Harakati za Chadema na mbinu za kuchukuwa dola

ukimfuatilia ritz ni walwale akina zomba william malecela wanaelewa rangi nyeupe na nyeusi ila njaa ndizo zinawasumbua tu hawana jipya.wanaogopa mabadiliko wanajua chama chao kilivyo vunda
 
Katika wachangiaje 50 wa thread hii si zaidi ya 4 walioyaunga mkono mawazo ya kizandiki ya mheshimiwa njaa kali Ritz!
 
Katika wachangiaje 50 wa thread hii si zaidi ya 4 walioyaunga mkono mawazo ya kizandiki ya mheshimiwa njaa kali Ritz!

Ni kweli mkuu mie naweza kuwa na njaa kali lakini ujumbe wangu umefika.
 
​kwa wanaccm wengi humu hawajui hata wanaingiaje wewe ulibahatisha siasa za lumumba mpelekee nape hunajipya chadema 1 sawa na ccm 100 bungeni ha ha ha
Ni kweli mkuu mie naweza kuwa na njaa kali lakini ujumbe wangu umefika.
 
zilipendwa hizi, enzi zetu zilipendwa sana, ila ndo hivyo tena wakati ukutA
 
Mimi nadhani wewe ndio una matatizo.. Kwa mtu yeyote anayeitazama nchi hii kwa Ukanda nadhnai yeye ndiye mwenye matatizo kwa sababu unategema mtu kutoka kanda nyingine atawezesha maendeleo kanda yake..Haya ndio makosa makubwa ya Muungano wetu na Zanzibar..

Makosa ambayo yaletufikisha hapa tulipo tukawapata kina Mwinyi, Mkapa na sasa JK kwa kutazama dini zao na Asili yao..Kwa fikra hizo Muungano unazidi kuwa na matatizo zaidi na zaidi na sasa imefikia mahala hatuwezi tena kuungana..Yalitokea Suda, Ethiopia na sasa imefika mahala Tanzania na Nigeria lazima zivunje muungano wao kutokana na tofauti zao..

Hata mie nadhani nyie Pro-Chadema wengi JF ndio mna matatizo sana ya ubaguzi hivi unaweza kunipa sababu za msingi karibia 95% Pro-Chadema hawamtaki Zitto Kabwe kwa sababu gani.
 
Last edited by a moderator:
Madhaifu ya CCM ni mengi zaidi ya mapungufu ya CHADEMA...CCM isipojirekebisha 2015 inaachia dola.Huu ni ukweli unaouma
 
Hata mie nadhani nyie Pro-Chadema wengi JF ndio mna matatizo sana ya ubaguzi hivi unaweza kunipa sababu za msingi karibia 95% Pro-Chadema hawamtaki Zitto Kabwe kwa sababu gani.
Kwa sababu hata siku moja sii Mnauye wala Mukama wala JK hawezi kufanya kazi na Chadema au kusifia sera na mipango yao. Pengine Mbatia pekee na ndio maana anaitaka nafasi ya Zitto, sijui na yeye mdini?.. I like Zitto, na tunampenda wengi lakini kuna wakati unashindwa hata kumtetea.

Ubaguzi wowote huitwa Ubaguzi ikiwa kundi moja linanufaika na jingine kukandamizwa. Waislaam hawakandamizwi Chadema, kutopewa nafasi haina maana wanatengwa isipokuwa Waislaam wenyewe wamejitenga na CUF kutokana na dhana na fikra kama zenu.
 
Mkuu hujajibu swali naona unazunguka unaleta stori za CUF halafu usiwasemee Waislam kuwa wamejitenga na CUF sijui umeipata wapi mie ni Muislam lakini sipo CUF labda ungeniambia Waislam wa Zanzibar na CUF yao...ebu nijibu kwa nini Zitto hapendwi na Pro-Chadema wengi JF.
 
Dah mkuu umesha futur au bado?... nimesema kwamba anayoyafanya Zitto hayawezi kutokea kwa Mnauye, Mukama wala JK kufanya kazi na CDM.. Zitto anafanya hivyo, ni kinyume cha miiko ya kisasa. Hivi nambie ni mwanasiasa gani unayemjua wewe mbali na Zitto anajihusisha sana na sera na mipango ya CCM?. Only Zitto na yuko Upinzani..Kwa nini asi cross tu kwenda upande wa pili ijulikane?.

And for that, he is very wrong na asiutumie Uislaam kujikinga hapana ni yeye mwenyewe kwa maamuzi aloyafanya hayana uislaam wala Ukristu. Uislaam maana yake ni TOTAL submission to God (Allah) sio kutiwa maji au kuitwa Mohammad, wako waarabu kiibao wakristu, Mabedui na wasiokuwa na dini wanaitwa Mohammad tena Ukerewe kwetu tunawaita Mwamedi..

Wewe hauko CUF hapa janvini lakini najua ni kada wa CUF hiyo CCM umekaa hapo kwa sababu ya JK ngoja uchaguzi ukaribie tutakusikia ukija na sura nyingine - Nakukumbuka sana 2010..
 
Mkandara Mungu akubariki na akupe maisha marefu.
 
Mkuu hujajibu swali naona unazunguka unaleta stori za CUF halafu usiwasemee Waislam kuwa wamejitenga na CUF sijui umeipata wapi mie ni Muislam lakini sipo CUF labda ungeniambia Waislam wa Zanzibar na CUF yao...ebu nijibu kwa nini Zitto hapendwi na Pro-Chadema wengi JF.

