Happy Birthday Tido Muhando, mwamba imara kwenye tasnia ya Habari

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,825
Alianzia redio ya Taifa, Radio Tanzania Dar Es Salaam, kabla ya kuelekea Kenya ambako alifanya kazi kwa miaka mingi kabla ya kujiunga na shirika la utangazaji la Uingereza, BBC katikati ya miaka ya 1990.

Mojawapo ya maswali aliyoomuuliza Rais Magufuli ilikuwa kuhusu Demokrasia nchini na upatikanaji wa katika mpya kwenye utawala wake, Rais Magufuli aliishia kumwambia Tido ana maswali ya kichokozi. Magufuli hakurudia tena kuita waandishi Ikulu na kupokea maswali, Tido alikuwa mmojawapo wa waongoza mahojiano hayo kati ya wawili mwaka 2016.

Tido pia amefanikiwa kufanya mahojiano na Rais Kikwete wakati akiwa madarakani na Rais wa sasa, Samia Suluhu. Pia alifanya mahojiano na mwanasiasa wa upinzani aliyejizolea umaarufu, Dkt. Wilbroad Slaa alipojiengua Chadema kuelekea uchaguzi wa 2015 baada ya ujio wa Edward Lowassa.

Mwaka 2018 Tido alifunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi aliyodaiwa kufanya 2008, mwaka 2019 upande wa Jamhuru ulishindwa kuthibitisha akaachiwa huru.

Hongera kwa kutimiza miaka 75 Tido ukiwa bado mwenye nguvu na afya. Mapinduzi uliyoyafanya TBC na Azam yanaonekana.

Tido Mhando.jpg
 
Back
Top Bottom