Bunge la 2000 hadi 2005 CUF waliwashirikisha Chadema kwenye kambi ya Upinzani! Sasa hapa nani mrafi wa madaraka kama sio Mbowe na Chadema? Maskini akipata makalio hulia Mbwata!
Huyu mtu ni mrafi na ana uchu wa madaraka. Ni mwepesi wa kusahau. Tukiachilia mbali mambo mabaya waliyoyafanya cuf miaka hiyo zaidi ya 10, lakini ni hivi majuzi tu kuanzia kipindi cha kampeni cuf walifanya mambo mabaya sana ya kuidhoofisha chadema. Machache ninayoyakumbuka kwa haraka ni haya:
1. Wakishirikiana na ccm na nccr, cuf walipandikiza chuki kwa wananchi dhidi ya chadema kuhusu udini na ukabila.
2. Waliisema vibaya sana chadema
3. Waliipigia kampeni ccm
4. Walitaka wananchi wasiichague chadema
5. Waliwazomea wabunge wa chadema waliposusia hotuba ya mkwere kwenye kikao cha kwanza cha bunge, zaidi ya yote hayo waliwaponda vibaya sana chadema.
6. Wakati wa mdahalo kuhusu kambi ya upinzani, cuf waliendelea na propaganda zao dhidi ya chadema
-Kutokana na hayo yote, mtu unabaki unajiuliza: Huu urafiki unaolazimishwa ghafla unatokea wapi?
-Wakati wanafanya huo uzandiki wao, cuf hawakujua kuwa itatokea siku watahitaji kuungana na cdm?
-Au walidhani wataendelea kuwa wao pekee ndio wenye dhamana ya kujenga kambi ya upinzani.
-Kwa bahati mbaya wanalazimisha sasa kuungana baada ya jaribio lao la kuunda kambi ndogo ya upinzani kukwama.
Mi nasema kama wana nia nzuri na taifa si lazima kuwemo kwenye hiyo kambi. Wao tayari ni wapinzani. Kutoa hoja au kutetea taifa si lazima uwe kwenye kambi. Wakati wanaomba kura hawakuahidi kutekeleza ahadi zao wakiwa kwenye kambi. Sasa huo umuhimu wa kambi unatokea wapi?
Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ndiye waziri mkuu kivuli, hivyo anapata
Sasa yote haya uyakose!, hata ningekuwa mimi, ningeomba kanuni zibadilishwe na kupata japo nusu ya marupurupu haya!
- Ofisi pale bungeni Dodoma yenye wafanyakazi 4 na ofisi ndogo Dar es Salaam yenye wafanyakazi 2
- Nyumba ya serikali pale Dodoma yenye watumishi wawili na ulinzi 24/7
- Gari la serikali lenye hadhi, na dereva/bodyguard, mafuta kumwezesha kuzunguka nchi nzima.
- Posho kama ya Waziri Mkuu.
- Ndiye mtu wa kwanza kuulizwa swali kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo.
- Kipaumbele kwenye safari za nje
- etc etc
Kuna nafasi bado ya kambi ya upinzani baraza la wawakilishi, mnaweza kujitoa SMZ mkawa wapinzani rasmi.
Ni lazima uchague kuwa baridi au moto, Huwezi kusimama katikati!!!
Amaizing kama wanataka ndoa na CDM wavunje kwanza ndoa yao na CCM huko zanzibar nafikiri CDM watabase kwa hilo.CUF ina ndoa na CCM, mbona wanataka kuolewa tena na Chadema?!!!!!!!!!!!
Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ndiye waziri mkuu kivuli, hivyo anapata
Sasa yote haya uyakose!, hata ningekuwa mimi, ningeomba kanuni zibadilishwe na kupata japo nusu ya marupurupu haya!
- Ofisi pale bungeni Dodoma yenye wafanyakazi 4 na ofisi ndogo Dar es Salaam yenye wafanyakazi 2
- Nyumba ya serikali pale Dodoma yenye watumishi wawili na ulinzi 24/7
- Gari la serikali lenye hadhi, na dereva/bodyguard, mafuta kumwezesha kuzunguka nchi nzima.
- Posho kama ya Waziri Mkuu.
- Ndiye mtu wa kwanza kuulizwa swali kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo.
- Kipaumbele kwenye safari za nje
- etc etc
Amaizing kama wanataka ndoa na CDM wavunje kwanza ndoa yao na CCM huko zanzibar nafikiri CDM watabase kwa hilo.
Hamad angefanya jitihada za ziada ili kupata wabunge wengi CUF aendelee kubaki kuwa kiongozi wa upinzani sio kubweteka, si aliona CHADEMA walivyochacharika.. sasa kapoteza kiti kihalali kabisa then anaanzisha siasa za maji taka... Angekuwa mjanja alivyoona kuna kila dalili Chadema kuwapita CUF kwa wingi wa wabunge angejiunga chapchap na Chadema labda angeambulia uasistant!!!!!.Tehe teh!! Kaazi kwelkweli..:clap2: