Ndugu zangu wanaJF kwanza kabisa niwaombe radhi kwa kuwa mbali nanyi wakati wote mlipokuwa mnafungua champaigne, majukumu yalikuwa yamenitinga sana kwa siku ya leo.
Pili napenda kuwashukuru wote mlionitakie kheri leo hii katika kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa ninawashukuru sana. Huu uzee umenijia vibaya hadi nikawa nimesahau jambo la msingi kama hili, nadhani ni kwakuwa shughuli hii imegongana na mambo yetu yale ya tohara!! lol
BTW, nimezipokea kwa mikono miwili na moyo mkunjufu kabisa dua zenu, sala zenu na zawadi zenu. Kwa hakika kabisa kila mmoja hapa JF amekuwa na mchango mkubwa sana katika maisha yangu tangu nijiunge hapa JF, tarehe 1 July 2008. Pamoja na misukosuko yote ninayokumbana nayo nimeweza kuhimili vishindo kwani sijawahi kupata ban wala warning.
Natambua mimi ni mwanadamu dhaifu, inawezekana kuna mahali niliwakwaza baadhi yenu, naomba nitumie fursa hii kuwataka radhi na tuangalie mbele kwakuwa hakuna aliye mkamilifu. Nitumie pia fursa hii kuwaomba tuendelee kushirikiana kadri tunavyoweza kila mmoja kwa nafasi yake. JF itufanye tuwe familia moja na yenye upendo zaidi. So far najivunia marafiki niliowapata hapa, mabinti(watoto) niliojipatia hapa-ni dhahiri kwamba mimi ni baba wa ukweli. Wengine nimefanikiwa kuonana nao 'LIVE", wengine ninawasiliana nao kwa njia za simu, emails, skype, facebook na twitter.
Niwatakie wote heri na fanaka katika maisha yenu na kazi zenu mnapokaribia mwisho wa mwaka huu wa 2012 na kutarajia kuanza mwaka mwingine wa mafanikio makubwa wa 2013.