Hapo zamani

Hapo zamani

Jonogomero

Member
Joined
Feb 8, 2012
Posts
99
Reaction score
27
Hapo zamani kwenda na mfuko wa rambo shuleni ilikuwa kawaida

Hapo zamani kulamba makamasi ilikuwa kawaida saaaana

Hapo zamani kuokota hela ilikuwa kawaida sana, siku hizi hata hela ya bandia kuokota ni kazi kweli kweli

Hapo zamani kusingizia unaumwa ili usiende shule ilikuwa kawaida

............ Hapo zamani.......................
 
Hapo zamani ukirudiarudia thread unapigwa BAN.
 
Hapo zamani kuitwa mchumba na binamu yako ni kawaida sana sikuhizi ukiitwa hata na ndugu watu wanajua tayari
 
Hapo zamani ilikuwa ngumu sana kuiona kondomu, lakini sasa hivi hadi watoto wadogo wamezigeuza mapulizo
 
HAPO ZAMANI MTU AKIFA MTAA UNAFUNGWA , SIKUHIZI MSIBA nyumba hii, NYUMBA YA PILI DISKO!!
 
hapo zamani, wanawake walikuwa wanajua kupika kama mama zao na hata akiwa mnene hana kitambi, ila siku hizi ni walevi na wana vitambi kama baba zao
 
Searching...100%
Loading...100%
Network Connected !

Hapo zamani kwenda shule bila viatu ilikuwa kawaida.
 
hapo zamani ulikuwa unaweza ukakaa town afu ukatafutiwa wife kijijini na life linasonga, siku hizi....
 
hapo zamani mdingi akinunua sofa,watoto mnatandikiwa mkeka chini.
hapo zamani hakukua na simu za mkononi,basi ile ya TTCL(posta na simu) inafungiwa kwenye kiboksi chenye kufuli.

hapo zamani kunywa soda ilikua hadi ulazwe.

hapo zamani stesheni ya redio ilikua RTD tu.
 
hapo zamani ukivaa raba DH unachekwa, vijana kwasasa eti ndio fashen
 
hapo zamani kulikuwa na sungura na fisi.
hapo zamani wanyama walikuwa wanaongea!!
 
Hapo zamani kwenda na mfuko wa rambo shuleni ilikuwa kawaida
Hapo zamani kulamba makamasi ilikuwa kawaida saaaana
Hapo zamani kuokota hela ilikuwa kawaida sana, siku hizi hata hela ya bandia kuokota ni kazi kweli kweli
Hapo zamani kusingizia unaumwa ili usiende shule ilikuwa kawaida
............ Hapo zamani.......................

Zamani zipi unazomaanisha maana inawezekana wote hatukuwepo
na wala hayo uliyoyataja hayakuwepo pia! Mi' nadhani hapo zamani
nilikuwa sijazaliwa...
 
Kina dada wanajua hii. Hapo zamani kuingia na roller kwenye sherehe ilikuwa fasheni. Hapo zamani ukiweka curl nywele hakuna kuosha.
 
Hapo zamani sikukuu ya krismas ikikaribia mnapelekwa mjini kununuliwa nguo mpya
 
Back
Top Bottom