Halmashauri ya mji Kibaha zoezi la Postikodi linahujumiwa

luangalila

JF-Expert Member
Jan 12, 2014
6,325
6,871
Nikiwa kama mkazi ndani ya Halmshauri ya mji huu,

Kiukweli zoezi la postikodi lina hujumiwa licha ya jitihada ya serikali kuwapa taarifa wananchi mara kwa mara juu ya zoezi hili.

Ndani ya halmashauri hii ikiwa leo ni tareh 15 ya mwezi April, kuna kata ambayo sitaitaja zoezi la ukusanyaji wa taarifa za nyumba na kugawa namba bado watendaji wanalipua lipua unakuta nyumba moja imepewa fomu lakini nyumba zingine hazijapewa fomu.

Haieleweki hizi fomu zinatolewa na afisa mwandikishaji postikodi au wananchi wanafuata fomu wenyewe katika ofisj ya kata, yaani in short ni vurugu mechi.


Embu nikaribishe maoni ya wadau toka halmashauri zingine nanyi mseme jambo
 
wasiliana na kiongozi wako wa mtaa, yaani Mwenyekiti wa Mtaa au zamani walikuwa wanajulikana kama Balozi wa nyumba 10, huyo ndiye anawajibika kuwasambazia watu wake hizo Fomu.

Hiyo fomu inaitwa;

"DODOSO LA TAARIFA ZA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI"
 
wasiliana na kiongozi wako wa mtaa, yaani Mwenyekiti wa Mtaa au zamani walikuwa wanajulikana kama Balozi wa nyumba 10, huyo ndiye anawajibika kuwasambazia watu wake hizo Fomu.

Hiyo fomu inaitwa;

"DODOSO LA TAARIFA ZA ANWANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI"
Asante kwa ushauri mzuri japo sitoufuata maana najua izo ni kazi za watu na wanalipwa kwa kazi iyo ...
 
Hata Dar es Salaam huku, hakuna lolote. Mwendo wa kubaaisha tu.

Postikodi huwekwa mahali panapojulikana Street, Plot Namba, na House Namba.

Dar es Salaam asilimia kubwa ya makazi hayajapangwa, ni kila mtu ajijengee anapoona panamfaa. Postikodi nchi nzima ni kutafuna pesa za wananchi bure.
 
Back
Top Bottom