Hamis Chaurembo: Dereva mjinga aliyeuwa abiria kwa mwendokasi Kigoma

Miaka ya 2000 Mwanzoni, Urambo Tabora, kuna jamaa alikuwa akiendesha gari ya Halmashauri, mkonga. Alikuwa na mwendo usio wa kawaida. Alikuwa akisema siku mkisikia nimepata ajali, basi mtenge tu msiba.

Na kweli, ajali iliyomkuta, humtazami mara mbili. Alikua akiitwa Chonza kama sijamsahau jina.

Kuna wengine ni wagonjwa wa akili na wana leseni za udereva.
Kujinenea ni vibaya
 
Asilimia kubwa ya abiria nao huwa wapumbavu, hupenda mwendokasi hata kama hakuna wanachokiwahi. Unakuta wanafurahia, wanamsifia na kumshangilia dereva anayewapeleka mwendokasi.

Sababu kuu ya mabasi ya Ally's na Katalama (dar- mza) kupendwa na abiria na kujaa mapema ni mwendokasi. Juzikati nipo Mza naona Katalama ikiingia saa moja na nusu inashangiliwa sana kwenye ile mitaa ya Buhongwa, Mkolani hadi inaingia Nyegezi stand! Niliwahi sikia kuna watu wanabet katika mchuano wa mabasi ya kampuni hizi mbili, na madereva hujua kabisa kuwa wanatakiwa kushughulika kwelikweli kuhakikisha mikeka ya waliowaamini inatick!

Mimi nikisikia tu hayo majina ya aka ya ajabu ajabu kama simba, ndege ya ardhini, sijui rocket, hata hilo gari sihitaji hata kuliona. Kuna kipindi nilighairi safari na sikurudishiwa hata mia baada ya kugundua gari ile ni special kwa wenye haraka zao.

Wanasema ajali haina kinga, lakini kwa kiasi kikubwa mwanadamu ana uwezo wa kupunguza au kuongeza uwezekano wa ajali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
3-6 hours
Mkuu..wewe uko Kibondo kweli???yaani Kibondo to Kakonko utumie masaa matatu??unatumia baiskeli au nini??
Mimi nipo Kasulu,huwa napita njia hiyo nikielekea Mwanza,Kibondo to Kakonko nilikuwa natembea nusu saa kipindi kile hata Lami hakuna!
 
Sipo huko mkuu mbona nimesema nimeweka kama ilivyo
 
Miaka ya 2000 Mwanzoni, Urambo Tabora, kuna jamaa alikuwa akiendesha gari ya Halmashauri, mkonga. Alikuwa na mwendo usio wa kawaida. Alikuwa akisema siku mkisikia nimepata ajali, basi mtenge tu msiba.

Na kweli, ajali iliyomkuta, humtazami mara mbili. Alikua akiitwa Chonza kama sijamsahau jina.

Kuna wengine ni wagonjwa wa akili na wana leseni za udereva.
Na maneno pia yana nguvu! Anachokiongea mtu mara kwa mara huishia kuratibu yatakayotokea maishani mwake.
 
Mimi nikiwa kwenye gari zinazoendeshwa na madereva kama hawa napiga kelele kweli kweli. Mara kadhaa nimegombana na madereva wa aina hii na kuna siku nimeshuka na kusubiri gari nyingine.
Bora kufika kwa kuchelewa kuliko kuwahi na kuishia njiani.
 
Back
Top Bottom