Hamad Rashid amesahau 1995 - 2000? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hamad Rashid amesahau 1995 - 2000?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MushyNoel, Jan 27, 2011.

 1. M

  MushyNoel Senior Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 104
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hamad Rashid alikuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ( bunge la tisa) 2005-2010.Kwa wakati huu wa bunge la kumi ambapo Chadema wamepata uhalali wa kikanuni wa kuunda kambi ya upinzani bungeni kwa kufikisha asilimia 12.5% ya wabunge wote bado Hamad Rashid anajaribu kujenga mazingira kwamba ni lazima kambi hiyo iwe ya wote.

  Kwamba ule uhalali wa CDM kuunda kambi hiyo sasa unakuwa ni lazima na wengine.

  Mwaka 1995 kuelekea 2000 CUF waliunda kambi ya upinzani bungeni wakishirikiana na UDP waliokuwa na wabunge 4 ili kwa kuwahusisha na wa UDP wafikie asilimia 12.5% kama taratibu zinavyosema. Waliwaacha NCCR nje tena NCCR mageuzi walikuwa na wabunge 28.

  Ni vizuri CUF wakaelewa kwamba kwa sasa (2005-10) CDM ndio wenye haki ya kuunda kambi ya upinzani bungeni.
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,575
  Trophy Points: 280
  Kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni ndiye waziri mkuu kivuli, hivyo anapata
  1. Ofisi pale bungeni Dodoma yenye wafanyakazi 4 na ofisi ndogo Dar es Salaam yenye wafanyakazi 2
  2. Nyumba ya serikali pale Dodoma yenye watumishi wawili na ulinzi 24/7
  3. Gari la serikali lenye hadhi, na dereva/bodyguard, mafuta kumwezesha kuzunguka nchi nzima.
  4. Posho kama ya Waziri Mkuu.
  5. Ndiye mtu wa kwanza kuulizwa swali kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo.
  6. Kipaumbele kwenye safari za nje
  7. etc etc
  Sasa yote haya uyakose!, hata ningekuwa mimi, ningeomba kanuni zibadilishwe na kupata japo nusu ya marupurupu haya!
   
 3. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Msg delivered!
   
 4. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  umefunga mjadala!!!
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kumbe ndiyo maana mpemba amechanganyikiwa! CDM wasikubali kuungana naye mpaka amewaomba msamaha hadharani.
   
 6. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mafweza hayo udenda unamtoka
   
 7. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,261
  Likes Received: 852
  Trophy Points: 280
  Wacha cdm tule raha ila kazi ya ukweli izidi kufanyika, cuf you had your time now it's no more, nyinyi si mna share na ccm kuleni vya ccm
   
 8. s

  smz JF-Expert Member

  #8
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 251
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama kiongozi wa Kambi ya upinzani anapata marupu rupu yote hayo, ni wazi Hamad inamuuma, inauma kuyakosa. Hata hivyo akumbuke kwamba amefaidi miaka yote 5 iliyoisha.

  Kutesa kwa zamu ndugu yangu. Mangi mambo yake yamenyooka na iko wazi kabisa, uongozi ni kama mbio za kupokezana kijiti. This time ni CDM
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Now I get it!
   
 10. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #10
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,510
  Likes Received: 5,741
  Trophy Points: 280
  UNAJUA UKISOMA KWENYE BAIBO HAYA MAMBO YALISHAANDIKWA KOR 5:19-23
  ULAFI ULAFI WAKO WATU WA MUNGU WENGI WALAFI PASIPO JIJUA YAANI MATUMBO YAO
  AYASEMI IMECHOKA..TUNAITJ KUSEMA IMETOSHA..WEWE KILA SEHEMU WEWE .MWENYEKITI WA MTAA,BODI,,SHULE,KANISANI,LOH UCHOKI...

  NARUDI KWA NDUGU YANGU HUYU MH HAMAD RASHID RAFIKI YANGU MKUBWA KWA KWELI KWANZA ANAJIAMINI LAKINI UPANDE MWINGINE KAMA BIN ADAM ANA MAPUNGUFU YAKE MENGI NAAMINI MUDA UMEFIKA WA KUREKEBISHA..HAMAD RASHID AMEKUWA MUDA WOTE AKIGOMBANIANA NA MBOWE KUHUSU KUONGOZA UPINZANI BUNGEN LAKINI MPAKA MBOWE ALIPOTUFUMBUA KUMBE ANAGOMBANIA SHANGINGI,,NYUMBA MASAKI..NA MENGINE MENGI TUYA POSHO AKUYAMALIZIA..

