Hapa ndipo yanapofeli makanisa ya kiroho

Hapa ndipo yanapofeli makanisa ya kiroho

Nikuulize kidogo mkuu Mshana ukisema makanisa unakuwa na maana ipi?

Hawa kwa mfano Mzee wa Upako, Mwamposa, na wanaofanana nao nao wanaingia kwenye makanisa?

Maana unaweza kuwalaumu kumbe wao hawapo kwenye category hiyo
Makanisa kwa maana hiyo ya hayo ya kwao
 
Mshana jr spiritual protocol ya kupokea ni kutoa, the more you give the more you receive especially when you give to the less privilage people Luka 6:38
Hii sheria naonaga wamebadilisha wameona wao hawana obligation na wamesahau baraka huambatana na laana. Badala yake wanaeneza chuki kwa T B Joshua badala ya kujifunza na kufanyia kazi.
Angalia pamoja na idadi kubwa ya makanisa bado maasi yameongezeka mana tuna muita Mungu mdomoni na sio kutoka moyoni.

. Kanisa lina dhima ya kutoa chakula cha kiroho lakini pia na chakula cha kimwili
. Kanisa lina dhima ya kutoa uponyani wa kiroho lakini na wa kimwili pia
. Kanisa lina dhima ya kutoa elimu ya kiroho lakini na ya kidunia pia
. Kanisa lina dhima ya kusaidia matatizo yote ya kiroho lakini na ya kimwili pia
TB ndiye mtumishi pekee ninayemwamini,ukisikiliza mahubiri yake ni tofauti kabisa na watu wanavyomwelezea
 
Dhima ya kanisa kama taasisi yenye kutoa tumaini kwa waliokata tamaa, wahitaji wa ujenzi wa kiroho ili kuweza kuwa na imani thabiti juu ya kile wanachohubiriwa na kukiamini
Kanisa ni sehemu ya jamii na ni jamii yenye wanadamu... Viumbe wa mwili wenye nyama... Mwili huu wenye nyama ni muunganiko wake na roho... Hivyo basi kanisa kama taasisi ya kiimani haipaswi kushughulika na roho tu bali na mwili pia... Huwezi ukashughulika na kimoja na kuacha kingine na bado ukadhani unatenda kwa ukamilifu.... Utakuwa umekengeuka...!

. Kanisa lina dhima ya kutoa chakula cha kiroho lakini pia na chakula cha kimwili
. Kanisa lina dhima ya kutoa uponyani wa kiroho lakini na wa kimwili pia
. Kanisa lina dhima ya kutoa elimu ya kiroho lakini na ya kidunia pia
. Kanisa lina dhima ya kusaidia matatizo yote ya kiroho lakini na ya kimwili pia

Hili litawezekanaje?
Huyu unayetarajia kumlisha chakula cha kiroho hakikisha kabla hajapata hicho cha kiroho amepata cha kimwili... Hivyo mjengee mazingira na uwezo ili aweze kujihudumia kimwili...
Huyu unayetarajia kumpa uponyaji wa kiroho... Msaidie kwanza apate uponyaji wa kimwili kwa kuwekeza kwenye Huduma za afya na vifaa tiba, hospital, na vituo vya afya
Huyu unayetarajia kumpa elimu ya kiroho.... Msaidie aelimike kiakili kwanza kwa kuwekeza kwenye elimu, shule vyuo na taasisi za kielimu.. Kwa njia hii ataweza kujihudumia kimwili.....
Huyu unayetarajia kumsaidia kiroho msaidie kwa kuwekeza kwenye vituo vya yatima wajane na wasiojiweza.....

Je makanisa haya ya watu binafsi... Yanayojulikana kama ya kiroho yanafanya yote haya ama yameweke tu kiroho kwa kufanya miujiza yenye harufu ya utapeli, wizi na mambo ya kishirikina? Kishapo matoleo ya waumini masikini kutumika kutimiza matakwa ya mwili na tamaa za kidunia zilizopiliza?
They are failing big time... Huruma ni kwa hao waamini na waumini wao

Usia Kuntu kabisa....
 
Well Mshara umetoa elimu nzuri sana kwa hawa viongozi wa makanisa. Jambo moja huwa natafakari msingi wa haya makanisa ni nini? Mi naona kuna shida ya kiroho ambazo zimetawala kuna unclean spirit zinatakontrol haya makanisa .Unakuta mwanzilishi wa kanisa alikuwa anahudumu kanisa flani wakatofautiana (hapa tusitake kujua msingi wa tofauti zao)na kiongozi mwingine roho ya uasi(rebellion) inamuingia anaondoka anaanzisha kanisa lake. Kumbuka hata akiondoka atatafuta watu wake wa kuondoka nao sasa asimame madhabahuni sasa majigambo yakutosha too much controlling anaona waumni kama ni mali yake , ataka kunyenyekewa mpk kuna wakati unajiuliza hawa ni kwamba wameamua kuwa mateka wa mtu .

Ndugu zangu wakristo wenzangu tusome biblia tutafute maarifa, na roho wa Mungu hatakuacha upotee ukimuweka Mungu mbele
Asante..
 
Acheni kuwasema watumishi mtapata laana,kwasababu hao wanaokwenda huko hawaitwi wanakwenda wakiwa na akiri zao timamu na nyie wote mnajua wajinga ndiyo waliwao unakosaje kupambanua wapiga dili na kanisa la Mungu ?

Hiyo laana iko katika kitabu gani cha biblia? Hawa ni binadamu kama sisi wanafanya makosa Warumi 15:14 Ndugu zangu,nimehakikishwa mimi mwenyewe kwa habari zenu ya kuwa ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana.
 
Kanisa ni moja tu aliloanzisha Yesu Kristo na kuweka askofu wa kwanza Petro. Kanisa hilo linaweza kukutajia viongozi wake kuanzia Petro hadi wa leo bila mwaka wowote kupotea toka mwaka 33AD.

Hakuna Kanisa lingine lolote linaloweza kutaja viongozi wake kwa udhibitisho toka mwaka 33AD hadi leo.

Makanisa yote waanzilishi wake wanafahamika hadi lini yameanza.

Hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kuanzisha Kanisa kazi ambayo alishafanya Yesu Kristo.

Kanisa hilo ni Moja, Takatifu Katoliki la Mitume. Watu binafsi hawafungui makanisa bali madhehebu, ministries. Ndio maana Kanisa Katoliki halikubali kuitwa Dhehebu maana si tawi bali mti wenyewe.

Kuhusu huduma za kikristo huko kwingine ni kweli zipo huduma Roho Mtakatifu anatenda katikati yao lakini humo humo kuna chui wengi wenye ngozi ya kondoo.
 
Kanisa ni nini?
 
Kila Mwenye Macho Aone Pia Mwenye Masikio Asikie Roho Wa Mungu Awaambia
 
Kanisa ni nini?
Haya chini ni maelezo niliyochopoa kutoka tovuti ya Catholic Answers.

Catechism of the Catholic Church states, "the word ‘Church’ (Latin ecclesia, from the Greek ek-ka-lein, to ‘call out of’) means a convocation or an assembly" (CCC 751).

The Vatican II’s Decree on Ecumenism (Unitatis Redintegratio) states that even though "our separated brethren (mfano Protestants, Anglicans e.t.c) . . . are not blessed with that unity that Jesus Christ wished to bestow on all those who through him were born again into one body, and with him quickened to newness of life—that unity that Holy Scripture and the ancient Tradition of the Church proclaim," nonetheless "large numbers have felt the impulse of this grace

On November 19, 1963, Archbishop Elchinger of Strasbourg delivered a speech that silenced the great Basilica of St. Peter. He asserted that "now the time has come to recognize with greater respect that there is also a partial truth" in the doctrines "taught by our separated brethren."
 
Well Mshara umetoa elimu nzuri sana kwa hawa viongozi wa makanisa. Jambo moja huwa natafakari msingi wa haya makanisa ni nini? Mi naona kuna shida ya kiroho ambazo zimetawala kuna unclean spirit zinatakontrol haya makanisa .Unakuta mwanzilishi wa kanisa alikuwa anahudumu kanisa flani wakatofautiana (hapa tusitake kujua msingi wa tofauti zao)na kiongozi mwingine roho ya uasi(rebellion) inamuingia anaondoka anaanzisha kanisa lake. Kumbuka hata akiondoka atatafuta watu wake wa kuondoka nao sasa asimame madhabahuni sasa majigambo yakutosha too much controlling anaona waumni kama ni mali yake , ataka kunyenyekewa mpk kuna wakati unajiuliza hawa ni kwamba wameamua kuwa mateka wa mtu .

