Hamad Rashid alipewa pesa na CCM kuanzishia ADC - Limbu

Mbalinga

JF-Expert Member
Apr 9, 2010
1,712
2,000
Wana JF Katibu Mkuu wa chama kipya cha ADC leo amenipa siri ya uanzishwaji wa ADC nikabaki ninashangaa. Anadai kuwa Mh Hamad alikwenda kuomba pesa kwa CCM kwa ajili ya mchakato wa kuanzisha chama na akapewa kwa masharti kuwa baadhi ya hao waanzilishi awaondoe mara watakapopata usajili wa kudumu. Baada ya kupata huo usajili Hamad ambaye ndiye mlezi wa ADC akafanya jaribio la kuwaondoa hao viongozi akakumbana na upinzani mkali sana. Lakini ndiyo hivyo tena wameshalamba pesa za CCM. Baada ya kupata habari hii nikatafakari yafuatayo:

1. Bendera ya ADC: Kwa makusudi waliamua kutengeneza bendera inayo shabihiana na ya CHADEMA. Kumbe huu ulikuwa makakati wa makusudi kuivuruga CHADEMA.

2. Harakati za ADC kanda ya Ziwa hasa Mwanza. Bw Limbu aliwahi kuniambia kuwa wanakwenda kuvunja ngome ya CHADEMA, nikamuuliza kwani CHADEMA ni chama tawala? lengo lenu ni kuingia Ikulu ama kuivunja CHADEMA? Je mkivunja ngome ya CHADEMA itawasaidia nini kama ADC? Na je kama mnapmbana na CHADEMA tukiwaita nyie watoto wa CCM tutakuwa tunakosea. Badala ya kujibu hayo maswali alifoka kweli kweli.

Nikagundua katika safari ya ukombozi wasaliti ni lazima wawepo. Wana mapinduzi tusikate tamaa, vita hii si yetu ni ya Mungu, na yeyote atakayezuia harakati hizi atakuwa anapambana na Mungu mwenyewe. Haiwezekani Tanzania ikaendelea kuhujumiwa na wana CCM wachache kwa faida yao kwa gharama ya mamilioni ya watanzania walala hoi halafu Mungu akaa kimya muda wote.

Ifahamike kuwa ADC ni CCM iliyokuja kubomoa CHADEMA NA CUF.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Jallen

JF-Expert Member
Mar 31, 2012
516
225
ADC ni CCM iliyokuja kwa mlango wa uani, wachambuzi wa mambo tulijua mapema!!
 
malaka

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
1,328
1,500
Kaka we kusoma hujui hata kuona huoni? Hivi rangi za kuweka kwenye bendera ziliisha mpaka zile bendera zao zifanane na CDM? Unajua kule bush wengi wao hawajui kusoma. Sasa wao dhumuni lao kubwa ni kuwachanganya watu kwenye hilo hasa katika karatasi za kupigia kura.

Ila uzuri wabongo kiasi flan wanajua pumba na mchele siku hizi.
 
Dec 11, 2010
3,321
0
Kama unajua kuwa adc ni zao lililo tawanywa kutoka ccj basi hutapata tabu kuandika mengi maana tabia ya mbegu ya mazao huzaa. Ccj imezaa adc, adc nayo itazaa baadae.
 
Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
0
Mkuu kwani
1/Tayari hichi chama ADC kimepata usajili wa kudumu?

2/Ile bendera yao
inayofanana na ya Chadema hawajaibadilisha bado?
 
Safari_ni_Safari

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
23,285
2,000
Kaka we kusoma hujui hata kuona huoni? Hivi rangi za kuweka kwenye bendera ziliisha mpaka zile bendera zao zifanane na CDM? Unajua kule bush wengi wao hawajui kusoma. Sasa wao dhumuni lao kubwa ni kuwachanganya watu kwenye hilo hasa katika karatasi za kupigia kura.

Ila uzuri wabongo kiasi flan wanajua pumba na mchele siku hizi.

Mkuu hapo kuna mkanganyiko.....hebu rekebisha kidogo
 
Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,460
2,000
Mwacheni apumzike Hamad Rashid, kafiwa na mkewe juzi juzi tu
 
Felixonfellix

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
1,672
1,250
Nina jirani yangu ni mkereketwa na nadhani ni kiongozi wa ADC pia, kwa masikio yangu siku moja akiwa anaongea na mwenzie kwenye simu alisema; "bado tupo busy na kanda ya ziwa, sehemu ambayo CHADEMA wanajifanya kuweka nguvu kubwa, tunahitaji kuwabomoa na kisha twaja huko Kigoma kuiendeleza kazi".
 
nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
15,108
2,000
haka kanchi kana watu wanaendekeza njaa kupita kiasi..no wonder watu kutoka ughaibuni wanaendelea kuiteka hii nchi,wasaliti wengi sana..
 
Aggrey86

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
853
195
Nina jirani yangu ni mkereketwa na nadhani ni kiongozi wa ADC pia, kwa masikio yangu siku moja akiwa anaongea na mwenzie kwenye simu alisema; "bado tupo busy na kanda ya ziwa, sehemu ambayo CHADEMA wanajifanya kuweka nguvu kubwa, tunahitaji kuwabomoa na kisha twaja huko Kigoma kuiendeleza kazi".

Dah! Yani kuna mambo yanatia hasira jamani ukiyasikia sasa watu mawazo yao ni kupambana na wapinzani wenzao tutafika kweli jamani kama ndo hivyo kweli dah!
 
Aggrey86

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
853
195
haka kanchi kana watu wanaendekeza njaa kupita kiasi..no wonder watu kutoka ughaibuni wanaendelea kuiteka hii nchi,wasaliti wengi sana..

Yani sijui wanataka watupeleke wapi jamani si wengine hatujawahi kufaidi matunda ya nchi hi lol....yani watu wengine mi wananitia gadhabu tu hivi ipo siku kweli tutakuja kutoka hapa tulipo kweli kama watu wazima na akili zao bado hawajui kama tunaibiwa jamani!
 
SaidSabke

JF-Expert Member
Sep 28, 2006
2,071
1,500
Chadema wafadhiliwa na ujerumani.ukweli hatuna wapinzani wa kweli bali tunao waganga njaa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom