Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,508
- 830,009
Dhima ya kanisa kama taasisi yenye kutoa tumaini kwa waliokata tamaa, wahitaji wa ujenzi wa kiroho ili kuweza kuwa na imani thabiti juu ya kile wanachohubiriwa na kukiamini
Kanisa ni sehemu ya jamii na ni jamii yenye wanadamu... Viumbe wa mwili wenye nyama... Mwili huu wenye nyama ni muunganiko wake na roho... Hivyo basi kanisa kama taasisi ya kiimani haipaswi kushughulika na roho tu bali na mwili pia... Huwezi ukashughulika na kimoja na kuacha kingine na bado ukadhani unatenda kwa ukamilifu.... Utakuwa umekengeuka...!
. Kanisa lina dhima ya kutoa chakula cha kiroho lakini pia na chakula cha kimwili
. Kanisa lina dhima ya kutoa uponyani wa kiroho lakini na wa kimwili pia
. Kanisa lina dhima ya kutoa elimu ya kiroho lakini na ya kidunia pia
. Kanisa lina dhima ya kusaidia matatizo yote ya kiroho lakini na ya kimwili pia
Hili litawezekanaje?
Huyu unayetarajia kumlisha chakula cha kiroho hakikisha kabla hajapata hicho cha kiroho amepata cha kimwili... Hivyo mjengee mazingira na uwezo ili aweze kujihudumia kimwili...
Huyu unayetarajia kumpa uponyaji wa kiroho... Msaidie kwanza apate uponyaji wa kimwili kwa kuwekeza kwenye Huduma za afya na vifaa tiba, hospital, na vituo vya afya
Huyu unayetarajia kumpa elimu ya kiroho.... Msaidie aelimike kiakili kwanza kwa kuwekeza kwenye elimu, shule vyuo na taasisi za kielimu.. Kwa njia hii ataweza kujihudumia kimwili.....
Huyu unayetarajia kumsaidia kiroho msaidie kwa kuwekeza kwenye vituo vya yatima wajane na wasiojiweza.....
Je makanisa haya ya watu binafsi... Yanayojulikana kama ya kiroho yanafanya yote haya ama yameweke tu kiroho kwa kufanya miujiza yenye harufu ya utapeli, wizi na mambo ya kishirikina? Kishapo matoleo ya waumini masikini kutumika kutimiza matakwa ya mwili na tamaa za kidunia zilizopiliza?
They are failing big time... Huruma ni kwa hao waamini na waumini wao