Hapa ndipo yanapofeli makanisa ya kiroho

Hapa ndipo yanapofeli makanisa ya kiroho

Je makanisa haya ya watu binafsi... Yanayojulikana kama ya kiroho yanafanya yote haya ama yameweke tu kiroho kwa kufanya miujiza yenye harufu ya utapeli, wizi na mambo ya kishirikina? Kishapo matoleo ya waumini masikini kutumika kutimiza matakwa ya mwili na tamaa za kidunia zilizopiliza?
Mkuu imeandikwa hivi; "utafuteni kwanza Ufalme wa MUNGU na hayo yote mtazidishiwa".

Je wanadamu wanaelewa "Ufalme wa Mungu" ni nini? Hapa ndipo tatizo linapoanzia, wengi hawajui na ndiyo maana wanadanganywa na haya makanisa tena siyo ya kiroho tu, bali makanisa mengi sana yanadanganya.
 
Samahani sana labda kwanza tufahamishane maana ya kanisa.

Kwangu mimi Kanisa ni Kristu, na sio taasisi wala kikundi cha watu.

Kanisa lina kazi kuu tatu tu 1. Kufundisha(Nabii), 2. Kuongoza(Mfalme), 3.Kutakatifuza(Kuhani)
Yesu Kristu ni Kuhani, Nabii na Mfalme. Hizo ndizo kazi za kanisa!
 
Last edited:
Unamaanisha nini kusema makanisa ya watu binafsi halafu ukayaita ya kiroho? kuna makanisa kama TAG, EAGT na mengineyo yasiyo ya watu binafsi na ni ya kiroho. Ungechora mstari kwenye hilo kwanza.
Nimemaanisha hivyo kwa mifano ifuatayo
. Kanisa la Gwajima
. Kanisa la mzee wa upako
. Kanisa la Kakobe
Baada ya hapo hufuata majina yake yanayotsmbulika kisheria... Lakini hata waumini wake ukiwauliza wanasali wapi watakwambia nasali kwa fulani
Pia Nimetuma neno makanisa ya kiroho kwakuwa ukiachana na kutanguliza mmiliki wake... Katika ujumla wake yanaitwa ama kujulikana hivyo
.
 
Kila Kanisa hata hayo ya kiroho yankuwa na malengo ya uanzishwaji wake. Kama haifati msingi wauanzishwaji tunaweza kuanzia hapo.
Lakini pia so lazima makanisa yanayoitwa ya kiroho yafanye sawa na yale mnayiyaita yasiyo ya kiroho.
 
Kanisa ni moja tu aliloanzisha Yesu Kristo na kuweka askofu wa kwanza Petro. Kanisa hilo linaweza kukutajia viongozi wake kuanzia Petro hadi wa leo bila mwaka wowote kupotea toka mwaka 33AD.

Hakuna Kanisa lingine lolote linaloweza kutaja viongozi wake kwa udhibitisho toka mwaka 33AD hadi leo.

Makanisa yote waanzilishi wake wanafahamika hadi lini yameanza.

Hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kuanzisha Kanisa kazi ambayo alishafanya Yesu Kristo.

Kanisa hilo ni Moja, Takatifu Katoliki la Mitume. Watu binafsi hawafungui makanisa bali madhehebu, ministries. Ndio maana Kanisa Katoliki halikubali kuitwa Dhehebu maana si tawi bali mti wenyewe.

Kuhusu huduma za kikristo huko kwingine ni kweli zipo huduma Roho Mtakatifu anatenda katikati yao lakini humo humo kuna chui wengi wenye ngozi ya kondoo.
Mkuu kuna uthibitisho wowote kuwa petro aliachiwa kanisa katoriki na Yesu wa Nazareth halafu kanisa likahamia Italia.
Kwa kumbukumbu zangu Petro alikaa yerusaleem sikumbuki kama alienda italia kuanzisha rc au kuwa papa wa kwanza kama anavyoitwa mahala pengine. Nisaidie hapo
 
Kuna kipindi nilikuwa kujijini huko nikakuta akina mama wanahangaika kufanya vibarua vya kulima eti wapate nauli ya kwenda kuonana na nabii wa kanisa flani wanaita efatha kama sijakosea!

Maisha magumu kweli!!

Halafu mwaka huu kulikuwa Kuna Uzi humu huyo nabii amenunua private jet mpya kabisa!

