Hamad Rashid, Dk. Slaa waunga mkono mgomo wa wafanyakazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamad Rashid, Dk. Slaa waunga mkono mgomo wa wafanyakazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, Mar 21, 2010.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wasema serikali imejitakia yenyewe
  [​IMG] Kapuya alipoulizwa akadai `nipo majuu`

  [​IMG]
  Hamad Rashid, kiongozi wa upinzani bungeni,Dk. Wilbroad Slaa, Mbunge wa Karatu (katikati)na Waziri wa kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana Prof. Juma Kapuya.  Wakati serikali ikihaha kujaribu kuzuia mgomo ulioitishwa na Shirikisho la Wafanyakazi nchini (TUCTA), baadhi ya wanasiasa wa vyama vya upinzani wameibuka na kuisuta kuwa imejitakia yenyewe na kuishauri kuwa njia pekee ya kujinasua ni kutekeleza madai wafanyakazi.
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jana kuhusiana na tishio hilo la mgomo, wanasiasa hao wamesema wanaunga mkono mgomo huo, kwa kile walichodai kuwa wafanyakazi wanatekeleza haki yao ya kikatiba baada ya kuona kuwa kwa muda mrefu sasa serikali imekuwa ikipuuza malalamiko yao.
  Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni (CUF), Hamad Rashid, alisema serikali imejitakia yenyewe kuingia katika mgogoro na wafanyakazi, kutokana na hatua yake kutosikiliza na kutekeleza madai yao ambayo wamekuwa wakiyatoa mara kwa mara.
  Alisema serikali imeshindwa kufuata taratibu na sheria za utumishi katika kushughulikia masuala ya wafanyakazi na matokeo yake wafanyakazi wameona njia pekee ya kudai haki yao ni kupitia migomo.
  "Tatizo ni serikali haifuati taratibu na sheria za utumishi, haya mambo ya yakusubiri mpaka mambo ya haribike ndiyo kulazimisha vikao vya maridhiano ni utaratibu mbaya, taratibu na sheria za utumishi zipo kila siku kinachotakiwa ni serikali kuzifuata na si kusubiri vikao" alisema.
  Alisema ugoigoi wa serikali katika kushughulikia masuala mbalimbali unawajengea tabia wanachi kuwa matatizo yao hayawezi kushughulikiwa mpaka kwa migomo, akitolea mfano mgomo wa walimu na wafanyakazi wa kampuni ya reli nchini TRL.
  "Serikali imewafanya wananchi waone kuwa matatizo yao hayawezi kushughulikiwa mpaka kwa migomo, ona walimu walianza kulipwa madai yao baada ya migomo, halikadhalika wafanyakazi wa TRL ni hadi pale walipoanza migomo. Swali la kujiuliza ni kwanini wanagoma?.... ni kwa sababu madai yao hayasikilizwi na hii ni mbaya sana", alisema kiongozi huyo wa upinzani bungeni.
  Hamad Rashid alitoa ushauri kwa serikali kuwa ifanye haraka kukaa meza moja na wafanyakazi ili kujadiliana nao na kisha kutekeleza malalamiko yao kwani endapo mgomo utafanyika kutaleta athari kubwa kwa taifa na wananchi.
  Alisema endapo serikali itaendelea kupiga danadana malalamiko ya wafanyakazi, ipo hatari ya kundi la wafanyakazi kuondoa kabisa imani na taasisi zinazoshughulikia masuala yao ikiwemo serikali yenyewe.
  Aliongeza kusema kuwa endapo mgomo huo utafanyika, pia utakuwa na athari kubwa kwa uchumi wa nchi kwani shughuli nyingi za maendeleo na huduma zitasimama.
  "Mgomo huo pia utawatisha wawekezaji wa nje kuwekeza nchini, kwani wengi wao hupendelea kuwekeza kwenye nchi ambazo hazina migomo" alisema.
  Alisema anaunga mkono mgomo huo endapo umefuata taratibu zote zinazotakiwa.
  Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, alisema anaunga mkono moja kwa moja mgomo huo, kwani ni haki ya msingi ya wafanyakazi pale wanapohisi kutotendewa haki.
  Aliilaumu serikali kuwa haipo makini katika kushughulikia masuala ya wafanyakazi na kwamba mgomo ndiyo njia pekee ya wafanyakazi kufikisha kilio chao kwa wahusika. Dk. Slaa, alisema wafanyakazi kwa muda mrefu wamekuwa wakitoa malalamiko yao bila ya kushughulikiwa na kuongeza kuwa hata yeye mwenyewe amekuwa akilipigia kelele suala hilo mara kwa mara lakini serikali imekuwa haisikilizi.
  "Nimepiga kelele siku nyingi, bungeni nimezungumza sana na hata kutahadharisha kuwa suala hili litatela matatizo lakini hakuna anayejali, kwa hiyo njia pekee ya kidemokrasia sasa ni mgomo", alisema Dk. Slaa, ambaye pia ni Mbunge wa Karatu na Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni. Alisema katika bajeti ya mfano iliyopendekezwa na kambi ya upinzani bungeni, walipendekeza kuwa kutokana na kupanda kwa hali ya maisha kima cha chini cha mshahara kiwe Sh 315,000 kwa mwezi lakini serikali ikapuuza.
  "Nilionya kuwa tofauti kubwa ya mishahara itajenga matabaka hakuna aliyejali, sasa kwa wakati wa sasa hata hiyo 315, 000 tuliyopendekeza haitoshi tena, maisha yamepanda sana.
  Hili ni fundisho kuwa serikali kuwa ikipata notisi za migomo inatakiwa kuchukua hatua za haraka badala ya kutoa visingizo kuwa hadi hali ya uchumi itakapokuwa nzuri ", aliongeza kusema.
  TUCTA imeitisha mgomo wa wafanyakazi nchini nzima kuanzia Mei Mosi mwaka huu, wakishinikiza serikali itekeleze madai yao mbalimbali ikiwemo nyongeza ya mishahara na kupunguziwa kodi kwenye mishahara.
  Kufuatia tishio hilo, juzi Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kuwaomba wafanyakazi wasitishe mgomo huo na badala yake warejee kwenye meza ya majadiliano.
  Hata hivyo, pamoja na ombi hilo la waziri, TUCTA imeendelea na msimamo wake wa kuendelea na mgomo huo, kwa kile inachoeleza kuwa tayari yameshafanyika mazungumzo mengi lakini serikali imeshindwa kutekeleza.
  Profesa Kapuya alipotafutwa kwa njia ya simu na gazeti hili jana ili aweze kueleza msimamo wa serikali baada ya TUCTA kukataa ombi lake, alisema yupo nje ya nchi.
  "Nipo nje ya nchi siwezi kuongea simu yangu haina dola ya kutosha", alisema Profesa Kapuya.
  Alipoelezwa kuwa mwandishi wa habari hii ndiye aliyepiga simu hivyo asiwe na wasiwasi wa kuishiwa na muda wa maongezi, alisisitiza msimamo wake na kukataa kuendelea kuzungumza.
  "Huku hata ukipiga wewe na mimi nakatwa nisamehe sana sitaweza kuzungumza", alisema waziri huyo.
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
  MAoni yangu: serikali itafute ufumbuzi na sio vitisho kwa wafanya kazi kwani ufanisi utapungua. Waziri ni Muongo angalia red highlighted, iweje ukipokea simu ukatwe fedha, nijulisheni jamani.
   
 2. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ana ROAM. Halafu ki credit sio DOLA, Prof Kapuya nae...........
   
 3. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Mh. Kapuya sio mwongo ila Mwandishi wa habari ndio hajui haya masuala ya Roaming yamekaaje, inawezekana hajawahi kusafiri nje au kama amesafiri hakuwahi kutumia huduma ya simu ya hapo nyumbani (pre-paid) akiwa kwenye roaming service. Ni kweli unapokuwa nje ya nchi na mtu anakupigia simu kwenye line yako ya VODA au ZAIN unapopokea unakuwa na wewe unakatwa pesa kwa ajili ya kupokea hiyo simu. Kama huna pesa kwenye simu yako huwezi kuongea wala kupokea simu. Alichotakiwa mwandishi kufanya ni kumpa Kapuya namba yake (yeye mwandishi) ili kapuya atafute namba ya simu ya hapo alipofikia (naamini chumba cha waziri kina simu ) alafu mwandishi ampigie tena.
   
 4. R

  Rafikikabisa JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Waziri tumutendee haki kuhusu simu yake kutokuwa na pesa za kutosha yuko sawa hapa. "Roaming" http://www.wirelessguide.org/plan/roaming.htm
   
 5. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #5
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Lakini issue ni Je waziri anaruhusiwa kuwa na kiasi gani cha pesa kwenye simu yake? au ndio yale mambo ya kusema anaogopa kuwa ataoneka fisadi kama ataweka vocha za kutosha kwenye simu? Lakini navyojua mimi wadau wakubwa kama mawaziri wapo kwenye post paid, yaani wanalipa baada ya matumizi. Wanapewa huduma hiyo kutoka na uagency wa shughuri zao. Sasa Mh. Minister inakuwaje anakuwa kwenye huduma ya Pre-paid???? ni utaratibu wa kawaida huu kwa mawaziri wetu???
   
 6. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2010
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  sasa akipeleka hiyo bill matumizi ya simu ni millioni si mtamugeuka tena na kumwita fisadi. Ama hatutageuka??
   
 7. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #7
  Mar 21, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Dr Slaa na Hamad wasiishie tu kuunga mkono kwa maneno mgomo huu,natamani wachukue hatua zaidi za kivitendo.
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Mar 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,382
  Trophy Points: 280
  watu wamebakia kuzungumzia matumizi ya simu!
   
 9. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #9
  Mar 22, 2010
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Msharika,

  Wewe na mwandishi wa habari naona mmefungwa goli na technologia ya jinsi call transnfer inavyofanya kazi kwenye simu.

  Roaming ni aina mpya ya call transfer. Idea behind ni kwamba mtu anapokupigia simu huwa hajui uko wapi, assumption yake ni kwamba uko mahali kwako kwa mfano TZ. Hivyo kama wewe kwa njia moja ama nyingine umeamua ku transfer simu yako kwenda mahali pengine au unatumia roaming, basi wewe ndio uko responsible na malipo ya hii sehemu ya pili. Hiyo call moja inakuwa charged twice.

  Hivyo kwa roaming, anayepiga kwa mfano kama ni TZ analipia amount ile ile kama ambavyo angelipa mpigiwa ungekuwa hapo hapo TZ. Gharama ya kutokea TZ kwenda aliko kwa mfano USA ni ya mpigiwa simu, hivyo kwa case hii ni ya waziri Kapuya.

  Hivyo hivyo hata ukiweka call transfer kwenye simu ya nyumbani kutoka namba moja kwenda nyingine, for billing purposes hiyo call inagawanywa katika sehemu mbili. Sehemu ya kwanza inakuwa ile ya kawaida na mpigaji ndio analipa. Sehemu ya pili inakuwa kutoka kwenye namba iliyopigwa kwenda namba ya pili na wewe mwenye namba uliyopigiwa ndio unalipia.

  Inasikitisha kuona hilo gazeti mpaka limechapishwa bila mhariri kuona hiyo habari sio sahihi.
   
 10. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #10
  Mar 22, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ..As MKijiji has dully noted...was this about Roaming Calls??
   
 11. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Anyway, We hope this time Wafanyakazi watafanya kweli badala ya kuishia kushikana mikono na kuimba 'hakuna tunachopoteza zaidi ya minyororo yetu'! Huko nyuma Viongozi wa wafanyakazi wameishatoa 'tisha toto' nyingi tu za kugoma lakini zikaishia kuyeyuka walipolambishwa pipi ama kutishwa kidogo tu. mabadiliko na mapinduzi mengi duniani yalianzia kwa wafanyakazi. If only we had our own Lech Walesa or even Chiluba (When he was still a good boy!!)...!
   
 12. m

  miner Member

  #12
  Mar 22, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo hapa si mazungumzo ya waziri na mwandishi na simu zao. Suala hapa la msigi jee hatua wanayotaka kuchukua wafanyakazi ni sahihi ? Unawaunga mkono ? Dr. Slaa na Hamad kuelezea hisia zao gazetini zinatosha ? Tujadili hayo na nini kifanyike badala ya Kapuya na mwandishi. Ninatamani wafanyakazi kutekeleza azma yao itabadili tabia ya ujeuri wa viongozi wetu, wafanyakazi wote duniani wametumia silaha hiyo kushinikiza haki zao kupatikana lakini Watanzania wanaweza ? Nilidhani waalimu wangeweza wakagawanyika na hawa pia wapo ambao wataenda kazini umoja na mshikamano ni wimbo tu.
   
Loading...