Wana JF Katibu Mkuu wa chama kipya cha ADC leo amenipa siri ya uanzishwaji wa ADC nikabaki ninashangaa. Anadai kuwa Mh Hamad alikwenda kuomba pesa kwa CCM kwa ajili ya mchakato wa kuanzisha chama na akapewa kwa masharti kuwa baadhi ya hao waanzilishi awaondoe mara watakapopata usajili wa kudumu. Baada ya kupata huo usajili Hamad ambaye ndiye mlezi wa ADC akafanya jaribio la kuwaondoa hao viongozi akakumbana na upinzani mkali sana. Lakini ndiyo hivyo tena wameshalamba pesa za CCM. Baada ya kupata habari hii nikatafakari yafuatayo:
1. Bendera ya ADC: Kwa makusudi waliamua kutengeneza bendera inayo shabihiana na ya CHADEMA. Kumbe huu ulikuwa makakati wa makusudi kuivuruga CHADEMA.
2. Harakati za ADC kanda ya Ziwa hasa Mwanza. Bw Limbu aliwahi kuniambia kuwa wanakwenda kuvunja ngome ya CHADEMA, nikamuuliza kwani CHADEMA ni chama tawala? lengo lenu ni kuingia Ikulu ama kuivunja CHADEMA? Je mkivunja ngome ya CHADEMA itawasaidia nini kama ADC? Na je kama mnapmbana na CHADEMA tukiwaita nyie watoto wa CCM tutakuwa tunakosea. Badala ya kujibu hayo maswali alifoka kweli kweli.
Nikagundua katika safari ya ukombozi wasaliti ni lazima wawepo. Wana mapinduzi tusikate tamaa, vita hii si yetu ni ya Mungu, na yeyote atakayezuia harakati hizi atakuwa anapambana na Mungu mwenyewe. Haiwezekani Tanzania ikaendelea kuhujumiwa na wana CCM wachache kwa faida yao kwa gharama ya mamilioni ya watanzania walala hoi halafu Mungu akaa kimya muda wote.
Ifahamike kuwa ADC ni CCM iliyokuja kubomoa CHADEMA NA CUF.
MUNGU IBARIKI TANZANIA