Wanachadema wengi walioko JF hawana chuki yoyote na zitto bali wanampenda sana na kumtumaini sana.
Kwahiyo ikitokea amefanya jambo ambalo hawalipendi na halina maslahi kwa chama au yeye binafsi hawapepesi macho katika kumweleza ukweli.
Kwahiyo kutofautiana mawazo au maono haimaanishi kwamba kuna chuki dhidi yake.
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi.

Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kinafanya harakati na mbinu kuchukuwa dola lakini kuna mapungufu mengi sana ambayo ni kikwazo bahati mbaya Chadema wenyewe hawatambui hivyo vikwazo ndani ya chama chao..

Chadema bado wanategemea wanachama wasiotabirika, wanachama wake ni wale wanaoingia wakati wa mikutano ya hadhara na maandamano, Chadema wamekosa uhalali wa mtawanyo wa wanachama hai katika kila kona ya nchi.

Chadema baada kupata mafaniko katika uchaguzi mkuu uliopita wamejikuta wakihodhi wajibu wa jamii kisiasa kwa niaba ya vyama vingine wakihisi kwamba wao ni bora zaidi mbele ya jamii kuliko vyama vingine vyote nchini..

Chadema mpaka sasa hawajawa na uhakika wa jinsi ya kumpata kiongozi wa juu katika nafasi ya Mwenyekiti au Urais kutoka kanda nyingine, Chadema kimeweza kupata umaarufu kisiasa lakini bado wanakabiliwa na tatizo la umakini, uzoefu na mbinu nina hakika uteuzi wa mgombea urais kutoka Chadema ataleta mtarafuku mkubwa ndani ya chama hicho viongozi wa Chadema kutoka kanda zingine hawataafiki mgombea urais atoke eneo moja tu kila uchaguzi.

Chadema inasumbuliwa na kasumba ya ubinafsi na upendeleo wa kifamilia, Chadema wamejikuta wakipiga teke demokarasia ndani ya chama chao na wabunge wake wa viti maalum wengi wao wanatoka katika koo za waasisi wa chama.

kila political movement ina nucleaus point, yaani uanzilishi. Hoja hii ya udini na ukabila ingetumika kama itaonekana kuwepo kitakapokuwa madarakani jambo ambalo halitegemewi, ndio nionavyo mimi. Hata hivyo hv tatizo ni kubwa kiwango hicho kweli wanabodi?
 
Wako watu wa kutoa ushauri kwa CDM na huo ushauri wao ukapokelewa kwa mikono miwili lakini sio wa kutoka kwako ritz labda mtu awe mgeni hapa jamvini. Kawashauri magamba wenzio.

Tutaje waliorithiana madaraka kama si ccm
NAPE,BABA ALIKUA WAZIRI
MATHAYO DEVID MATHAYO,BABA ALIKUA WAZIRI
NCHIMBI,BABA,MAMA
MALIMA,BABA ALIKUA WAZIRI
MACHA,BABA ALIKUA BALOZI NA RAFIKI WA JK
KIKWETE,BABA ALIKUA DC
LUKUVI,BABA,SHANGAZI,MJOMBA
MAKAMBA,BABA ALIKUA KATIBU WA CCM
KILANGO,BWANA ALIKUA WAZIRI
TABWE,MAMA ALIKUA MBUNGE
MEMBE,SHEMEJI NI RAIS
VUA,RAIS NI RAFIKI WA BABA

SASA ENDELEA......
WALIOINGIA KWA MLANGO WA ONGO.......
 
Sio kila hoja ni ya kujadili kwa hoja,huwezi kuleta utani eti tujadili kwa hoja,zingine za kujadili kwa matusi ndo ukajiulize kwa nini umetukanwa tu
 
Mchana nilipopita hapa nilifurahi sana kuona Ritz leo kaanzisha thread ambayo kwa haraka haraka nilidhani anaweza kujenga hoja kisha akaitetea kwa umahiri kabisa. Na hata michango ya mwanzo ilipoanza kutolewa kwa jazba, alisema pro CDM hawawezi kujenga hoja, wanatukana tu.

Kusema ukweli Ritz hata wewe umenivunja moyo sana. Kumbe hata wewe kelele zote hizo na kejeli zote hizo, mwisho wa siku nimekuja kugundua kwamba hata wewe ni sifuri kabisa. Mbona baada ya pale sioni ukijibu wala kujenga hoja yenye mashiko hapa? Hivi kumbe hata wewe ni buyu kabisa. Iko wapi heshima yako. Kumbe ndio maana sikuwahi kuona umeachangia hoja kwa zaidi ya sentensi tatu. Maana kweli, siku zote huwa unaandika vimistari viwili, vitatu basi!

Kwa hiyo kumbe lengo lako lilikuwa kuzungumzia Zito tu basi?! Sasa si ungeanza kujenga hoja juu ya zito tu, kulikuwa na haja gani ya kutaja chama kizima?! Mimi naamini wewe ni mwenyeji sana humu ndani hata zaidi ya tulio wengi, imekuwaje unashindwa kujua kuwa kuna watu wenye uwezo mkubwa kujenga na kutetea hoja, mpaka leo hii unakuja kuchemka kiasi hiki?!
 
Back
Top Bottom