Halima Mdee amsambaratisha Magufuli

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mwenyekiti wa BAWACHA Taifa Halima Mdee jana alitikisa Jimboni Chato kwa kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara kuwahi kuhutubiwa jimboni hapo miaka ya karibuni.

Awali Mdee alilakiwa na umati mkubwa wa watu wakiwa na msururu mrefu wa magari,pikipiki,baiskeli huku akina mama wakiwa kandokando ya barabara wakipunga matawi ya miti.

Ujumbe mkubwa wa Halima Mdee kwa wanaChato ni kuikataa Katiba Haramu ya CCM na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Halima Mdee maarufu kama Tanzanian Iron Lady alipokea kadi 200 za watu walioamua kujitoa CCM na kujiunga Chadema.Huku mamia ya wananchi wengine ambao hawakuwa na chama wakijiunga pia Chadema.

Ikumbukwe jimbo la Chato linaongozwa na mbunge wa CCM John Pombe Magufuli ambaye ni waziri wa Ujenzi.

Ni simulizi hapa Chato kuanzia jana mpaka asubuhi hii kumzungumzia Halima Mdee na Chadema!

1658198_658862364212406_8498540439566593170_o.jpg

10612779_658862337545742_528341973315421299_n.jpg

10407380_658862304212412_6823844216364614988_n.jpg

10669105_658862190879090_1474681969313438198_o.jpg
 
Mkuu Molemo tupia basi picha za watu hao walihudhuria mkutano pamoja na akina mama ambao walikuwa wakipunga matawi njiani.

Picha huongea zaidi kuliko maneno.
 
Last edited by a moderator:
We masauti nadhani akili zako ziko matakoni kwanini asitoke yeye ninani,
hakuna utawala wa milele kwanini mnakuwa na akili mgando tena za kipumbafu.watanzania tumeamka haki kwa wote.
 
Kwa Chato siwezi kushangaa kwani jamaa hakubaliki na hana ushawishi tena kutokana na mabavu yake ktk kila kitu.
 
Kati ya hao walioshiriki mkutano ni wangapi wapo tayari kupiga kura? Bado na sisitiza kinachowafanya watu wajae kwenye mikutano hii ni ukosefu wa ajira. Watu wangekuwa na kazi usingewaona wakijaa kwenye viwanja hivi kusikiliza watu waliopo kwenye kazi zao.
 
Nakushauri na wewe ukafanye mkutano wako huko Chato alafu tuwaone hao wasiokuwa na ajira wakijitokeza.
 
Kati ya hao walioshiriki mkutano ni wangapi wapo tayari kupiga kura? Bado na sisitiza kinachowafanya watu wajae kwenye mikutano hii ni ukosefu wa ajira. Watu wangekuwa na kazi usingewaona wakijaa kwenye viwanja hivi kusikiliza watu waliopo kwenye kazi zao.
jipe moyo, nmeshuhudia kwa macho yangu watu wanafunga maduka wanawah kucklza mkutano wa chadema
 
Back
Top Bottom