  KWA MNAOMWONA GARI AANAYOTEMBELEA MBOWE KWA KWELI NIMEWIWA KUELEWA KWA NINI JAMAA ALIKUWA AKIGOMBANIA WATU WAACHE SHERIA ZA BUNGE NA KUMFWATA YEYE

  MASKINI JANA SPIKA AKAMMALIZA KABISA SASA BASI UPINZANI N MMOJA TU ATI LEO ANATAKA WAPINZANI WASHIRIKIANE ..WAKATI WA KUPIGA KURA MKAJITENGA,,,WAKATI WABUNGE WA CHADEMA WANAONDONKA MKO BUNGEN ENDELEENI KUKAA MISUKULE YA CCM HIVYO HIVYO MPAKA MWISHO WA BUNGE OK...

  ONYO

  MBOWE MARUFUKU KUWASHIRIKISHA HAWA WATU KWENYE UWAZIRI PINZANI..HAWA AKUNA TOFAUTI NA SUMU ...WALIKUWA WAKITISHIA UPINZANI ATI WATAKIONA CHADEMA KWENYE MAAMUZI KAMA WATAKIONA LEO HII UNATAKA WASHIRIKIANE NA WEWE KAMA NANI,...

  Dearest
  HAMAD UMEFIKA WAKATI HATA KAMA ULILEWA MADARAKA MZEE WANGU HUWA YANABADILIKA SAME CCM IKO LEO KESHO CHADEMA CUF WANARUDI MADARAKANI....SO UWE NA KIPIMO NDUGU ZANGU WAKRISTO WANASEMA ULAFI UARIBU UMBO LAKO..SITAKI NIFIKE UKO KAMA UKINLAZIMISHA

  NAWATAKIA BUNGE JEMA WOTE MSIWE WAHUDHURIAJI BALI WATENDAJI
   
 11. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #11
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kumbe!Ndio maana inamuuma na anataka waungane
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Jan 27, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  CUF imo ndani ya serikali ya CCM kule Zanzibar na Maalim Seif ni Makamu wa Kwanza wa Rais. Hadhi ya CUF kuendelea kuitwa wapinzani upande mmoja wa Muungano ni kichekesho kama sio dhihaka kwa siasa za ushindani!
   
 13. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #13
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kumbe vurugu zote ni kwa sbb kuna mafungu ya maana!
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yaani siasa za bongo sometimes ni kichekesho tu!!!!!!!!!!
   
 15. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #15
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,214
  Likes Received: 3,626
  Trophy Points: 280
  Pasco;

  Kiongozi wa Upinzani Bungeni anapata tena bure kabisa BIMA NONO YA AFYA nchini TZ au hata huwa hamna usumbufu kabisa kwake tofauti na Mbunge wa kawaida kama ataamua kwenda nje ya nchi kupata matibabu ya afya yake!

  Pia kidemokrasia ndiye anayepaswa kutaarifiwa kwanza na serikali iliyopo madarakani mambo muhimu yanayohusu dola ya Bunge ikiwemo ni lini na saa ngapi Rais atafika kulihutubia Bunge.

  Mkuu wa Upinzani Bungeni sehemu yeyote duniani ina ulaji sana hata sikushangaa kabisa kusikia Mbunge Hamad wa CUF bado anaitolea udenda nafasi hii!
   
 16. Offish

  Offish Senior Member

  #16
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 172
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nawashangaa Kafulila na wenzake kukomalia hilo nyuma ya Hamad, ondokeni huko kama mko serious. Vinginevyo wananchi watawahukumu come 2015!!! Acheni siasa za majitaka za akina Mmbatiaa et al..........
   
 17. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #17
  Jan 27, 2011
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  2009 nikiwa Pemba wadau walinijulisha kwamba jamaa kaongeza mke kigoli, mayb aliproject kwamba ataendelea kuwa mkuu wa kambi ya upinzani,sasa mambo yameanza kwenda kombo anatafuta pa kutokea....
   
 18. Don Alaba

  Don Alaba Senior Member

  #18
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 158
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ukweli mtupu
   
 19. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #19
  Jan 27, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Sasa nimeelewa kwa nini jamaa kichwa chake hakitulii!
   
 20. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #20
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Daaaah,maskini hamad atakondaaa,,....kumbeeee
   
Loading...