Halima Mdee: Mifuko ya Jamii hoi, pensheni hatihati kulipwa

Usininukuu kirahisi hivyo.
Tunahitaji Chama mbadala na serikali itakayojenga mifumo imara ya Kidemokrasia yenye kujali maendeleo ya watu.
Chadema imenajisiwa na Uroho wa Mbowe kukwepa Demokrasia ndani ya Chama huku akiwatanguliza wenzake kupigania Demokrasia toka kwa Mwenyekiti wa CCM Chama cha Kijamaa kisicho na Demokrasia nje ya Chama lakini ndani ya Chama kiliasisiwa kidemokrasia na kinajitahidi kwa kiwango japo kidogo.

Mbowe angekua na Dola angekuwa ni kama Mungu asiyehojiwa na mtu yeyote mbinguni na duniani.
Hatutaki viongozi kama hao mana ndio wanaozuia watu kuhoji na kudai haki zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
May 22, 2020
Bungeni Dodoma
Tanzania

DAKIKA 17 ZA HALIMA MDEE BUNGENI LEO

Mh. Halima James Mdee mbunge wa CHADEMA aichambua taarifa ya CAG aliyepita na CAG mpya ambao wote wameonesha jinsi taasisi kubwa kama Mifuko ya Jamii na National Housing kushindwa kujiendesha.



Mifuko ya Jamii ipo hoi na kuna hatari walengwa wa Mafao kupata tabu kulipwa stahili zao kwa wakati.

Pia shirika la Nyumba National Housing imefika kikomo cha kukopesheka yaani Bilioni 300 tayari shirika limekopa na kisheria haliruhusiwi kukopa na hivyo kushindwa kumaliza miradi yake kama ule wa Kawe jijini Dar es Salaam.

Mradi wa Kawe National Housing waTanzania wengi waliwekesha pesa zao mbele wakitengemea mradi huo wa Kawe ungekamilika na wakaweza kuhamia ktk apartments zinazoangalia fukwe ya bahari ya Hindi. Lakini mradi umesimama na waTanzania pesa hawajarudishiwa.
Source: millard ayo

More Info kuhusu mradi uliokwama:

Muonekano wa mradi wa Kawe ambao umekwama kutokana na National Housing kukaukiwa na pesa pia haliwezi kukopeshwa


Source : NHC Tanzania

Huyu dada ni moja ya wAbunge waliohangaikia sana amani ya maisha yao! Inatia huruma. Mungu atamsimamia! Hata akikosa Ubunge, Mungu atamfungulia njia pengine!
 
Mkuu una hoja ya uhakika. Mbowe angetoka mwaka huo akaruhusu damu mpya asingekuwa anapata shida hizi. Mwaka jana aliogopa kutoka kwa sababu aliona akitoka watasema anakimbia baada ya kuona chombo kinaenda mrama; akajiapiza kwamba wacha kimfie tu. Kweli naona CHADEMA kinakata roho mikononi mwake.
CHADEMA ilikuwa na historia nzuri ya kurithishana madaraka kuanzia Mzee Mtei na Bob Nyanga Makani. Pia akina Mzee Brown Ngwilulupi. Alivyoingia Mbowe sijui kabadili Makamo Wenyeviti wangapi? Makatibu wangapi lakini YEYE YUPO! Kamkuta Kabourou, kaondoka yeye yupo! Kaja Slaa kaondoka Mboqe yupo! Kaja Mashinji katoka Mbowe yupo!!! Chacha Wangwe, kaja kaondoka; MBOWE YUPO! Mzee Arfi kaja kaondoka, MBOWE YUPO! Kaja Prof Safari kaondoka, MBOWE YUPO!! Lowassa kaja kaondoka, Mbowe yupo! Sumaye kapita, Mbowe YUPO!
Nimecheka sana.
Na Mimi sina shaka na uzoefu wake??
Awamu ya tatu imepita Mbowe yupo!
Awamu ya nne Mbowe yupo!
Ya Tano ,yupoo!!
Nachoka kabisa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom