Uchovu wa abiria kwenye basi la mwendokasi

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
1,976
3,124
Safari yetu ni ya takribani kilomita 2015 na 2025 hivi, ni asubuhi na mapema tupo ndani ya basi la kampuni ya "chapa kazi express" abiria tuliomo ndani ya basi ni 45 japo abiria wengine wanaweza ongezeka kwenye vituo vya mbele. Mara anaingia mtu mmjo wa kiume akiwa ameongozana na mwanamama mmoja, huyu wa kiume anajitambulisha kuwa yeye anaitwa Musa na anamtambulisha huyu mwingine kwa jina la Salimia (kwa utani abiria mmoja anasikika "huyo salimia ndo ile dawa ya kuchua ya kupunguza maumivu?"). Musa anasema katika safari yetu ya leo yeye ndiye dereva mkuu hivyo yatupasa tumsikilize kwa makini anachotaka tuzingatie kwenye safari yetu.

Anaanza kwa kutueleza kuwa safari yetu itaanza saa kumi na mbili kamili, dk 15 toka sasa, anaendelea kuwa jambo la Kwanza ambalo kila abiria yapasa azingatie ni usalama ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kila abiria anafunga mkanda, pia kila abiria yampasa kumuomba mungu wake wakati wa safari ili tuweze kufika salama kwani mungu ndiye ajuaye mwisho wa kila mwanadamu, anaendelea kwa kumtaka abiria mmoja wetu ainuke na kufanya dua ya pamoja huku akisisitiza sana yeye kama dereva kuombewa wakati wote kwani kila ajali inasababu.

Pia anaeleza kuwa gari yetu itapita maeneo kadha wa kadha na tutapata kushuhudia uzuri wa miji mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuona maziwa na asali viuzwavyo kwenye baadhi ya maeneo, vile vile anatueleza kuwa basi litasimama kwenye hoteli mbili kwa ajili ya chai na chakula cha mchana lakini anasisitiza kuwa watoto wadogo watagharamiwa hitaji hilo na kampuni kwani nauli walipayo watu wazima yatosha kufanya hivyo.

Baada ya dk 15 safari yetu inaanza, dereva anaonekana kuwa na umakini mkubwa kiasi kwamba mapema ameweza kubaini kuwa matairi mawili "moja la mbele kushoto na lingine la nyuma kulia" yana matatizo kwani hayaonyeshi ushirikiano hivyo anaamulu makondakta wayabadili haraka sana, anasimulia kuwa kwa uzoefu wake matairi ya china si imara na ni bora nchi yetu ingepiga marufuku uagizaji wa matairi hayo na ingejenga viwanda vingi ili kutengeneza matairi hayo hapa nchini pamoja na bidhaa nyingine. Abiria wengi wanaonyesha kufurahishwa na wazo hili huku wakisema kuwa hii ingeongeza ajira na uchumi wa nchi kukua, abiria mmoja aliyeketi kiti namba 43 anasema "hata wanangu wawili walio maliza chuo kikuu wangepata ajira".

Baada ya kubadili tairi safari inaanza tena, mara hii wanainuka vijana wawili ambao ni wahudumu ndani ya basi wakitangaza kuwa kila abiria lazima awe na tiketi iliyo halali, dereva anaongeza kuwa kama kuna abiria atakuwa hana tiketi ni lazima ashushwe kabla, kila abiria anonekana kutafuta tiketi yake huku wengine wakiwa hawakupewa tiketi na mawakala wa kampuni, wengine tiketi zimepotea na wengine wameweka kwenye mabegi yao yaliyo kwenye buti, bahati nzuri binafsi naiona tiketi yangu na kauli mbiu ya kampuni imeandikwa mwishoni mwa tiketi "vuja jasho ule", abiria wote walioshindwa kuonyesha tiketi zao na wale walioonyesha lakini si tiketi halali wameamuliwa ama kushuka wenyewe ndani ya basi ama watapelekwa kituo cha polisi kwa hatua za kisheria.

Ni takribani kilomita mia tangu safari ianze, dereva sasa anaendesha kwa mwendo kasi sana, abiria mmoja aliyeketi kiti cha nyuma anapiga kelele kuomba kupunguza mwendo, dereva yu mkali sana sana, anasema yeye ni dereva mahili sana wala hawezi kujaribiwa wala kutishwa na kelele hizo, abiria wengine wanashangilia na kusema hii ni gari ya mwendo kasi sio kama gari zingine kama ile tulipanda jana "anaizungumzia gari ya kampuni ya mwafrika " abiria mwingine anahoji lakini hii si ni kinyume na sheria za nchi kuendesha gari kwa mwendo kasi? Abiria mmoja anajibu "bora kuvunja sheria ili tufike mapema hayo mambo ndo yalifanya jana gari ya mwafrika ichelewe kufika". Dereva anaongeza "kondakta huyo abiria mshughulikie haraka".

Hadi sasa kwa umbali wa takribani kilomita mia abiria wengi wamechoka sababu ya mwendokasi na barabara ina mashimo, kona kali na miteremko, wengine wanalalamika kizunguzungu, wengine kichefuchefu na wengine wameanza kutapika japo wengine wanaonyesha kushangilia, binafsi natamani safari iishe haraka japo umbali bado mrefu sana, abiria mwenzangu anasema angejua angekata tiketi ya basi jingine.

Tunaomba mungu tufike salama na hatujaacha kumuombea dereva wetu pengine abadili mawazo yake awasikilize abiria wake.
 
Dereva wa hilo gari nahisi kama hajatoka mbinguni basi atakua ni miongoni mwa malaika watukufu kabisa tena walio daraja la juu la utukufu. Nawaza tu kulingana na adha za hiyo safari yenu.
 
Tatizo abiria nao wakati mwingine ni wasumbufu, mara atake kununua nyanya mara mkaa, sina uhakika kama kwa mwendo huo mtafika salama ila ni bora kujaribu.
 
Ubunifu wako ni mzuri lakini jitahidi kuongeza ubunifu zaidi katika fasihi ili kuongeza ladha fulani ya uwasilishaji wa ujumbe.
 
Tatizo humu humu kuna watu wako siti ya nyuma, wanaumwa matumbo ya kuharisha wanalalamika speed ikiendelea kuwa hiihii watajiny*a.

Huku wengine tunatamani gari ipae kabisa ikiwezekana.
 
Back
Top Bottom