Mbona mna majawabu mengi ,hivi kuna kitu mnaogopa ?
Iwe kuolewa kuoa huo ni utoto but the message is clear anatapatapa hana msimamo simple.Kwahiyo cdm iko tayari kuolewa na mume aliye fukuza mke wake wa kwanza? duh really amazing
Sure, ikiwa kila siku yeye ni kuitisha waandishi na kuzungumzia hilohilo haoni kuwa anazidi kuwachefua CDM.Huyu HR ni wakuogopa kama ukomo. Mbona katika bunge lililopita mwanzoni CUF iliunda kambi ya upinzani yenyewe tu bila ya kushirikisha chama chochote. Hivi sasa nini kimebadilika? Kwa mwenendo huu, hata kama chadema ilikua na nia ya kushirikisha vyama vingine kwenye kambi yake, ni vema kikasubiri kwanza, uenda yakajitokeza mengi.
Kwa nini wasilazimishe CCM iwateue mawaziri toka CUF??
kweli kwanini walijifanya wasaliti kipindi cha kuchagua spika? sizitaki mbivu hiziHuo umoja ungeanzia kwenye kuchagua spika na naibu wake ningeona kweli wana dhamira ya kweli
Wewe umeachika?Wanataka kuwaoa chadema si kuolewa
Mume ndio hupeleka posa upo!
jamani kamabi ya upinzani ina marupurupu si haba. vikao kila siku, posho mbilimbli na hata tatutatu kila siku na kiongozi wake anatunzwa na serikali kama waziri. kila kikao cha kamati ya uongozi ya bunge anahudhuria, katika kikao cha kupanga shughuli za kila siku za bunge anahudhuri ana posho anatia kibindoni, ukichanganya na posho ya kikao chenyewe cha bunge na kamati zake, utajua hamadi anasumbuliwa na ugonjwa gani. mnadhai hata zito alipolilia cheo kile alikuwa mjinga? hamadi anakumbuka mbali jamani msameheni!
Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ndiye waziri mkuu kivuli, hivyo anapata
Ofisi pale bungeni Dodoma yenye wafanyakazi 4 na ofisi ndogo Dar es Salaam yenye wafanyakazi 2
Nyumba ya serikali pale Dodoma yenye watumishi wawili na ulinzi 24/7
Gari la serikali lenye hadhi, na dereva/bodyguard, mafuta kumwezesha kuzunguka nchi nzima.
Posho kama ya Waziri Mkuu.
Ndiye mtu wa kwanza kuulizwa swali kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo.
Kipaumbele kwenye safari za nje
etc etc
Sasa yote haya uyakose!, hata ningekuwa mimi, ningeomba kanuni zibadilishwe na kupata japo nusu ya marupurupu haya!
kumbe ndiyo maana mpemba amechanganyikiwa! CDM wasikubali kuungana naye mpaka amewaomba msamaha hadharani.