Kaka we kusoma hujui hata kuona huoni? Hivi rangi za kuweka kwenye bendera ziliisha mpaka zile bendera zao zifanane na CDM? Unajua kule bush wengi wao hawajui kusoma. Sasa wao dhumuni lao kubwa ni kuwachanganya watu kwenye hilo hasa katika karatasi za kupigia kura.
Ila uzuri wabongo kiasi flan wanajua pumba na mchele siku hizi.
Limbu, Saidi Miraji(Alikuwa kiongozi wa Cuf na kampeni manager wa Lipumba 2010), Hamad Rashid(Yeye ni mlezi wa ADC japo yupo Cuf kwa zuio la mahakama!!)Viongozi wake ni kina nani?
Mwacheni apumzike Hamad Rashid, kafiwa na mkewe juzi juzi tu
Nina jirani yangu ni mkereketwa na nadhani ni kiongozi wa ADC pia, kwa masikio yangu siku moja akiwa anaongea na mwenzie kwenye simu alisema; "bado tupo busy na kanda ya ziwa, sehemu ambayo CHADEMA wanajifanya kuweka nguvu kubwa, tunahitaji kuwabomoa na kisha twaja huko Kigoma kuiendeleza kazi".
haka kanchi kana watu wanaendekeza njaa kupita kiasi..no wonder watu kutoka ughaibuni wanaendelea kuiteka hii nchi,wasaliti wengi sana..
Kama unajua kuwa adc ni zao lililo tawanywa kutoka ccj basi hutapata tabu kuandika mengi maana tabia ya mbegu ya mazao huzaa. Ccj imezaa adc, adc nayo itazaa baadae.
Chadema wafadhiliwa na ujerumani.ukweli hatuna wapinzani wa kweli bali tunao waganga njaa