Harakati za Chadema na mbinu za kuchukuwa dola | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Harakati za Chadema na mbinu za kuchukuwa dola

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ritz, Aug 1, 2012.

 1. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Wanabodi.

  Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, kinafanya harakati na mbinu kuchukuwa dola lakini kuna mapungufu mengi sana ambayo ni kikwazo bahati mbaya Chadema wenyewe hawatambui hivyo vikwazo ndani ya chama chao..

  Chadema bado wanategemea wanachama wasiotabirika, wanachama wake ni wale wanaoingia wakati wa mikutano ya hadhara na maandamano, Chadema wamekosa uhalali wa mtawanyo wa wanachama hai katika kila kona ya nchi.

  Chadema baada kupata mafaniko katika uchaguzi mkuu uliopita wamejikuta wakihodhi wajibu wa jamii kisiasa kwa niaba ya vyama vingine wakihisi kwamba wao ni bora zaidi mbele ya jamii kuliko vyama vingine vyote nchini..

  Chadema mpaka sasa hawajawa na uhakika wa jinsi ya kumpata kiongozi wa juu katika nafasi ya Mwenyekiti au Urais kutoka kanda nyingine, Chadema kimeweza kupata umaarufu kisiasa lakini bado wanakabiliwa na tatizo la umakini, uzoefu na mbinu nina hakika uteuzi wa mgombea urais kutoka Chadema ataleta mtarafuku mkubwa ndani ya chama hicho viongozi wa Chadema kutoka kanda zingine hawataafiki mgombea urais atoke eneo moja tu kila uchaguzi.

  Chadema inasumbuliwa na kasumba ya ubinafsi na upendeleo wa kifamilia, Chadema wamejikuta wakipiga teke demokarasia ndani ya chama chao na wabunge wake wa viti maalum wengi wao wanatoka katika koo za waasisi wa chama.
   
 2. M

  Makamuzi JF-Expert Member

  #2
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 1,157
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Hayo maneno tulishazoea,una kingine kipya?kama hauna ntafute nkupe viroba vya konyagi ili utoe mapovu vizuri
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ritz una maoni mazuri na chokonozi juu ya CDM ambayo yatasababisha Mnakasha hasa kuhusu nafasi ya mgombe Urais na Uenyekiti wa CDM. Ila sasa subiri haki kutoka kwa jamaa wa CDM ambao wanadhani kila anayeikosoa CDM basi ni mgomvi wao.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #4
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ukweli unauma
   
 5. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pro cdm huwa hamna hoja zaidi ya kutukana
   
 6. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #6
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Rtz ficha upumbavu wako
   
 7. m

  mamajack JF-Expert Member

  #7
  Aug 1, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ubinafsi upo ccm kama hujui.angali ilivyokazi kumpata mgombea urais.
  M.k.were alimtengeneza bonge la kashfa mzee wetu yule mzanzibar,eti sio mtz,yawezakuwa angeshinda yeye angefanya kazi kwa maslahi ya nchi,
  waulize pia kina sumay,
   
 8. R

  Rommy01 New Member

  #8
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 31, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Seriously this is rediculous.....
   
 9. K

  Korogwe Vijijini Member

  #9
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 28, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilichogundua ni kwamba watu wengi wanafwata ushabiki kwenye siasa mana jamaa ametoa uchambuzi wa maana ila watu wanajaribu kukosoa.Kwa wasomi wazuri wa sheria wanaona ukwel na ata lisu anajua ukwel ila anaupindisha anayebisha atakuwa ana mawazo chakavu na aniandikie no. ili tubishane vizuri
   
 10. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu Kimbunga, Mkuu kingxvi, tatizo la Pro-Chadema wengi wao hawataki tutaje mapungufu ya Chadema sio siri nguvu ya Chadema kiuchumi na kiushawishi bado inabaki katika Kanda ya Kaskazini hii inatokana na ukweli waasisi wa chama na walezi wake wenye nguvu kiuchumi wanatoka kanda hiyo.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mheshimiwa mbona unajichosha kwa kusukuma ukuta wakati kimbuga kinavuma. Utaondoka wewe na ukuta wako tukose hata kiganja cha kuzika
   
 12. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,935
  Likes Received: 673
  Trophy Points: 280
  yaani kuna watu wanahangaika ku-post mambo ya hovyo hovyo kama wewe

  watch the walk of your steps .., this post portrays your thinking capacity is at standstill
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Tatizo lingine huyu ni diwani wa Chadema Arusha badala ya kujibu hoja kaja na viroja.

  Diwani naomba unijibu swali langu la msingi Chadema wana tofauti gani na CCM..Kwa nini viongozi wa Chadem a wamerithisha familia zao nafasi nyeti za uongozi na koo za waasisi wa Chadema wamepewa ubunge.
   
 14. Kaitampunu

  Kaitampunu JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,682
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Wako watu wa kutoa ushauri kwa CDM na huo ushauri wao ukapokelewa kwa mikono miwili lakini sio wa kutoka kwako ritz labda mtu awe mgeni hapa jamvini. Kawashauri magamba wenzio.
   
 15. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #15
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kwani wabunge wa ccm wanatoka kwenye koo za watu gani? Karibia kila waziri wa zamani au Rais watoto wao ni wakuu wa mikoa au wabunge au mawaziri... Ningeshauri mue mnafunga hiyo midomo yenu ka hamna cha maana cha kusema
   
 16. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #16
  Aug 1, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  umeliona hilo mkuu je na vyama vingine kama CCM,CUf, ADC, DP, UDP nazo unaziongeleaje? kwa point ambayo umeiongea hapa?
   
 17. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #17
  Aug 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Juu ya CDM mtaweweseka sana tu. Na bado!
   
 18. M

  Mlyafinono Senior Member

  #18
  Aug 1, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tutajie mgombea urais wa ccm 2015
   
 19. B

  Bukutonaga JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2012
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 246
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  NI KWELI

  1.Chadema ni bora zaidi
  2.Chadema ya leo ina wanachama wengi sana tena walio hai
  3.Chadema haina mambo ya ubinafsi na upendeleo kama ilivyo CCM
  4.Viongozi wa chadema kutoka kanda zingine wataafiki Mugombea kutoka kanda yoyote ya nchi kikubwa awe mwadilifu,mzalendo kama walivyo wagombea wetu wa nafasi za urais walotangulia.


  Majungu hayo yapeleke LUMUMBA ndo kuna habari za udaku,watanzania tumechoka tunataka tumaini jipya "MANENO YA LAWRENCE MASHA"

  Thanks
   
 20. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kwanza nikiri kwamba kukosoa ni utamaduni wa kujenga, hapo hakuna shaka.

  Umeanza vizuri kabisa mkuu, ila mimi napingana na wewe kidogo hapo kwenye red. Sishangai kwani unapokuwa vitani huchagui silaha. Na hii imekuwa silaha ambayo wapinzani wa CDM wamekuwa wakiitumia kwa muda mrefu sasa, inagawa binafsi naona kama kwa sasa haina nguvu sana ktk vita hii.

  Kitu ambacho watu wengi sasa, ama kwa makusudi au kwa kutokujua, mfumo wa kisiasa wa sasa sio kama ule wa kumwondoa mkoloni. Kipindi cha uhuru, adui alikuwa mkoloni, kwa hiyo vuguvugu la mageuzi lilijumuisha jamii zote za kitanzania. Ila kwa sasa ni tofauti, vuguvugu la mageuzi linahusu jamii moja, yaani familia moja(Tanzania). Kwa maana kwamba unapambana na adui ambaye ni ndugu yako, ili upate support itategemea jinsi gani utawashawishi wanafamilia wenzako kukuunga mkono.

  Kwa maana hii mwanzo wa mageuzi lazima utaanza na mtu mmoja, kisha wawili, theni watatu, wanne, watano.... nk. Kwa vyoyote huwezi kuanza na kupata wafuasi wengi kwa mara moja. Hilo sijui kama unalitambua au la, ila kumbuka unapokuwa unaanza vuguvugu kama hili adui yako naye hajalala. Lazima na yeye anatafuta mbinu za kukudhoofisha, ndio maana hapa hata wewe unatumika kuwadhoofisha wapinzani. Hii ni haki yako kabisa, maana haya ni mapambano.

  Kwa issue ya ukanda au ukabila/familia halina tofauti na maelezo yangu ya hapo juu. Siku zote vuguvugu la mageuzi huanza na watu wenye mawazo na itikadi inayofanana. Hii haimfungi mtu kuanza na jamaa zake, wafanyakazi wenzake, marafiki zake kwa sababu unapoanza kunadi sera zako ni lazima utaanza na watu walio karibu yako. Na hii ina sababu nyingi tu, maana pengine ndio watu unaowaamini, mimi sioni kama hilo ni tatizo. Hata wewe kesho ukifikiria kuanzisha taasisi fulani, watu wa kwanza kuwaona lazima ni watu wako wa karibu unaodhani unawaamini.

  Kuhusu kuenea sehemu mbalimbali nchini, hii iko wazi. Moto siku zote utaanza na majani makavu point A kisha utaenea hadi point B, C, D....nk. Namaanisha kwamba kuenea kwa CDM sehemu mbalimbali nchini kutategemea uwezo na kasi yake ya kujinadi, ambayo hata hivyo lazima ku'overcome resistance kutoka kwa wapinzani wake wanaozidi kila kukicha. Lakini hata hivyo wanajitahidi, maana hata wewe umekiri kwamba uchaguzi uliopita wamepata mafanikio fulani. Huu kwao ni mwanzo mzuri.

  Kuhusu mgogoro wa uongozi ndani ya chama, mimi huwa sipendi kuishi kwa hisia. Maana mambo mengi yamekuwa yakichukuliwa kwa
  'hear said' tuuu, lakini ukijakufuatilia unakuta ni mbinu tu za kuwombea adui yako njaa. Lakini ukweli unabaki kwamba muda huo ukifika kila kitu kitakuwa wazi, tutajua nani ndiye nani.

  Ninachosisitiza ni kwamba,sio tu CDM, bali hata vyama vingine vilivyopo na vitakavyoanzishwa, visinyimwe fursa ya kujieneza kwa sababu nyepesi nyepesi kama hizi ulizotoa hapa. Waachwe watanzania wachague vyama na viongozi wanaowataka.

  Nadhani nimeeleweka mkuu.
   
Loading...