Haya mambo yalinifikirisha sana
 
Kuna kipindi nilikuwa kujijini huko nikakuta akina mama wanahangaika kufanya vibarua vya kulima eti wapate nauli ya kwenda kuonana na nabii wa kanisa flani wanaita efatha kama sijakosea!

Maisha magumu kweli!!

Halafu mwaka huu kulikuwa Kuna Uzi humu huyo nabii amenunua private jet mpya kabisa!

Haya mambo yalinifikirisha sana
Ni uchoyo na ubinafsi uliopitiliza kununua kitu cha gharama kama hicho badala walau kujenga hata kituo cha watoto yatima na wazee
 
.
IMG-20191118-WA0160.jpeg
 
Dhima ya kanisa kama taasisi yenye kutoa tumaini kwa waliokata tamaa, wahitaji wa ujenzi wa kiroho ili kuweza kuwa na imani thabiti juu ya kile wanachohubiriwa na kukiamini
Kanisa ni sehemu ya jamii na ni jamii yenye wanadamu... Viumbe wa mwili wenye nyama... Mwili huu wenye nyama ni muunganiko wake na roho... Hivyo basi kanisa kama taasisi ya kiimani haipaswi kushughulika na roho tu bali na mwili pia... Huwezi ukashughulika na kimoja na kuacha kingine na bado ukadhani unatenda kwa ukamilifu.... Utakuwa umekengeuka...!

. Kanisa lina dhima ya kutoa chakula cha kiroho lakini pia na chakula cha kimwili
. Kanisa lina dhima ya kutoa uponyani wa kiroho lakini na wa kimwili pia
. Kanisa lina dhima ya kutoa elimu ya kiroho lakini na ya kidunia pia
. Kanisa lina dhima ya kusaidia matatizo yote ya kiroho lakini na ya kimwili pia

Hili litawezekanaje?
Huyu unayetarajia kumlisha chakula cha kiroho hakikisha kabla hajapata hicho cha kiroho amepata cha kimwili... Hivyo mjengee mazingira na uwezo ili aweze kujihudumia kimwili...
Huyu unayetarajia kumpa uponyaji wa kiroho... Msaidie kwanza apate uponyaji wa kimwili kwa kuwekeza kwenye Huduma za afya na vifaa tiba, hospital, na vituo vya afya
Huyu unayetarajia kumpa elimu ya kiroho.... Msaidie aelimike kiakili kwanza kwa kuwekeza kwenye elimu, shule vyuo na taasisi za kielimu.. Kwa njia hii ataweza kujihudumia kimwili.....
Huyu unayetarajia kumsaidia kiroho msaidie kwa kuwekeza kwenye vituo vya yatima wajane na wasiojiweza.....

Je makanisa haya ya watu binafsi... Yanayojulikana kama ya kiroho yanafanya yote haya ama yameweke tu kiroho kwa kufanya miujiza yenye harufu ya utapeli, wizi na mambo ya kishirikina? Kishapo matoleo ya waumini masikini kutumika kutimiza matakwa ya mwili na tamaa za kidunia zilizopiliza?
They are failing big time... Huruma ni kwa hao waamini na waumini wao
Bahati mbaya ni kuwa ulichoandika ni kinyume na biblia. Hakuna jambo kama hilo na wale wanaoshabikia ni wanaotaka kusikia wakipendacho, itching ears.

Sishabikii makanisa ya kiroho kwa kile yakifanyacho, bali pia sishabikii hiki ulichoandika kwani ni uongo mnele ya maandika matakatifu. Tuitafute kweli ya biblia na sio kile tunachokitamani kiwe.
 
Tumeaswa kuitafuta elimu... Elimu ni dhana pana sana... Kile unachodhani ni uongo ndio kinaweza kuwa chenye ukweli wenye uhalisia mwingi ndani yake.. Lakini bado haimaanishi kwamba kwakuwa tu hukubaliani na nilichoandika basi post hii haina maana
Bahati mbaya ni kuwa ulichoandika ni kinyume na biblia. Hakuna jambo kama hilo na wale wanaoshabikia ni wanaotaka kusikia wakipendacho, itching ears.

Sishabikii makanisa ya kiroho kwa kile yakifanyacho, bali pia sishabikii hiki ulichoandika kwani ni uongo mnele ya maandika matakatifu. Tuitafute kweli ya biblia na sio kile tunachokitamani kiwe.
 
Back
Top Bottom