Halima Mdee: Mifuko ya Jamii hoi, pensheni hatihati kulipwa

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
8,829
2,000
May 22, 2020
Bungeni Dodoma
Tanzania

DAKIKA 17 ZA HALIMA MDEE BUNGENI LEO

Mh. Halima James Mdee mbunge wa CHADEMA aichambua taarifa ya CAG aliyepita na CAG mpya ambao wote wameonesha jinsi taasisi kubwa kama Mifuko ya Jamii na National Housing kushindwa kujiendesha.


Mifuko ya Jamii ipo hoi na kuna hatari walengwa wa Mafao kupata tabu kulipwa stahili zao kwa wakati.

Pia shirika la Nyumba National Housing imefika kikomo cha kukopesheka yaani Bilioni 300 tayari shirika limekopa na kisheria haliruhusiwi kukopa na hivyo kushindwa kumaliza miradi yake kama ule wa Kawe jijini Dar es Salaam.

Mradi wa Kawe National Housing waTanzania wengi waliwekesha pesa zao mbele wakitengemea mradi huo wa Kawe ungekamilika na wakaweza kuhamia ktk apartments zinazoangalia fukwe ya bahari ya Hindi. Lakini mradi umesimama na waTanzania pesa hawajarudishiwa.
Source: millard ayo

More Info kuhusu mradi uliokwama:

Muonekano wa mradi wa Kawe ambao umekwama kutokana na National Housing kukaukiwa na pesa pia haliwezi kukopeshwa
Source : NHC Tanzania
 

kinje ketile

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
539
1,000
Dah.....Kamanda wa kike huyu.....sina hakika iwapo atarudi...
Sisi huku mama lishe na machinga tegeta kwa ndevu mbona umetusahau..? Kila siku hoja ni mifuko mifuko...hlf baada hapo unageukia ATCL..hlf tena tunasikia uko kwenye kesi kisutu..ujue barabara zetu zingine hazipitiki...!!
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
746
1,000
CCM na serikali yake wanachukua pesa za wafanyakazi waliotaabika miaka yote kazini wanafanyia mambo yao bila ridhaa ya wenye mali.

Huu ni wizi tu kama ulivyo wizi mwingine wowote, halafu wanajitapa serikali ya wanyonge, sijui wanyonge wa aina gani wanaowazungumzia, watastaafu wanahangaikia mafao yao wengine mpaka wanafariki!

This is not fair.Sent using Jamii Forums mobile app
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
746
1,000
Chadema kwa uzushi ata shetani anawashanga,uzuri watanzania waneshawaona mambumbumbu
Sauti ya zege anajindaa kuachia Jimbo na kashfa

Sent using Jamii Forums mobile app
jimbo la kawe ndo la kwanza kurudi kundini inshallah.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo jimbo mlikuwa nalo kabla hakuna chochote mlichofanya, leo mnalitaka tena, nyie ni sawa na tajiri mpumbavu asiejua kutumia alichonacho kwa manufaa yake na wengine, anajirundikia tu ndani halafu anachekelea tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
23,687
2,000
CCM na serikali yake wanachukua pesa za wafanyakazi waliotaabika miaka yote kazini wanafanyia mambo yao bila ridhaa ya wenye mali.

Huu ni wizi tu kama ulivyo wizi mwingine wowote, halafu wanajitapa serikali ya wanyonge, sijui wanyonge wa aina gani wanaowazungumzia, watastaafu wanahangaikia mafao yao wengine mpaka wanafariki!

This is not fair.Sent using Jamii Forums mobile app
Definition yao ya wanyonge ni tofauti kabisa na wanyonge walioko huku mtaani..
 
Top Bottom