front, akishirikiana na takribani mameya wengine 20. Lengo lao lilikuwa kuwania urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Usiku wa Julai 20, 2013, Díaz aliingia katika eneo lenye ulinzi mkali ambako Massa aliishi. Alikaa karibu na lango kuu kwa takribani saa mbili, akizungumza na walinzi huku akisubiri mke wa Massa aondoke nyumbani.
Baada ya nyumba kuwa tupu, Díaz aliingia ndani ya eneo la makazi hayo. Alifyatua risasi moja kutoka kwenye bastola ya Bersa ya milimita 5.6 (.22 LR), iliyokuwa na kifaa cha kupunguza sauti, akilenga kamera ya usalama iliyokuwa nje. Hata hivyo, alishindwa kuiharibu kamera hiyo na kufuta ushahidi wa uvamizi wake.
Kisha alivunja njia ya kuingia ndani ya nyumba na kuiba sefu ya chuma. Ndani yake kulikuwa na vifaa vya USB vilivyohifadhi taarifa kuhusu kipindi ambacho Massa alihudumu katika nyadhifa za umma, vito vya thamani na pesa taslimu 65,000 za Argentina.
Lakini hakufanikiwa kutoroka bila kuacha ushahidi.
Saa 15 tu baada ya tukio hilo, Díaz alikamatwa. Polisi walichunguza kamera za usalama zilizokuwa Tigre na kugundua picha zilizorekodi kuwasili na kuondoka kwake eneo la tukio.
Katika nyumba yake, polisi walipata vifaa vya USB vilivyoibwa kutoka kwa Massa pamoja na bastola iliyolingana na ganda la risasi lililoachwa eneo la tukio.
Ingawa alishtakiwa kwa wizi wa kutumia nguvu, mahakama ilitambua kuwa tukio hilo lilikuwa na sura ya vitisho vya kisiasa dhidi ya Massa na mkewe, Marisa Galmarini, ambaye pia alikuwa mwanasiasa na kiongozi aliyechaguliwa katika eneo la Tigre.
Mnamo Machi 2015, Alcides Díaz Gorgonio alihukumiwa kifungo cha miaka 18 jela kwa kosa la wizi huo. Hata hivyo, baada ya kukata rufaa, adhabu yake ilipunguzwa hadi miaka 11.