Hamad Rashid: Zitto ataondoka na wengi!

Hamad Rashid: Zitto ataondoka na wengi!

Tatizo la Chadema mna wafuasi sio wanachama. Anayebisha alete hesabu ya wanachama wa Chadema kitaifa. Na wapiga debe hawajengi chama kinajengwa na wanachama.

Ngedere wewe kwani ccm yako ina wanachama wangapi?zaidi ya mateja na wauza mandazi mliokuwa mnawaonga pilau ,kanga na t-shirts na sasa wameshtuka sijui mtatafuta akina nani sasa hivi.
 
hivi mtu mshamba kutoka buzebazeba ndio tumkome sisi ? kama kweli katamka maneno haya basi hastahili huruma hata kidogo .
 
Msiba ni wa CDM lakini wanaolia na kujigaragaza ni CCM. Kweli Zitto alikuwa pandikizi la CCM ndani ya CDM.-HONALULU
 
haya ni maneno tu, hata kwenye kanga yapo. CCM watamtumia sana kisha watamtupa kama kondomu. ukiona mwanaUKAWA anasifiwa na maCCM ujue kuna walakini.
 
Napata shida kuamini habari hii kama kweli alisema hivyo au la, kuna hoja ya Hamad hapo pia anyway siingizi siasa ila uwa ninaamina sana habarizinazoandikwa na mwananchi na kampuni nzima ya mwananchi kwa maana ya magazeti mengine ya kampuni hii na kwa kweli nimejiridhisha kuwa haliko biased kama mengi yalivyo hivyo kuwa na weledi mkubwa kwenye habari, kwa gazeti hili lililobeba hoja hii cjui mmiliki wake ni nani kwanza mana mmiliki ana determine aina ya habari, uzito na ukweli wake, magazeti yanayomilikiwa na viongozi wa vyama yako biased kwa vyama na itikadi ya vyama husika, vivo hivyo yale ya dini yako biased na dini zao but Mwananchi\citizen wako neutral sana kwenye habari.

Nkirudi kwenye hoja kwa kutakuwa na effect au la kwa Upande mwingine ni ukweli kutakuwa na athari kiasi fulani sababu Zitto ana wafuasi wake hivyo watamfuata na wengine wameshatangulia kama wengi tunavyojadili kwenye jamvi humu, kwenye uongozi uwa lazima kufanya maamuzi ila vizuri kupima ukubwa wa risk ( risk assessment ) ya maamuzi hayo then unachagua kati ya kukaa na hiyo risk au kufanya maamuzi na kulipa gharama za hiyo risk ambayo inatakiwa iwe ndogo kuliko gharama za kukaa nayo, ni matumaini yangu CHADEMA walipima ukubwa wa risk ( risk assessment ) ya kumfukuza au kumwacha ZItto abaki kwenye chama na hivyo watakabiliana na changamoto zitakazojitokeza na kama hawakufanya hivyo then CDM itayumba mana hawakujiandaa kwa hilo.

Nimemskiliza Prof Baregu sku moja nkaskia anamshauri Zitto aombe msamahaa ili akubaliwe kurudi na aendelee na chama na kwa ninavyomuheshimu huyu mzee nkaisi CDM ilishapima risk ya maamuzi haya na kujipanga zidi ya changamoto zitakazotokana na uamuzi huu.

Zitto ni mwanasiasa so matalajio ya wengi ni kwamba atafanya siasa kwenye chama kimojawapo na kama ataamua kujiunga na chama kipya, itachukua muda kukifanya kijulikane kwa wananchi cuz kuna sehemu tayari hivi vyama vimekita mizizi sana hivyo chama kipya kinatakiwa kufanya kazi ya ziada kupenya.
 
DSC005731.jpg




Hiyo ni kauli ya Zitto ambapo gazeti limeripoti akisema watamkoma na huku Hamad Rashid akisema ataondoka na wengi.

