Mnamo Agosti 1945, ujumbe wa siri uliotumwa kwa njia ya mawasiliano ya Siri(encrypted message ) uliwafedhehesha sana ma undercover wa Australia. Ujumbe huo ulifichua kwamba, wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, shughuli zao za siri katika kisiwa cha Timor zilikuwa zimejulikana kwa majeshi ya Japan.
Jeshi la Japan lilipovamia visiwa vya Timor mnamo Februari 1942, kisiwa hicho kilikuwa bado kimegawanywa katika makoloni mawili: koloni la Ureno na la Uholanzi. Kikosi kidogo cha majeshi ya Washirika (Allied forces)kilichokuwa kisiwani humo kilipambana kishujaa, lakini muda mfupi baadaye kilizidiwa nguvu na wanajeshi wa Japan.
Sasa Mnamo Julai 1942, Idara ya Australia ya Upelelezi wa Kijeshi (
Services Reconnaissance Department — SRD) ilianza kutuma vikosi vya siri huko kwenye visiwa Timor kusaidia upinzani dhidi ya Wajapani.
Hata hivyo, SRD ilikuwa shirika jipya ambalo halikuwa na uzoefu wala mafunzo ya kutosha kukabiliana na polisi wa kijeshi wa Japan, walioitwa
Kempeitai.
Karibu wanajeshi wote wa Washirika waliotumwa katika visiwa hivyo walifuatiliwa na Kempeitai muda mfupi baada ya kuwasili. Baadhi yao waliuawa, wengine wakafungwa, na wengine wakalazimishwa kushirikiana na Wajapani.
Wakazi wa Timor waliacha kwa kiasi kikubwa kupambana na Wajapani baada ya chifu mmoja wa eneo hilo, Dom Alexio Corte-Real, kuuawa pamoja na familia yake yote mnamo Mei 1943.
Hadi vita vilipomalizika, Waaustralia hawakufanikiwa kujenga kituo imara cha shughuli zao za siri kisiwani humo.
Mnamo Septemba 1943, mwendeshaji wa redio wa kikosi maalumu cha Australia kilichoitwa
Z Special Unit, AJ Ellwood, alikamatwa baada ya timu yake, iliyokuwa na jina la siri
LAGARTO, kunaswa na Wajapani.
Wajapani walipata vitabu vya jumbe za siri ambavyo Ellwood alikuwa amevizika wakati wa kukimbia kwao. Kisha wakamtesa hadi akasalimu amri na kuanza kutuma ujumbe kwa makao makuu ya SRD kwa maelekezo ya Wajapani.
Kuanzia wakati huo, Kempeitai ilikuwa imepenya kabisa katika mtandao wa mawasiliano ya siri wa Australia.
SRD haikugundua kwamba mwendeshaji wake wa redio alikuwa amegeuzwa na kuwa chanzo cha taarifa kwa adui. Badala yake, iliendelea kuamini ujumbe wake bila kuutilia shaka.
Matokeo yake, timu nne zilizotumwa Timor baada ya hapo ziliuawa au kukamatwa karibu mara tu zilipowasili. Hata hivyo, majanga hayo hayakuhusishwa na ukweli kwamba Ellwood alikuwa amegeuzwa na kutumiwa kama chambo na Wajapani tangu awali.
Mnamo Agosti 12, 1945, Japan ilikuwa inakabiliwa na kushindwa katika karibu kila upande wa vita. Katika kipindi hicho, ujumbe wa mwisho ulitumwa kwa Waaustralia kwa lengo la kuwadhihaki kutokana na juhudi zao za siri zilizokuwa zimeshindwa.
Wajapani walitumia mfumo huohuo wa usimbaji (encrypted)wa ujumbe wa Australia ili kuhakikisha ujumbe huo unafika na kueleweka na waliokusudiwa.
Ujumbe huo ulisema: hivi
Nippon to LMS: Thanks you for your assistance for this long while.Hope to see you again. Until then wish your good health.
Nippon Army.
Tafsiri ya ujumbe huo ukiwa;
“Kutoka Japan kwenda LMS: Asanteni kwa msaada wenu katika kipindi hiki chote. Tunatumaini tutakutana tena. Hadi wakati huo, tunawatakia afya njema. Jeshi la Japan.”