Ndugu zangu wakristo wenzangu tusome biblia tutafute maarifa, na roho wa Mungu hatakuacha upotee ukimuweka Mungu mbele

Waubiri wengi wanatumia matatizo ya waumini kama mtaji kwao.Ni kwa uweza wa Mungu tu tunaweza kunusurika na haya.
 
Haya chini ni maelezo niliyochopoa kutoka tovuti ya Catholic Answers.

Catechism of the Catholic Church states, "the word ‘Church’ (Latin ecclesia, from the Greek ek-ka-lein, to ‘call out of’) means a convocation or an assembly" (CCC 751).

Naona maana ya kanisa kwa tafsiri yao haijatofautiana maana kibiblia lakini naona kama umepokea isivyo sawa maana ya kanisa....

Kanisa ni nini? siyo jengo bali ni wale waliomo ndani yake. Imo katika Biblia, Matendo ya mitume 17:24 "Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo yeye kwa kuwa ni Bwana wa bingu na nchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono."

Kanisa ni watu wanao amini Imeandikwa wefeso 2:21 "Katika yeye jingo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika bwana." 1Wakorintho 3:16 "Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu na yakuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?.

Kazi ya kanisa ni ipi? Kanisa inaeneza ijili Imeandikwa 2 Timotheo 4:2 "Lihubiri neno uwe tayari wakati ufaao na wakati usiokufaa karipia kemea na kuonya kwa uvumilivu wote na mafundisho."

Kanisa limepewa maagizo na Mungu. Imeandikwa katika Waefeso 4:12 "Kwa kusudi kuwakamilisha watakatifu hata kazi ya huduma itendeke hata mwili wa Kristo ujengwe."

Kila mshiriki ana jukumu maalum. Imeandikwa katika 1 Wakorintho 12:13, "Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja kwamba tu wayahudi au kwamba tu wayunani ikawa tu watumwa au ukawa tu huru nasi tulinyweshwa Roho mmoja."

Wakristo tu wafariji wenzetu Imeandikwa Waebrania 10:25 "Wala tusiache kukusanyika pamoja kama ilivyo desturi ya wengine; bali tuonyane na kuzidi kufanya hivyo kwa kadiri muonavyo siku ile kuwa inakaribia.
 
Mimi hapa jirani kulikua na bar, enzi zake ilitikisa, baada ya kujengwa bar nyingi na za hali ya juu hii ilipoteza wateja kabisa wakaweka na kiti moto lakini ikawa bure sasa hapa juzi tu nashangaa napita pale nakuta imegeuzwa kanisa. na zamani palikua na ufuska wa ajabu. it's so sad...!!!
 
Labda tungeeanza na tafsiri ya " kanisa la kiroho ni lipi?"
Tukishajua hilo nafikiri mada itakuwa simple kuijadili.
 
Mleta mada acha uvivu Fanya kazi kwa hiyo anataka serikali au kanisa likulishe? Karina waumini ambao wanatakiwa kuhubiriwa umuhimu wa kufanya kazi ni walokole wengi wavivu Na wapenda dezo.Mpendwa nyingi mdomoni uchapa kazi sifuri.Mleta mada naona Na wewe ni mmojawapo.
 
Unamaanisha nini kusema makanisa ya watu binafsi halafu ukayaita ya kiroho? kuna makanisa kama TAG, EAGT na mengineyo yasiyo ya watu binafsi na ni ya kiroho. Ungechora mstari kwenye hilo kwanza.
 
Ingawa pia sina hakika kama umefanya uchunguzi wa kina kujua kama haya maknisa ya kiroho hayatoi huduma ya kijamii. Mimi najua yanatoa sana katika level yao ya kiuchumi.Primary purpose ya makanisa ya kiroho kikwelii ni kupeleka injili hivyo bajeti kubwa sana inaelekezwa huko. Na ukifuatilia huduma nyingi zinazofanyika hasa vijijini na maeneo yasiyofikiwa huwa huduma za kijamii zinatolewa.
 
Back
Top Bottom