Kichwa cha habari katika gazeti kinasomeka:
"Zitto:Watanikoma"

CHANZO:Jamboleo

My take;
Kama kweli hayo ndio matamshi ya Zitto,basi huyu dogo ni very arrogant na hapaswi kuhurumiwa hata kidogo.

anapata kiburi na mamilioni aliyoingiziwa kwenye account ya ujerumani
 
Mkondakaiye wala usidhani Zitto anapendwa na watu wengi wa Mwandiga. CHADEMA imekuwa na nguvu kubwa Kigoma kabla hata Zitto hajawa Mbunge au Kiongozi wa CHADEMA. Kuna watu wengi sana walihusika kuijenga CHADEMA kigoma kabla ya Zitto kuwa mbunge.

Kifupi tambua tu, siasa za ajabu ajabu za Zitto akiwa mbunge na kiongozi mwandamizi wa CHADEMA zimehusika sana kuirudisha nyuma CHADEMA Kigoma.

Mkuu hilo nikweli kabisa,Siasa uchwara za Zitto kwa mkoa wa Kigoma zimeiludisha nyuma Cdm badala ya kuijenga.Nakwa ushahidi kujua kwamba watu wa Kigoma wanaipenda Cdm ngoja nijaribu kuweka video ya mkutano wa mh Mbowe siku anampa Zitto na Kabourou makavu laivu bila chenga
 
Last edited by a moderator:
Hamad Rashid amefeli kabisa kabisa akienda kule jimboni kwake ata kushuka kwenye gari kusalimia watu ni shida, ni mnnafiki mnaffiki kila mahali na Zaidi alivyokuja kuiunga mkono katiba mpya ya ccm
 
Don't say that, CHADEMA was already facing a political hemorrhage,if not UKAWA we would have been saying different things right now. Sometimes you have to accept the reality, live with it and move on instead of being so adamant against the reality, you might end up losing.

I hate people like you. Your colleague wrote in Swahili language, then wonderful enough (I know not why?) you reply in English. No fair my friend. It's not a challenge to you but a reality bearing in mind that Swahili is your official language in TZ.
 
Siku zote naamini kuwa unapokuwa msaliti basi huwezi kuwa na mwisho mzuri. Na utaandamwa na mikosi tu ktk maisha. Na waliokudanganya kuwa msaliti watakuwa wanakucheka nakukudhihaki ukiwa haupo nao. Pia hawawezi kukuamini kabisa kwakua umrahisi kushawishika. Hata kama ni system inakutumia basi ni kwa manufaa yake tu na itakuwa inakuangalia kwa jicho la tatu.
 
hamad rashid ni lazima atamke hayo kutafuta huruma ya CUF /USHAURI WANHU KWA CUF FUKUZENI HUYO NI MSALITI WENU
 
Christiano Ronaldo alivyoondoka Man U pamoja na kupendwa sana hakuondoka na yeyote
 
I hate people like you. Your colleague wrote in Swahili language, then wonderful enough (I know not why?) you reply in English. No fair my friend. It's not a challenge to you but a reality bearing in mind that Swahili is your official language in TZ.

The same with what you did
 
Mfa Maji Haachi Kutapatapa, Is too late, Mbona alifukuzwa Siku Nyingi na hakuna Impact yoyote ambayo CHADEMA imefeel. Kashachelewa Labda atawapata watu wa Jimboni mwake; Watanzania Kwa Sasa Tunaongelea Kuwapa DOLA UKAWA na sio CHADEMA.

Kufutiwa/Kufukuzwa Uanachama ni Jambo ambalo si geni kwa Siasa za Tanzania, Tumewaona wanasiasa wengi tu katika hili. Sidhani Zitto yeye anaweza Kutushangaza sana WaTZ Kiasi cha Kutubadili Mwelekeo Tulionao.

Yeye aende aendako hata CCM walikokuwa Wanapeleka Taarifa lakini Mwisho wa Siku UKAWA Ndio habari ya Mjini.

Kuuliza sio ujinga hivi huyo hamadi rashid alikuwaga chama gani?
 
Back
Top Bottom