Harakati ya kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Thailand

JF-Expert Member
Nov 15, 2019
262
778
Kifupi Zanzibar hawatupendi wa Tanganyika kwa kudhani wao ni waarabu koko wa oman (fikra za kimaskini)
Sasa kuliko kuleteana shida huko mbele ya safari, naomba serikali ifikirie kuuvunja huu muungano kwa amani bila damu kumwagika.

Haiwezekani kero za muungano zinatatuliwa tu zile zinazo wa favor wazanzibar huko Wabara tunaonekana punguani ndani ya muungano.
Sasa Zanzibar lazima iamue kuwa mkoa ndani ya Tanzania au ijitoe kwenye muungano.

Mawakili wa Tanzania wenye utaalamu juu ya mambo ya sheria fungueni kesi ya kupinga huu muungano sisi wananchi tutawaunga mkono. Hili jambo la Zanzibar kujiona bora kuliko nchi kamili ya Tanzania na wananchi wake halikubaliki hata kidogo.

Baada ya kuuvunja huu muungano huu uchwara, Wazanzibar mlio bara mjiandae kurudi kwenu Zanzibar au muukane uraia wa Zanzibar na muwe raia kamili wa Tanzania.

Heli kufadhili na kuithamini mbuzi Utakunywa mchuzi kuliko kuthamini watu fulani hivi wasiojitambua na kujali utu wa ndugu zao.

Naomba viongozi wetu muweke usawa kwenye huu muungano, Watanganyika tusibaguliwe tunapoitaji ajira na ardhi ya Zanzibar kwa sababu tunaaminishwa kwamba hii ni nchi moja.
 
Acha ukabila. Na uhasama. Hamna Mzanzibari yoyote anaepinga Uepo wa muugano ila anacholalamika ukandamizaji na mifumo iliowekwa baina ya bara na visiwani.
Sisi wa zanzibari tupo wachache lakini tunapinga kukandamiziwa na mkubwa yoyote.
 
Kimsingi Wazanzibar ndio wenye haki ya kulalamika na siyo Watanganyika.

Population yao ni ndogo sana, ni aibu kwa Mtanganyika kuwalalamikia Wazanzibar wakati power zote zipo Tanganyika.
Sasa kama viongozi wetu hawa equalize mambo sisi wananchi tufanyeje. Si ni kuingia front tu
 
Kuna watu wanafikiri huu Muungano,ni wa watu,au ulitengenezwa kidemokrasia,na unaweza kuvunjwa kwa makaratasi au mahakamani

Hicho kitu hakipo,kama ambavyo,Mtwara waliishawahi kutaka wajitenge,na rasilimali zao,zisije dar!au mikoa ya kaskazini Arusha,Klm,Tanga kutaka kujitenga,Hilo haliwezekani,deepstste imeamua hivyo!

Zenj,ni sehemu ya Tanzania kama ilivyo Kigoma,Tabora,Tanga,au Singida,sasa unatenga vipi sehemu ya nchi!?hicho kitu hakipo,mtaishia kuumizwa tu

Kwa wale wanaofatilia duru za kimataifa,watakuwa wanajua kilichowapata wale waliotaka kujitenga wa Jimbo la Catalonia kule Spain,walifulumshwa,wakakimbia nchi,sasa hv wapo jera.

Au fatilia kinachoendelea Hongkong na China,harsfu eti umwambie Mchina,aiache Hongkong iwe huru!!

Don't be naive guys!?Zenj haitatoka ndani ya Muungano,it's a security issue,Kuna vitu ccm wanaweza kufanya,lakini inapokuja swala la Zenj,hapo issue inakuwa sio Siasa Tena,ni survival ya Tanzania!!

Zenj will never go away,get it into ur heads and move on!!Malalamiko ya wananchi yapo Kagera,Kigoma,Tabora,Mtwara,lakini sio sababu za hiyo mikoa kujitenga,Swala la Muungano,ni kubwa kuliko hata Raisi wa Tanzania!

Hata yeye akilegalega,wapo hardliners watamtuliza tu,
 
Eti sisi wa
Eti sisi wananchi tutakuwa nyuma yenu mawakili!!!wananchi wa wapi?
Muungano ni tunu yetu na Kila kiongozi wa mihimili yote mpaka jeshini huapa kuulinda

Kuhusu kuvunjika hii will never happen
 
Wanasemaga Mshika mawili moja humponyoka ! Kwanza Katiba mpya ? Au kuvunja muungano ?? 😅
 
Kimsingi Wazanzibar ndio wenye haki ya kulalamika na siyo Watanganyika.

Population yao ni ndogo sana, ni aibu kwa Mtanganyika kuwalalamikia Wazanzibar wakati power zote zipo Tanganyika.
Kwani population inatakiwa iwe kigezo cha kulalamika? Basi waongeze kuzaana. Kuwa na power haina maana ya kuwa tuwaonee.
 
Ushawai pata kesi ya ugaidi??? Ww jiingize kwenye masuala ya muungano

Waulize uamsho waliukataa muungano wakasota jela miaka 7
 
Kifupi Zanzibar hawatupendi wa Tanzania bara kwa kudhani wao ni waarabu koko wa oman (fikra za kimaskini)
Sasa kuliko kuleteana shida huko mbele ya safari, naomba serikali ifikirie kuuvunja huu muungano kwa amani bila damu kumwagika.

Haiwezekani kero za muungano zinatatuliwa tu zile zinazo wa favor wazanzibar huko Wabara tunaonekana punguani ndani ya muungano.
Sasa Zanzibar lazima iamue kuwa mkoa ndani ya Tanzania au ijitoe kwenye muungano.

Mawakili wa Tanzania wenye utaalamu juu ya mambo ya sheria fungueni kesi ya kupinga huu muungano sisi wananchi tutawaunga mkono. Hili jambo la Zanzibar kujiona bora kuliko nchi kamili ya Tanzania na wananchi wake halikubaliki hata kidogo.

Baada ya kuuvunja huu muungano huu uchwara, Wazanzibar mlio bara mjiandae kurudi kwenu Zanzibar au muukane uraia wa Zanzibar na muwe raia kamili wa Tanzania.

Heli kufadhili na kuithamini mbuzi Utakunywa mchuzi kuliko kuthamini watu fulani hivi wasiojitambua na kujali utu wa ndugu zao.
😠😠
 
Back
Top Bottom